Duuuh siamini toto la ukweli hapa facebook
Wiki nne hivi zimepita tangu nifahamiane na binti mmoja hapa facebook na kuanza kuchati nae.Mwanzoni nilianza kuchati nae zile chati za kilokole mambo dada, umependeza dada, habari za familia, Mungu aibariki siku yako, umeshindaje dada na maneno kama hayo.
Baadae zikaanza zile chati za duh leo mpendwa nimeona umetokelezea sana, mara yeye anajifanya thanks darling na kujifanya sorry kaka huwa najisahau nisamehe kutamka darl.
Mmmh suala la darl nikaona linanoga na mimi n ikawa najifanya wife wa mie niambie na kisha najifanya kupotezea kumbe kimoyomoyo naona hili deal na na kujisemesha endelea tu mama.
Basi bwana chati zimeeenda weee zimeeenda weee mpaka sasa ikawa waziwazi kuwa mimi ni hubby wake bwana.
Mtoto anajua kuchati kumbe ule ulokole wake ulikwa fake bwana, nami sasa nikaona isiwe taabu nikazidisha mapenzi mtandao
Basi juzi kanicheki kwa inbox na kuniambia kama vipi siku ya jana tuonane mida kama ya saa tisa maana atakuwa akatoka ofisini kwake.
Ebwana yule binti akakushuka kwenye gari alilokuwa akiliendesha mwenyewe wakati huo mimi ninamzoom tu.
Basi bwana akaja mpaka pale na tukaagiza chakula akala baada ya hapo akasema twende lodge tukaenda akachukua chumba kwa ajili ya wageni wake waliokuwa njiani wakija mbeya na kisha tukaachana na mimi nikarudi nyumbani
Kudadadeki cheki ulivyotoa mimacho ukiwaza maujinga yako na utajifanya kutokomenti kwa aibu.........
0 comments: