Sala nzuri na usiyotakiwa kuikosa kwa asabuhi hii na siku hii mpya

06:46:00 Unknown 0 Comments


Moyo wenye shukrani ndio unaouhitaji kuuomba kutoka kwa MUNGU wako asubuhi hii. 

Wakati unashukuru kwa kila kitu ulichobarikiwa kuanzia afya , kazi zako, familia na kila kitu, unatakiwa kumshukuru MUNGU kwanza na sio mtu mwingine.

Mambo yanapoenda tofauti na vile ulivyopanga ifunge mikono yako na kumwomba MUNGU akupe ujasiri wa kuyafanikisha yaende sawa. 

Wakati una amani na furaha zidi kumshukuru MUNGU wako kimya kimya huku ukimwomba akuzidishie baraka,  kwani bila hivyo anauwezo wa kuvinyang’anya pia.

Unavyomshukuru na kuwaweka maadui zako mikononi mwake hakikisha huombi kulipiza visasi, ila omba awabadilishe na waone umuhimu wako kwani MUNGU wetu ni wa watu wote na sio wa visasi.

Wakati mambo yanazidi kuwa tofauti zaidi na uelewa wako muombe MUNGU akupe busara na uvumilivu wa kuyashinda majaribu hayo vinginevyo siku yako itakuwa mbaya zaidi.

Kuna wakati utapata mahitaji yako haraka kuliko ulivyotegemea, mshukuru MUNGU kwani bila yeye plani zako ni sawa na bure.

Kuna wakati unamwomba MUNGU vitu ambavyo ungependa uwe navyo na vinachelewa, jitahidi kuwa mvumilivu MUNGU anajua muda muafaka wa wewe kuwa na hivyo vitu.

Hata kama una matatizo mengi kama vile umasikini, magonjwa na mengine Mengi, zidi kumshukuru MUNGU na kujituma kwani kila baada ya mvua kali upinde wa mvua hutokea kuashiria neema

Usimchangulie MUNGU Baraka uzitakazo bali omba mkono wake ubariki kila utakachokifanya na kuwa na matokeo mzuri

Utakaponusurika katika jaribu lolote baya mshukuru MUNGU haraka na ukilitaja jina lake kwa furaha kwani yeye ni MUNGU wa ushindi

Ikifika kipindi unahitaji kumwomba MUNGU kitu na ukajikuta unashindwa cha kusema, tadhadhali sema au Andika ,"ASANTE, MUNGU KWA KILA ULICHONIPA"

Sala hii fupi itatosha kuibariki siku yako na kuwa ya Baraka. 

Hivyo mshukuru MUNGU kila wakati na jitahidi kumshukuru kwa hali ya upekee kama yeye akupavyo baraka zake kiupekee pia.

AMEN

You Might Also Like

0 comments: