Hebu leo tuongelee harakati za hawa jamaa wa mziki wa kizazi kipya (BONGO FLEVA)

10:34:00 Unknown 0 Comments



Kuna jambo la MUHIMU ambalo limezoeleka na wengi na twalifahamu ila hatuliangalii kwa jicho la namna ya kipekee

Hebu leo tuongelee harakati za hawa jamaa wa mziki wa kizazi kipya (BONGO FLEVA)

Nimebahatika kukaa na wanamziki wengi wengi wao nimewashuhudia tangu wanaanza harakati zao mpaka wanakuwa maarufu na wengine wakiibukia na idadi kubwa wakiwa mbioni kuelekea kwenye kutoka.

Kwa mara ya kwanza ukikutana na kijana ambaye ana ndoto za kutoka kimziki na ukakaa nae kwa muda ukiongea nae unaweza kufikiri kachanganyikiwa tena sana.

Nasema kachanganyikiwa kwani kila mara utakuta akiimba na kujisahihisha bila kusahau daftari la kuandikia nyimbo kila wazo jipya litakapomjia na atajinyima kula au kufanya kila mbinu ya kutafuta fedha aende studio.

Kama hatoshi ukimtembelea nyumbani kwake basi muda mwingi yupo na cd za wasanii wa kila aina na ana watu ambao kwake ni ma-role models na atajitahidi kukopi hata falisafa yake na wengi wanakuwa wadadisi sana na ndoto kubwa sasa huwa kwenda studio.

Anavyoongelea kwenda studio kwa unayefahamu utagundua kuwa huko nako sio kazi rahisi kwani anaweza kwenda na kurudishwa au hata kutopata bahati ya kuurekodi mziki wake na wakati mwingine hata kuonana na huyo producer na kama akibahatika kuonana na producer kuna wengine hupewa majibu ya kukatishwa tamaa.

Hawa jamaa pamoja na kukatishwa tamaa huwa na roho ngumu au mioyo isyokatishwa tamaaa kwani ataweza kuzunguka huku na kule akihakikisha anatimiza ndoto hiyo.

Haya sasa kabahatika kautoa wimbo wake na swali ni namna gani wimbo huo utapewa airtime na vituo vya radio na hata kusikilizwa kumbi za starehe?

Hapa kijana atajitahidi kwa namna yoyote afahamiane na dj au mtangazaji kwa namna yoyote hata kutumia marafiki wa jirani na kuhakikisha wimbo unapigwa na hata kama hatopokelewa basi atarudi studio tena na tena na kutumia njia hizo hizo mpaka anakuwa mtu maarufu na kupata show ambazo zinampa kula.

Najua wengi tunafikiri labda mafanikio ni mpaka atakapofika levo ya kitaifa ila mimi naongelea kwa upande wa mafanikio ya kawaida kwa kulingana na uwezo wa kila mtu hata wasanii wakubwa ambao nao wamepitia huku.

Hawa jamaa kiukweli huwa wananifundisha mambo yafuatayo.

1. Kuwa na ndoto pamoja na kuzifanyia kazi usiku na mchana bila kupumzika mpaka zitimie.

2. Kuwa na malengo na msimamo wa kile unachokitaka maishani na kuamini kuwa utafikia ndoto zako tu

3. Kuwa na imani na kile ukifanyacho huku ukijaribu kujipa mifano ya waliofanikiwa na kusoma walifanyaje na kuiga nyendo zifaazo

Unaweza ukajifunza mengi sana kama ukipata nafasi ya kukaaa nao pia

#Inspirational  #Motivation


You Might Also Like

0 comments: