Ebola ni ugonjwa wa kuogofya kwa sasa kwakuwa hauna tiba wala chanjo na husambaa kwa kasi sana. Hofu hii isitufanye tukawa watoa taarifa za kupotosha kwenye jamii.

10:06:00 Unknown 0 Comments



Ebola ni ugonjwa wa kuogofya kwa sasa kwakuwa hauna tiba wala chanjo na husambaa kwa kasi sana. Hofu hii isitufanye tukawa watoa taarifa za kupotosha kwenye jamii. Kama mwanahabari au mwanajamii jihadhari na utoaji taarifa za kubuni kwa jambo la hatari namna hii. Wenye mamlaka ya kusema ni wataalamu wa afya na mamlaka zinazohusiana nazo. 

Kwa sasa kila mgonjwa mwenye dalili zenye utata anapewa uangalizi mkubwa ili endapo ni kweli wasiambukize wauguzi katika harakati za uchunguzi lakini pia ugonjwa usisambae. Katika hali kama hiyo unakuta wagonjwa wanaohofiwa huwekwa katika mazingira yaliyotengwa. 

Sasa ukiona au kusikia taarifa kuhusu hatua hizi isitafsiriwe kuwa tayari ugonjwa umeingia Tanzania. Speculation kama hizi zilitumika Rwanda ilipomuweka mwanafunzi wa Udaktari raia wa Ujerumani aliyekuwa akitokea Liberia katika mazingira ya uchunguzi wa afya kutoa taarifa za kupotosha hadi jamii ya kimataifa ikafahamu kuwa Rwanda imepatwa na ugonjwa huo kumbe si kweli ilikuwa hatua za uchunguzi tu. 

Taarifa kama hizi ina madhara makubwa kwa taifa letu hasa kwa sekta ya kitalii kwakuwa watu wataanza kuogopa kuja Tanzania wakihofia Ebola. Pia mfahamu kuwa si kila mtu katika nchi za Ulaya, Asia na Amerika anafahamu Jiografia ya Afrika. 

Akisikia nchi moja ya Afrika ina Ebola yeye anafikiria Afrika yote imepatwa na Ebola kwa dhana kuwa Afrika ni nchi moja. Kumbe Afrika ni bara na siyo nchi moja au vijinchi vidogo kama visiwa vilivyokaribiana. Raia moja hapa nchini alikwenda Tanzania kwa shughuli zake aliporudi nikakutana naye nikamuliza vipi safari yako umefurahia Tanzania? 

Jibu lake la kwanza akasema anamshukuru Mungu amerudi salama hajaambukizwa Ebola. 

Hii ilinistua sana nikaelewa kwamba uelewa wa watu kuhusu Afrika ni mdogo sana. Kwa dhana hii na kama mwanajamii nashauri wanajamii tuwe makini sana kukuza taarifa zisizothibitishwa na mamlaka husika. 

Pia kila mtu asiwe mzungumzaji wa mambo usiyofahamu kiundani. Ila tuzingatie hadhari zinazotolewa na vyombo vyetu vya afya na kuhusu namna ya kutoa taarifa kwa vyombo husika endapo tutatilia mashaka dalili za Ebola miongoni mwa wanajamii. Wanahabari utoaji wetu wa habari ulenge kuelimisha jamii yetu kuhusu ugonjwa huu ila isiwe kwa namna ya kuwatisha wananchi na kwa mrengo wa ushabiki. 

Tuzingatie maadili ya taaluma yetu na zaidi tutawaliwe na uzalendo kwa Taifa letu. Mungu ibariki Tanzania iepushe na Ebola. 

Burra, Tokyo, Japan.

You Might Also Like

0 comments: