Soma kisa cha punda wa ajabu aishie mbeya

11:06:00 Unknown 0 Comments




Mkulima mmoja ambaye yeye alikuwa anafanya biashara ya kuzalisha chumvi na kuwauzia wanakijiji wake, alipata bahati ya  kummiliki punda mwenye nguvu sana.

Pamoja na punda huyu kuwa na nguvu na kumsaidia kuivusha chumvi ikiwa katika mifuko kwenda vijiji jirani kwa kuvuka mto, lakini pia punda huyu alijaliwa akili na ujanja sana.

Siku moja yule mkulima akawa anavusha mifuko ya chumvi huku kaiweka mgongoni mwa yule punda.

Lakini siku hiyo yule punda akawa kila wakifika pale mtoni anauzamisha mgongo na chumvi kuanza kuyeyuka. Na kila mzee alivyojitahidi kubadili mifuko na kuzianika zile chumvi lakini bado punda alizama kila alipowekewa mfuko mpya wa chumvi ili wavuke pale.

Mkulima akatafakari kwa muda akaona kwa nini punda anizidi akili?

kisha akamrudisha punda nyumbani na kumbebesha magodoro makubwa mawili, lakini ikaonyesha kuwa yule punda hakutaka kabisa kubeba vitu siku hiyo na hivyo alipofika mtoni yule punda akajizamisha tena makusudi.

Lakini safari hii yule punda alipozama magodoro yakabeba maji na aliposimama mzigo ukawa mkubwa na kumlemea yule punda na kuanza kupiga kelele za maumivu.

Yule mkuliwa akakaa pembeni na kucheka sana kwa akili aliyoitumia

Somo:

Ukifikiri wewe ni mjanja zaidi jua kuna wajanja zaidi yako na daima usizidharau nguvu au plani za mpinzani wako katika kila jambo ufanyalo.

Lakini pia wajanja wengi hunasa kwenye tundu bovu

You Might Also Like

0 comments: