Fuledi aanika waziwazi matukio mchanganyiko aliyokutana nayo weekend iliyopita........ Soma

Mwalimu: Kama nikikupa simu 1, halafu nikakupa nyingine 1 na nyingine 1 utakuwa na simu ngapi?
Mwanafunzi: Simu 4 sir.
Mwalimu: No. Nisikilize kwa makini. Kama nikikupa simu 1, halafu nikakupa nyingine 1 na nyingine 1 utakuwa na simu ngapi?
Mwanafunzi: Simu 4 sir.
Mwalimu: No! Jamani mitoto ya siku hizi! Ngoja niweke swali kwa mtindo mwingine basi. Kama nikikupa chungwa 1, halafu nikakupa jingine 1 na jingine 1 utakuwa na machungwa mangapi?
Mwanafunzi: Machungwa matatu.
Mwalimu: Vizuri sana. Sasa kama nikikupa simu 1, halafu nikakupa nyingine 1 na nyingine 1 utakuwa na simu ngapi?
Mwanafunzi: Simu 4 sir.
Mwalimu: Hivi we kidudumtu hiyo 4 unaitoa wapi?????!!!
Mwanafunzi: Kwa sababu nyumbani tayari nina simu 1 mwalimu. Ukijumlisha na hizo unazonipa zitakuwa 4 lazima!
Nani kakariri hapo? Mwalimu au mwanafunzi?!
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Siku moja jioni majira ya saa kumi na moja marafiki watatu wakaao nyumba moja waliamua watoke kidogo.
Wakatembea umbali mrefu kwa miguu huku wakifurahi na kubadilishana mawazo kwa furaha na mwishowe kuishia sehemu ambako wakapata chakula cha pamoja na kisha kurudi nyumbani.
Huko nyumbani wakakutana na wanafamilia wengine na kuongea kidogo mpaka muda wa kulala ulipotimia na kisha kwenda kulala.
Usiku ule mdogo wao wa kike ambaye ni mwanafunzi wa chuo fulani akaona ni vyema aandae chai na vitafunwa kwa ajili ya kesho yake.
Akawasha jiko la mkaa na kuweka ndani na kabla ya kufanya chochote usingizi ukamwelemea na kulala.
Kwa kuwa mkaa mbichi hutoa moshi wenye sumu, usiku ule wale vijana ndani ya ile nyumba walikosa hewa na siku ya pili yake baada ya majirani kuona ukimya usio na kawaida wakavunja mlango na kuona wakiwa taabani baada ya kukosa hewa usiku ule na kuwakimbiza hospitali.
Wakiwa njiani wale vijana wakakata roho na mmoja akafanikiwa kufika hospitali na baada ya matibabu ya siku kadhaa akapona na kuwa mzima.
Wakati akitoa ushuhuda jinsi alivyopona pona alisema, "Kabla ya kulala niliomba kwa Mungu kuwa naikabidhi nafsi yangu mikononi mwako, naikiwa nitakufa usiku huu naomba uipokee nafsi yangu"
Akaendelea kusema, "Usiku ule wakati nahisi kukosa pumzi na nguvu ghafla nilimwona mtu nisiyemfahamu wala kumfananisha akinipepea na kuniambia utapona tu mwanangu, Naamini mtu huyo si mwingine bali ni Mungu"
Ndugu zangu, ni wangapi ambao tunalala na kuamka bila kumshukuru Mungu na kuomba ulinzi wake?
Umeshajiuliza ni magapi yanaweza kutokea ukiwa usingizini na ukafa bila kujijua?
Je unaiamini mifumo ya umeme, gesi uitumiayo au hata mafuta ya taa au gari yako yenye mafuta ya hatari kulipuka ndani ya nyumba yako?
Una kila haja ya kumshukuru Mungu wako kila wakati na kuomba ulinzi wake katika maisha yako.
Vijana wale waliagana kuwa tutaonana kesho na mipango mingi mbele yao bila kujua Mungu ndio mwenye funguo za kesho.
---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mzee mmoja aliyechoshwa na kelele za baba mwenye nyumba kwa jinsi alivyokuwa akimdai fedha ya pango aliamua kwenda kijijini kwake huko pwani akapumzike kidogo na kuiacha
familia kwa muda.
Alipofika pale akaamua aende kutembelea shamba lake la minazi la urithi aliloachiwa na marehemu baba yake.
Kufika pale alishangaa kuona kuna dalili za kuvuna nazi nyingi sana, na huku akiendelea kufurahia akaamua akwee mnazi mmoja ili aone ukubwa wa nazi hizo.
Alishangaa kuona jinsi ambavyo nazi zile ni nyingi na kubwa akafurahi sana na kuona kuwa sasa ataweza kupata fedha ya kwenda kulipa pango na hata kununua kiwanja kidogo.
Kwa furaha akiwa pale juu ya ule mnazi mrefu kapiga makofi na kusahau urefu aliopo kutoka ardhinii kisha akaanguka,na mpaka anakufa yule mzee alikuwa hawezi kutembea peke yake na nazi zote zile zilivunwa na kuuzwa ili kupata fedha za kumuuguza.
Funzo
Usiusherehekee ushindi kabla haujawa mikononi mwako
******************************************************************************
Mama mmoja baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda mrefu bila ya kupata mtoto huku akijaribu kila njia bila mafanikio, alingiwa na shetani na kuwa na roho ya ukatili sana.
Mama huyu akaanza kuwachukia watoto na mbaya zaidi akawachukia watoto wa jirani yake ambao walikuwa wakija pale nyumbani wanaingia moja kwa moja sebuleni na kulilia juice au hata kufungua mlango wa friji na hatimaye kuinywa juice kama wangebahatika kuiona.
Wivu wa kutokuwa na mtoto ukazidi kumfanya mama yule awe na roho ya ukatili zaidi ya shetani na kujisemesha kuwa lazima ahakikishe na majirani wanaumia kwa kukosa watoto.
Akachukua sumu na kunyunyuzia kwenye juice na kisha kuiweka kwenye friji na kuingia ndani huku akijifanya kama amelala ili wale watoto wakija kunywa wafe.
Usingizi mzito ukampitia yule mama na akaja kushtushwa na sauti ya mguno ya mtu aliyekuwa akitaabika na maumivu ya tumbo akajua kuwa sasa watoto watakuwa taabani.
Mama akajikaza kutotoka na baada ya muda akatoka nje na kushangaa kuona ni mumewe ambaye alikuwa akitapatapa baada ya kurudi kutoka kazini na kuona atulize kiu yake kwa kunywa juice bila kujua ilikuwa na sumu na kufa hapo hapo.
Funzo
Mungu wetu hujua jinsi ya kututunza sisi pamoja na mitego mibaya na hila mbalimbali tunazowekewa na mwovu shetani na vibaraka wake.
Sala
Nakuombea nawe kila aliyepanga kukufanyia baya kabla ya mwaka huu haujaisha aaibike na apate maumivu mara mbili yake.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mama mmoja alipata bahati ya kuolewa na mme mmoja ambaye alikuwa na utajiri mkubwa sana.
Baba huyu alikuwa anafanya kazi katika taasisi moja ya kifedha katika nchi fulani na mkewe pia alikuwa mhasibu katika benki moja maarufu nchini huko.
Maisha yao yalikuwa gumzo mtaani kwani kila mtoto wao alisoma shule za nje ya nchi hiyo na pia kila waliporudi waliendesha magari tofauti ya kifahari na kutumia fedha kwa anasa.
Kila mwananchi wa mtaa huo alitamani maisha ya familia ile na kila mwisho wa mwaka familia ile ilitumia pesa nyingi kusafiri kwenda kijijini kusalimia wazazi huku kila mtu akiwa na gari lake kuanzia baba mpaka watoto
Mara nyingi yule mama alikuwa na dharau hasa akienda sokoni na buchani, alishangaa kuona mtu akinunua nyama nusu kilo badala ya mguu mzima wa ng'ombe au kisamvu ambacho yeye alidai kuwa ni mboga ya sungura.
Watu wengi walikereka na tabia ile na kumwambia ingawa yeye aliona ni sawa na alichukulia kama ni wivu dhidi ya utajiri wao.
Miaka kadhaa badae kuna wizi wa fedha ulitokea ofisini kwa baba na baba akasimamishwa kazi huku akipewa mshara nusu mpaka pale ushaidi ulipo kamilika na kuonekana kuwa alihusika na kuachishwa kazi bila kupewa haki zake.
Wakiwa sasa wanatafakari nini kinaendelea na wanatumia mshahara wa mke tu aliyebaki kazini na hawataki kuamini kuwa wanatakiwa kupunguza matumizi ya fedha mara mama naye akakumbwa na kashfa ya ubadhilifu wa fedha na kufukuzwa kazi na baadhi ya mali kama nyumba na maduka kutaifishwa na kubaki na nyumba moja waliyoijenga kwa siri maeneo fulani
Maisha yakawa magumu na wakawarudisha watoto kutoka masomoni nje ya nchi na kuwaleta nchini mwao katika shule za kawaida ingawa ilikuwa ngumu kwa watoto kuzoea mazingira haya kwank kwao ilikuwa ni kama kushuka thamani.
Mara wakaanza kusikia mtoto wao wa kike kawa changudoa ili apate fedha za matumizi kwa kuwa hadhi yake ilishuka kwa kukosa fedha kabla ya baba kupata mashtuko uliochangia kupooza mwili baada ya kusikia mtoto wao wa kiume naye kawa shoga ili aweze kupata fedha za matanuzi pia.
Miezi michache baadae baba akafariki na mama mpaka sasa anauza vitenge na nguo za kutembeza mtaani kama mmachinga na mpaka sasa watoto washaharibika.
Ndugu yangu nakusihi kamwe usidharau maisha na watu wakuzungukao kwani huwezi jua Mungu ana mpango gani na maisha yao na yako pia.
Mshukuru Mungu kwa kila baraka uliyonayo na kila mara mheshimu kila mtu na kuheshimu uwezo wake kifedha na hata mawazo kwani sote twamuomba baba mmoja ambaye ni Mungu wa watu wote na hutubariki tofauti kwa nyakati tofauti.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Marafiki wawili waliamua kujiajiri na kuanzisha kampuni ya pamoja ambayo ilijihusisha ya masuala ya uuzaji wa magari.
Walipendana na kuzidi kushikamana mpaka siku moja wakaja kuishuhudia biashara yao ikizidi kuwa kubwa na kuwavutia wateja wengi zaidi.
Walimshukuru Mungu kwa bahati hiyo na kuuzidisha uhusiano wa familia zao na mapenzi baina ya familia hizi mbili yakaongezeka maradufu na kufanya kuwa familia za mfano pale wilayani kwao.
Miaka ikazidi kwenda na mafanikio yakazidi kuwa mikoni mwao nao wakamshukuru Mungu wao kwa bahati hiyo.
Miaka michache baadae mmoja wao hali yake ikaanza kusumbua kutokana na maradhi yasifofahamika na akaugua kwa muda mrefu na wakizunguka sehemu mbalimbali kutafuta tiba bila ya mafanikio yoyote yale.
Mke wa yule mme mgonjwa akawa akimfuata yule rafiki wa mme wake ambaye wanafanya biashara kwa pamoja japo ampe fedha kidogo za kumsaidia kumuuguzia mgonjwa kwani wao akaunti yao ya familia ilikuwa imepukutika kabisa.
Pamoja na kuwa alikuwa akipigwa kalenda na rafiki pamoja na kupewa maneno yasiyo ya busara yaliyomshangaza kuwa ni vipi rafiki kabadilika, mara hii aliumia na kulia baada ya rafiki kumpa SANDA na kusema ikamsaidie kupunguza bajeti wakati wa mazishi ya mme wake maana hataweza kupona kamwe.
Mama aliondoka huku akiwa analia na kuomba kwa Mungu kuwa amponyeshe mme wake na kumfanya awe hai na kushuhudia jinsi rafiki alivyomgeuka mapema.
Wiki moja baadae yuke rafiki aliyetoa sanda alipatwa na ajali mbaya na kuvunjika uti wa mgongo na sasa yeye amekuwa kilema, yaani ni mtu wa kubebwa na haja zote hujisaidia hapo hapo alipo.
Yule rafiki mgonjwa alitoka hospt na sasa ni mzima na anaendelea na kazi kama kawaida.
Funzo
Rafiki kabla hujafa hujaumbika hivyo thamini na kuwajali wale wote wenye matatizo bila kuwakejeli au kuvicheka vilema vyao au hali walizonazo kwani nao hawapendi.
Na daima kumbuka kuwa rafiki wa kweli kwa marafiki zako katika nyakati zote, yaani nyakati za jua na mvua.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
0 comments: