Ona jinsi watu walivyo wepesi wa kupima madhaifu ya wenzao

07:08:00 Unknown 0 Comments



Kulikuwa na mkulima mmoja ambaye yeye alifuga ng'ombe na kutengeneza siagi ambazo aliziuza kwa watu wa eneo lake na miongoni mwa watu hao pia kulikuwa na muuza mikate mmoja aliyekuwa akizinunua siagi zeile.

Muuza mikate alikuwa akinunua kilo moja ya siagi kila siku kutoka kwa mkulima huku mkulima nae akinunua kilo moja ya mkate kila siku kutoka kwa muuza mikate.

Siku m oja muuza mikate baada ya kufika nyumbani kwake akaamua apime siagi ile kuhakikisha kama kweli ni kilo moja.


Alipoipima siagi ile haikuwa na uzani wa kilo moja hivyo kwa hasira akampeleka mkulima yule mahakami.

Hakimu akamuuliza yule mkulima, "je unakipimo ambacho hutumia kupima siagi zako kujua kama zina kipimo sawa?"

Mkulima akajibu, Hapana mheshimiwa mimi ni mkulima maskini na sina uwezo wa kununua kipimo hicho cha gharama ila huwa natumia kipimo cha asili. 

Kipimo gani hicho? hakimu aliuliza

Kila siku mimi huwa na nunua kilo moja ya mkate kutoka kwa muuza mikate huyu, hivyo mimi kwa kuwa huamini ile ni kilo kamili kama makubaliano yetu yalivyo, basi nami hutumia mkate ule kuuweka katika chombo kingine na siagi chombo kingine na kisha kuwianisha na vikilingana humpa siagi yake.

Hivyo kama kuna mtu wa kulaumiwa ni huyu muuza mikate kwani yeye atakuwa hakunipa kipimo sahihi.

Funzo gani twapata hapa

Katika maisha twapata vitu sawa na vile tunavyovitoa kwa wengine.


Kwa kila fedha au malipo utoayo hebu jiulize unatoa sawa na ambavyo ungetegemea kupokea? Kuwa mkweli au kutokuwa mkweli hujijenga na kuwa tabia.

Kuna watu wanadanganya na kuhakikisha mambo yanakuwa vile watakavyo kwa kushuhudia uonge ili mradi wafanikie, lakini nani wanamdangaya zaidi ya kujidanganya wenyewe?

You Might Also Like

0 comments: