HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 24

14:03:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 24

ILIPOISHIA JANA

Mama pachu aliendesha gari huku  akionesha kuwa na mawazo na kuchanganyikiwa zaidi juu ya ni nani aliyetoa siri hiyo na kumpa mpigaji na kama haitoshi akaanza kuhoji kuwa nini itakuwa hatma ya yeye na ndoa yake hasa akikumbuka jinsi baba pachu alivyo mtu wa hasira na maamuzi ya ghafla.

Akiwa katikati ya dimbwi la mawazo hayo mama pachu alipigiwa simu na baada ya kuipokea msemaji alimchanganya zaidi kwani alisema................................

ENDELEA

Akiwa katikakati ya dimbwi la mawazo mama pachu alipigiwa simu na baada ya kuipokea msemaji alimchanganya zaidi kwani alisema, " Unaelekea wapi sasa huko?".

Mama pachu alisimama haraka na kugundua kuwa alikuwa ameshaanza kuachana na mji wa  uyole akiwa njiani kuelekea nje ya jiji la mbeya. Akasimama na kugeuza gari kisha akarudi mpaka uyole stand ambako alinunua baadhi ya mahitaji na kuanza kurudi kuelekea nyumbani.

Nyumbani aliwakuta baba pachu na mwakibubu wakiwa katika maongezi yao na moja kwa moja alipitiliza mpaka chumbani ambako alikaa kwa dakika nyingi kidogo na kisha akarejea jikoni tofauti na kawaida yake.

" Mama pachu vipi mbona umeingia ukiwa na mawazo tofauti na kawaida?" alihoji baba pachu baada ya kugundua kuwa mkewe hakuwa katika hali  ya kawaida.

"siwajua tena mme wangu masuala ya sokoni na ukizingatia vumbu la mbeya niliamua nipitize kujiweka safi kidogo kabla ya kuja kukusalimia mme wangu, vipi mmeshindaje wagonjwa wangu?" aliongea mama pachu huku akijifanya kutabasamu na kisha kuelekea jikoni kujibiwa na mazungumzo kidogo.

Chakula kilikuwa tayari baada ya muda mfupi wakala na kumsindikiza mwakibubu nyumbani kwake na baada ya hapo wao walirejea nyumbani. Baba pachu alibaki sebuleni na mama pachu akawa chumbani akiwaandalia watoto sehemu ya kulala.

Ghafla simu ikaita na mama pachu alikurupuka na kwenda kuichukua kisha akajifanya kama anaipokea huku akiitoa sauti na kujiongelesha kuwa mpigaji kakata na baada ya hapo akatoka nje na kwenda kuipokea.

" Umejisikiaje nilipokukutanisha na huyo shukurubu wako?" Alihoji mpigaji

"Jamani kwani nimekukosea nini? Naomba tafadhali mme wangu asigundue nitaachika mimi nisamehe niambie wataka nini yaishe?" yalikuwa ni maneno ya mama pachu ambaye kamwe usingedhani angeweza kuwa mdogo kiasi hiki kwa jinsi ambavyo alifahamika kwa ujasiri.

" Wewe si ulikuwa unapenda kufuatilia mambo ya watu na muda mwingi simu ya mmeo ulikaa nayo hata kama mlijiwekea mikakati ya kuaminiana? Kwanini sasa ulimsaliti mwenzio?" hata kabla mama pachu hajajitetea simu ile ilikatika na haikupatikana tena.

Mama pachu alingia ndani na kwenda kwenye kabati lake nguo na kuchukua pajama yake kisha akalala bila hata ya kuongea na baba pachu na simu akaizima.

Asubuhi yake mama pachu aliamka akiwa na mawazo mengi na baada ya kuandaa chai alimwaga mmewe na kuondoka. Aliendesha gari mpaka nje ya kanisa liitwalo AFRICAN PEOPLE MIRACLE MINISTRY na kukutana na mchungaji kiongozi ambaye alimchukua mama pachu mpaka ofisini kwake.

Mama pachu akaanza kueleza kilichompeleka pale na kusimulia juu ya simu na  jinsi hiyo simu inavyomsumbua na kufichua baadhi ya siri zake ambazo zaweza mkuhatarishia ndoa yake na kuwa sasa alitaka masada zaidi.

Mchungaji Zuba ambaye yeye hujiita BABA JUSI na mtabiri mwenye kuokoa nafsi zilizopotea alianza kwa kumsimulia mama pachu juu ya ulimwengu wa giza.

"Karibu sana mpendwa na umekuja sehemu sahihi kabisa, na ni vyema utambue kuwa hiyo ni ya nguvu za giza ambazo humwingia mtu na kukaa sehemu mbalimbali za mwili, na pia kumbuka bila kuwa na maombi maalumu pepo huyu ni mbaya sana kwani husababisha mengi " Aliongea mchungaji huyo huku akinyanyuka kutoka katika kiti chake na kumsogelea mama pachu.

Pamoja na kuonekana kuwa umri umesoga lakini mama pachu alijaliwa kuwa na umbo zuri ambalo kila binti wa sasa angelilia. Mama pachu sio mnene sana au mwembamba sana lakini kutokana na kufuatilia mazoezi pamoja na ulaji wenye kufuata vigezo vya afya mama pachu hakuwa na tumbo kubwa na kulifanya lile umbo lake namba nane kuchoreka vyema. Uso wake ulionesha kuwa ni bado angali binti na mbaya zaidi ni mpangilio wa mavazi pamoja na ubunifu wa vywele zake vitu vilivyomfanya aendelee kukodolewaa macho hata kama pete ya ndoa ining'aa kidoleni.

" Sasa basi unatakiwa kuelewa kuwa pepo huyu hukaa sana maeneo ya kiunoni na ni lazima kuwa hivi karibuni utakuwa umepatwa sana na maumivu ya kiuno, sasa tutaanza maombi na muda huu na wakati mimi nafanya maombi ya kuvuja vunja hizo nguvu za giza basi nitakuomba wewe uwe unacheza kwa kukatika huku ukiimba pambio" aliongeza neno hilo mchungaji huku akianza kuomba

Mama pachu alianza kufanya kama alivyoagizwa huku akiwa kafumba macho na maombi yakiwa yanaendelea, lakini ghafla alishtushwa kuhisi  mikono ikiwa imezunguka kiunoni mwake huku mchungaji huyo akiwa ana hema juu juu kama vile alitaka kumnong'oneza kitu kwa nyuma.

"Mchungaji gani huna haya wewe? unataka kufanya nini?" mama pachu liongea kwa jazba huku akimlamba vibao viliwi mchungaji huyo ambaye wakati huo eneo lake la mbele ya suruali lilionekana kuwa limemtuna kama vile alikuwa kaficha tango.

Mama pachu aliufungua mlango na kuondoka huku akiwa sasa hajielwi ni nini afanye au aende kwa nani aombe msaada.Wakati huo sauti ya mchungaji ilisikika kwa mbali ikiita rudi wewe!! rudi wewe!!! pepo mbaya kakukumba njoo ufanyiwe maombi.

Hakika sasa huu ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwa mama pachu hivyo ikambidi atafute sehemu na kumpumzika huku akitafakari nini kiendelee. Akiwa pale alishangaa kaletewa kinywaji na kuambiwa na mhudumu kuwa kinywaji hicho tayari kimeshalipiwa.

Mama pachu alishangaa na alipohoji ni nani kamlipia yule mwanamke alionesha kwa kidole maeneo ya kaunta na kumwona bibi Gusa Unate akiwa na chupa kubwa ya wine, kavaa miwani ya jua, cheni matata shingoni  huku kimwoneshea alama ya dole gumba mama pachu.

Wakati huu Mama pachu hakutabasamu zaidi ya kuishiwa nguvu na kutikisha kichwa kama ishara ya kumshukuru kwa ofa hiyo. Na kabla hajamalizia gari la polisi liliingia maeneo hayo na polisi wawili walionekana wakija eneo hilo na wakaelekea jikoni na kuagiza chakula.

Hamadi ile mama pachu anageuka meza ya bibi ilikuwa tupu na alipouliza kwa mhudumu bibi yuko wapi, mhudumu alijibu, " Aisee yule bibi katimka hapa kwa mbio za ajabu na sijui wapi kaelekea"

Wakati  akiendelea kusikuliza maneno ya mhudumu mama pachu alipokea simu na simu hii ilikuwa ni kutoka kwa baba pachu akimuuliza yuko wapi kwani kuna mgeni kaja nyumbani akimsubiri.

Alinyanyuka na kuondoka kuelekea nyumbani ambako alikutana na mama toinyo na wakati huu mama toinyo alikuwa akimtaka mama pachu amtunzie siri yake ili ndoa yake isiingie kasoro.

" Shoga yangu mimi mwenyewe nina matatizo yangu tena makubwa wewe nenda tu ila kama ukiweza jisalimishe mwenyewe kwa shemeji maana hii dunia sitaki kukutisha ila wewe tambua dunia hii ni ndogo sana" Aliongea mama pachu huku akifuta macho yake

Mama toinyo aliondoka eneo lile akiwa na mshangao mkubwa kuwa kuna nini kinaendelea  ingawa alipiga moyo konde kuwa kamwe hatatubu maana ingemshushia heshima yake pale mtaani na kutengwa na kazi za kanisa.

Saa nane na dakika 50 mwakibubu alingia nyumbani kwa baba pachu na kumkuta mama pachu akiwa kakaa pale pale alikokuwa amekaa na mama toinyo na kaionesha hali ya kuwa katika msongo mzito wa mawazo. Bwana mwakibubu akauliza, " Shemjei mama pachu!! Mbona kama jana na leo nakuona hauko katika hali yako na kama haitoshi muda sio mrefu nimeliona gari lako likitoka  kwa yule mchungaji zuba?" Aliongea mwakibubu

" Shemeji yangu yaani majanga yanayowakuta wewe na baba pachu naona yananizidi uwezo, maana mara leo mlewe sana, kesho mpate ajali, mara kazini hampo tena na sasa hivi hameleweki eleweki yaani suala hili nitanipa wakati mgumu sana hivyo nilienda kwa yule mchungaji ili awaombee" aliongea mama pachu kwa ujasiri mkubwa

" Shemeji usiwe na shaka sisi tupo safi na hivi tukipona tu vizuri tunaanzisha kampuni yetu hivyo tutakuwa na wakati mkubwa wa kujiimarisha na kuyasahau haya kwani ni stress za kazi tu......" hata kabla mwakibubu ahajamaliza kuongea simu yake iliita.

Mama pachu aliposikia sauti ya simu alishtuka na kuanza kwenda nje kabla ya.........................................................

Je nini kitamtokea mama pachu ?

Usikose kisa hiki jumatatu  jioni

MUHIMU

Kwa msomaji wa simu ya ajabu aiishie Mbeya kesho tutakuwa na cake nyingine party pale hoteli ya penge kuanzia saa saba mchana mpaka saa mbili kamili za usiku kwa kiingilio cha shilingi 5000 tu.

Karibu ushiriki nasi katika burudani hii ukiwaona live kina mwakibubu, baba pachu, mama pachu, mama amigo, bibi gusa unate na marafiki wengine wengi amabao ni wasomaji wa hadithi hii.

Pia kama una birthday yako kutakuwa na zawadi nyingi za kushtukiza.

Wasiliana nasi kwa namba 0713317171 whatsapp au piga namba 0654690368 ili kupata tiketi yako mapema kwani nafasi ni kwa watu 30 tu

Karibuni like Simu ya Ajabu

You Might Also Like

0 comments: