Hivi ni nini kinakufanya utambue kuwa muda wa kuoa umefika??? Msome zuzu huyu

11:38:00 Unknown 0 Comments




Jamaa yetu miezi kadhaa iliyopita kaja kutuambia kuwa anahitaji kufunga ndoa kwani ameonyeshwa na Mungu mke na anahitaji kuanza maisha ya kuwa na familia.



Kila mtu pale kijiwen alifurahia sana wazo la bwana Dan la kuamua kufunga pingu za maisha. Lakini kuna mwenzetu akamuuliza Dan, "Kaka umekuwa na msichana huyo kwa muda gani na je umejipanga vya kutosha?"



Dan alijibu kuwa yeye Mungu kamwonesha huyo dada na wanafahamiana kidogo hivyo watamudu maisha na kuwa wataanza maisha kwenye chumba anachoishi bwana dan.



Duuh, kila mtu pale kjiwezi akaishiwa nguvu kwani hata chumba hicho anachoishi bwana dan ni chumba alichopewa ajihifadhi kwa msaada wa wasamaria wema pale mtaani na kama haitoshi dan hana kipato cha uhakika zaidi ya kufanya kazi za deiwaka.



Ili kumaliza yale mazungumzo tukamwambia basi yeye ajitahidi kwenda kuwashirikisha wanajumuiya ambao tunasasli nao pale mtaani na kwa kuwa alikuwa ni mshiriki mzuri wa masuala ya kidini basi tukaamini watalipokea na kulijadili na sisi tutamchangia.



Basi Dan akaenda kwa wanajumuiya na wote wakakubaliana naye ingawa wengi wakahoji inakuwa vipi kaonyeshwa huyo mwanamke na yeye hajawahi kuwa na mahusiano naye? Ila baada ya kujieleza vya kutosha basi wakakubaliana naye.



Dan hakuwa na ndugu yoyote hapa jijini hivyo jukumu likawa chini ya jumuiya kwani yeye familia yake walikuwa wakiishi msoma na kwa maelezo yake ni kuwa walikuwa hawana uwezo wa kutosha.



Wanajumuiya wakamwita dan na kumuuliza kama alikuwa amejiandaa kiasa gani ili taratubu zianze. Yeye akadai kuwa Mungu kamwonesha huyo binti na lazima afunge harusi.



Mzee mmoja yeye ni fundi kushona akatoa msaada wa kumshonea nguo bure, mama mmoja yeye ni mpambaji akatoa mapambo na viti vyake vitumike siku ya harusi pamoja na vyombo vya kupikia.Na wanajumuiya wengine wakaanza kuchangishana na kufanikiwa kupata fedha kidogo ya kufanya harusi. Ingawa Dan yeye akawa hana hata kidogo.



Kule msoma wakawa ndugu sita wamejiandaa pamoja na mke mtarajiwa kuja jijini kwenye harusi lakini hawna fedha za nauli. Ikabidi mwanajumuiya mmoja ajitolee kuongea na ndugu yake ambaye ni mfanya biashara wa samaki asaidie kuwapa lift kwenye gari lake anapokuja jijini.



Wakafanikiwa wakaja na kufikia katika nyumba ya mama ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya. Shamra shamra zikaendelea lakini kumbuka bwana harusi hakuwa na hela ya shela hivyo ikabidi arudi kwa wanajumuiya kuwa anaomba msaada.



Siku ya harusi wanajumuiya wakatoa magari mpaka kanisani ambako harusi ilifungiwa huko na kufuatiwa na chakula kilicholiwa kwenye viwanja vya kanisa. Ingawa watu waliumia sana kula wali wa maji ( bila pilau) na soda kisha kutawanyika.



Baada ya harusi wale wageni wakawa bado wako kwa yule mama mwenyekiti wa jumuiya na hawaoneshi dalili za kuondoka. ikabidi yule mama amfuate dan na kumuuliza vipi wageni wataondoka lini?



Dan akasema kwa sasa hawana nauli ya kurudi ila Mungu ataonesha njia na wataondoka tu. Yule mama akashikwa na hasira lakini akajikaza na kuamua kukusanya wanajumuiya wenzake ili wajadiliane na wakakusanya nauli na kuwapa warudi kijijini kwao msoma.



Baada ya kuondoka wageni wale dan akamfuata yule mama tena na kumwambia sina chakula pale nyumbani hivyo nitaomba msaada. mama wa watu akawa hana jinsi na kumpa chakula ili jamaa aweze kuanzia maisha na mkewe.



Hali ikawa ngumu na mkewe akaanza kufanya kazi za ndani majumbani kwa watu ili wapate kula ingawaa ikawa ni kwa shida sana. Dan akamua kwenda kwa yule mama na kumwambia amepata kibanda cha biashara na hana uwezo wa kulipia pango na bei yake ni shilingi 300,000.



Mama akaona isiwe taabu akampa fedha na kipindi hicho mkewe ana mimba kubwa na hawezi kufanya lolote zaidi ya kukaa nyumbani. Dan akaenda kulipia pango lile miezi sita.



Lakini kumbe dan hana tena fedha ya mtaji hiyo ikabidi arudi kwa yule mama kuomba msaada ingawa mama alipanic lakini hakuonyesha ikabidi amwambie aje siku ya pili yake. Mama akaondoka mpaka kwa rafiki yake na kuuliza hivi huyu dan ana kichaa au mzima?



Baada ya kushauriana ikabidi wachange ili wampe na kuona nini kitatokea. hatimaye wakamppa dan. Dan akaenda na kuanza biashara yake vizuri na ikawa na matumani.



Sikuchache baadae dan akapata ajali akiwa anatoka kazini kurudi nyumbani na kulazwa kwani alivunjika mguu na mkono na mke sasa hawezi kufanya lolote hivyo ikabidi wanajumuiya ambao sasa walikuwa wakimsaidia yeye na dan waombe yeye arudi msoma na wao wamsaidie dan ambaye mpaka sasa yupo hospital.



Tuombe dan apone ili tuendelea kupata series za maisha yake...... maana bado mimi simwelewi kabisa.






You Might Also Like

0 comments: