Kisa cha kijana aliyehitimu masomo ya utalii na kukosa kazi hapa TZ

11:29:00 Unknown 0 Comments


Miaka 10 iliyopita Dan alihitimu shahada yake ya utalii na kuhangaika kwa zaidi ya miaka miwili bila kupata kazi ya aina yoyote ile hapa nchini.

Siku moja akiwa kakaa nje ya hotel moja kachoka na kuichiwa nguvu baada ya kumaliza usaili ambao pia hakubahatika kupata ajria mzee mmoja alimwomba masaidie kupakia mizigo kwenye gari lake.

Baada ya kupakia mabox yale mzee akamshukuru na kumwambia Dan kuwa sina fedha ya kukulipa ila nakupa box hili moja dogo nenda nyumbani na utakachokiona kipokee hata kama ni kidogo na mzee akaondoka.

Dan akalichukua lile box na alipofika nyumbani alilifungua na kushuhudia kuna mbegu za mboga za majani aina ya figiri na mchicha. Hakutaka kuendelea zaidi kwa hasira akatupa lile box na kulia akiona kama ilikuwa ni dharau.

Aliendelea kutafuta kazi bila mategemeo na siku moja akiwa nyumbani anafanya usafi katika bustani yao ya nyumbani wazo likamjia kuwa naweza kutengeneza bustani na kuzipanda zile mbegu na kuachana nazo.

Mboga zile zilistawi sana kwa kuwa shamba lile liliachwa kwa muda mrefu na hakuweka aina yoyote ya dawa au mbolea na kumvutia jirani yake aitwaye Salome ambaye alikuwa ni meneja wa hoteli moja ya kitalii pale mjini.

Salome alipoambia mboga zile hazina madawa ya aina yoyote alimpa tenda Dan ya kuzipeleka mboga zile kila siku asubuhi katika hoteli yao na dan alifanya kwa muda na kuona kuna uhitaji wa kuongeza ukubwa wa eneo.

Mwaka mmoja baadae dan akawa amepata eneo kubwa kaajiri vijana wengi na amefanikiwa kupata tenda za kupeleka mboga katika hoteli nyingi za kitalii na kila siku akaifurahia ajira yake na kumkumbuka yule mzee ambaye kamwe hakufanikiwa kuonana nae.

Rafiki, haijalishi ni kwa namna gani umehangaika katika maisha yako ukitafuta kufanikiwa au kufikia malengo yako amini kuna mafanikio mbele yako.

Kuna mafanikio mbele yako kama utaacha kudharau ideas ndogo na kuzifikiria kubwa huku ukiwa huna uwezo wa kufikia hayo mawazo makubwa kwa wakati huo.

Kufanikiwa huja pale mtu unapoweza kufahamu fursa zilizopo mbele yako na kuzifanyia kazi kwa wakati na umakini huku ukimshirikisha Mungu.

Wengi tunatamani kuajiriwa na kulipwa fedha nyingi na marupurupu kibao wakati hatuna uzoefu wa mambo madogo ambayo yangetupa uzoefu mkubwa wa kufikia ndoto hizo.

Waweza share kama tupo wote

Tangaza na blog hii wasiliana na whatsapp 0713317171

 





 

You Might Also Like

0 comments: