Usiusherehekee ushindi kabla haujawa mikononi mwako
Mzee mmoja aliyechoshwa na kelele za baba mwenye nyumba kwa jinsi alivyokuwa akimdai fedha ya pango aliamua kwenda kijijini kwake huko pwani akapumzike kidogo na kuiacha
familia kwa muda.
familia kwa muda.
Alipofika pale akaamua aende kutembelea shamba lake la minazi la urithi aliloachiwa na marehemu baba yake.
Kufika pale alishangaa kuona kuna dalili za kuvuna nazi nyingi sana, na huku akiendelea kufurahia akaamua akwee mnazi mmoja ili aone ukubwa wa nazi hizo.
Alishangaa kuona jinsi ambavyo nazi zile ni nyingi na kubwa akafurahi sana na kuona kuwa sasa ataweza kupata fedha ya kwenda kulipa pango na hata kununua kiwanja kidogo.
Kwa furaha akiwa pale juu ya ule mnazi mrefu kapiga makofi na kusahau urefu aliopo kutoka ardhinii kisha akaanguka,na mpaka anakufa yule mzee alikuwa hawezi kutembea peke yake na nazi zote zile zilivunwa na kuuzwa ili kupata fedha za kumuuguza.
Funzo
Usiusherehekee ushindi kabla haujawa mikononi mwako

0 comments: