Wivu + Viroba = Vimenifanya niropoke upuuzi wangu wa siri.. sasa nyumbani pamewaka moto
Sikuamini kama Habiba angeweza kunisaliti na kutembea na rafiki yangu wa karibu ambaye ni sawa na kaka yangu.
Kwa hasira nikaamua kwenda kupata viroba vitano vya haraka na kwenda mpaka nyumbani anakoishi kwa sasa, kwani mimi nimeoa na nakaa na familia yangu ila huyu Habiba yeye ni dem ambaye ni bibi mdogo wangu na natembea nae kwa siri.
Tulifahamiana naye mwaka mmoja uliopita nikiwa nasafiri kutoka Bar kwenda Mbeya kumsalimia rafiki yangu Fuledi na tangu hapo huwa ni kama zaidi ya mke wangu mdogo na tumekuwa na ugomvi mara kwa mara hasa akishika mimba anapotaka kuzaa mimi huwa namshauri atoe na yeye hataki.
Kutokana na ugomvi huo akaamua anifanyie kisasi kwa kutembea na Fuledi ili tu anifanye nichukie na ndio maana leo hii kaamua anisaliti mbele ya Fuledi ambaye kaja dar kunisalimia.
Ingawa siwezi kumchukia Fuledi kwani alikuwa hamfahamu ingawa habiba anamfahamu sana kupitia picha zake katika simu yangu na alishawahi kumwona siku nilipokuwa mbeyaingawa ilikuwa kwa mbali ila anamfahamu fika na aliniambia angefanya hivyo mie nikadhani utani.
Niliingia nyumbani mwake nikiwa nimefura kwa hasira nikampa vibao kama saba mfululizo na kumuuliza kwa nini kanisaliti.
Akiwa anajiandaa kujibu nikampa teke liliomfanya aangukie kwenye sakafu akiwa katanguliza kichwa na kisha kushindwa kuinuka.
Bila kumwangalia nikaendelea kumpa mateke mpaka nikachoka kumbe maskini muda huo wote alikuwa anatokwa na damu puani na kushindwa kupumua.
Baada ya kugundua nikataka kukimbia nikaona itakuwa ngumu kwani watu wanajua nipo ndani na walikuwa wakiusikiliza ugomvi ule.
Nikamshika kifuani na kuona hata pumzi ilishamkata nikiwa najaribu kufikiria nini cha kufanya mara mdogo wake wanaeyeishi nae akaingia na kuona dada yake ameanguka pale asakafuni bila hata kuuliza akaanza kupiga kelele akisema nimemuua dada yake.
Watu wakaanza kuja pale na kunishika huku wamepiga simu polisi, wakati huo wote viroba vilikuwa vimenitoka na ninalia kwa sauti ya chini chini. Nikachukuliwa na kuingizwa kwenye gari la polisi nikawa naondoka huku nalia na naunagalia mtaa ule kwa mara ya mwisho kwani niliona hukumu ya kifo ndio inanikaribia.
Nikawakumbuka mke wangu kipenzi na mtoto wangu wa pekee kwa uchungu nikalia kwa sauti kubwa mara hii kabla ya kushtushwa na kibao kutoka kwa mama watoto wangu akisema wewe mbona unalia usiku huu huku unataja jina la Habiba, Habiba ni nani wako huyo?
Mpaka sasa nashindwa kujua kama wife aliridhika na jibu langu kuwa ni ndoto tu au nahitaji kumwomba samahani na kuweka mabo wazi kwani kiukweli habiba ni nyumba ndogo yangu.
Nimechanganyikiwa
0 comments: