Basi baba akawaamuru waichukue ile shela na kwenda kuifukia.

05:26:00 Unknown 0 Comments

Ni ndefu ila poteza dakika zako tano kuisoma

Kulikuwa na mzee mmoja ambaye alikuwa tajiri sana, Mzee huyu alibahatika kuwa na binti mmoja na ambaye alimpenda sana na
hata kumwandika kuwa mrithi wa mali zake zote pindi mzee atakapoiaga dunia.

Siku moja mzee huyo alipata taarifa kuwa binti yake alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
kijana mmoja wa familia isiyojiweza kabisa, na wazazi wake walikuwa wakifanya kazi katika
moja ya mashamba ya tajiri huyo.

Yule tajiri alijawa na hasira kwani kwake ile ilikuwa ni fedhea kwa familia yake hivyo akamwuita binti yake na alipomuuliza binti
yake alikubalia, mzee kwa hasira akawafukuza wale wazee na kuahidi kutoa fedha nono kwa
polisi yeyote atakaye mtia mbaroni kijana Yule.

Basi kijana yule ikabidi amfuate binti na kumwambia hali halisi na kuwa sasa wazazi wake wako katika hali mbaya na yeye anasakwa hivyo ni vyema wakiachana maana
anaona Maisha yake yapo hatarini pamoja na familia yake.

Binti Yule akawa akiiba fedha na kuwapelekea wazee wale ili wajikimu na baadae akamshauri
Yule kijana kuwa wakimbie waende mbali wakajifiche na kuanza Maisha yao wakiwa kamamme na mke.

Baada ya mabishano ya siku kadhaa Yule kijana akakubali na binti akachukua fedha nyingi za kuweza kuanza Maisha popote pale watakapoamua kuishi na
kuukimbia mji.

Yule tajiri alipatwa na butwaa na hakuamini kama binti yake kakimbia, akaamua kuwachukua wazazi wa Yule kijana na
kuwafunga bila mafanikio na kuamua kuwaachia huru.

Mkewe na Yule tajiri
aliendelea kuhuzunika na kunung’unika kwa muda wote mpaka mmewe akaamua kutoa
Tangazo kwenye magazeti ya nchi ile na kusema amemsamehe mwanae hivyo arudi tu na ameafikiana nao kuwa waoane.

Hivyo warudi kwa ajili ya harusi.
Taarifa zikamfikia Yule kijana akiwa na mpenzi wake Yule mtoto wa tajiri, kwa pamoja wakaamua kurudi na wakapokelewa na mzee
na akawaambia kuwa watafunga harusi mapema wiki itakayofuata na gharama zote zitakuwa zake na Yule kijana atashirikiana na Yule binti katika kusimamia mali za Yule mzee.

Siku tatu baadae wakaamua waende kuandaa suti na shela kwa ajili ya harusi, waingia kwenye duka la nguo za harusi binti alivaa
shela ikawa imemkaa safi sana na Yule kijana naye suti ilimfaya aonekane maridadi sana,
akaamua kabla ya kuvua ile nguo avuke barabara aende ng’ambo ya pili akanunue ice cream maana binti Yule alikuwa anapenda
sana kula ice cream.

Baada ya kuinunua ice cream na anavuka barabara arudi pale kwa mpenzi wake gari likamgonga Yule kijana na Yule binti baada ya
kuona vile alimkimbilia na alipofika pale damu iliruka na kutengeneza doa kwenye ile shela, wakamchukua na kwenda nyumbani ambako baadae mazishi yalifanyia.

Baada ya mazishi binti Yule aliendelea kuhuzunika na hakutoka
ndani kabisa.

Siku moja baada ya miezi kadhaa kupita usiku
akiwa kalala alimtokea bibi mmoja na kumwambia katika ile shela kuna doa la damu hivyo anatakiwa alifue litoke au balaa litamtokea.

Yule binti kweli asubuhi aliamka na
kwenda kuitazama ile shela na kukuta ina doa, akafua sana mpaka doa akaona limeoptea.

Lakini alipolala tena Yule bibi akamtokea tena na kumwambia lile doa halijatakata hivyo afue
tena au balaa itaikumba familia yake.

Siku ya pili akaamka na kufua lakini kila alipofua Yule bibi alimtokea na kumwambia vile viele,Yule binti akaona sasa kachoka ni vyema amshirikishe mama yake. Mama yake akashangaa sana kwani naye aliota ndoto kama ile ile na alikuwa akiogopa kuwashirikisha.

Mama na mtoto wakafanya siri
na kulifua tena lile shela na hata baada ya kulifua Yule bibi aliwatokea tena na kuwaambia kuwa bado doa lipo.

Mmmh kazi ikawa ngumu ikabidi
wamshirikishe baba, baba naye kumbe amekuwa akitokewa na Yule bibi na na akawa anaona sio vyema kuwashirikisha wanafamilia.

Basi baba akawaamuru waichukue ile shela na kwenda kuifukia. Baada ya kuifukia Yule bibi

aliwatokea na kipindi hiki alikuwa mkali zaidi na kuwaambia wana siku mbili tuu za kulifukua ile shela mpaka doa litakate la sivyo kuna jambo kubwa litawatokea .

Familia nzima walilifua kwa ushirikiano na wakakubaliana kuwa sasa limetakata na
wakalianika na kulipiga pasi baada ya kukauka na uliweka sandukuni.

Usiku wakiwa wamelala
waliambiwa wameshindwa.Basi familia siku ya pili walikutana na kusimuliana wote wakaonyesha kuota ndoto sawa.

Siku ya pili wote wakaenda kazini na kumwacha Yule binti akiwa nyumbani peke yake.

Akiwa kakaa peke yake na huku akisubiri mwisho wake na akilia kwa uchungu na kumkumbuka mchumba wake,mara mlango
ukagongwa na baada ya kumkaribisha binti Yule alistaajabu kuona ni Yule yuel bibi mzee
ambaye amekuwa akiwatokea usiku.

Lakini mara hii alikuwa kashika kopo dogo mkononi na kumpavyule binti kisha akaondoka zake.

Je unafikiri Yule bibi kizee alimpa kopo la nini?

Jibu ni kuwa alimpa kopo la sabuni ya unga aina ya OMO ambayo hutoa madoa kwa uhakika

Weka tangazo bure katika blog hii Whatsapp 0713317171

You Might Also Like

0 comments: