HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 23

12:41:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "


Season 23



ILIPOISHIA JANA

Mama pachu huku akianza kuwa na hofu akarudi chumbani na kuifuta ile simu iliyopigwa na kisha akalala. 

Asubuhi mama pachu aliamka kwa kuchelewa na kumkuta baba pachu akiwa kakaa sebuleni akisubiri kwenda hospitali. Basi mama pachu akachukua simu yake na kuona kuna missed calls 8 na meseji 3 moja kati ya meseji hizo zilimfanya mama pachu akimbie haraka na kwenda nje.

Meseji hiyo iliandikwa.........................................................................

ENDELEA


Meseji hiyo iliandikwa, " Wewe endelea na kazi zako ila saa tisa kamili leo uwe umejiandaa nitakupigia simu na kukupa maelekezo ya nini cha kufanya" Mama pachu kwa hofu iliyoambatana na masawali mengi juu ya ujumbe huo ikamtanda na kumfanya aanze kuipigia ile namba ili apate undani wake.
Alijaribu kuipigia lakini namba ile ikaonesha kuwa haipo na kama haitoshi akaanza kuikumbuka kuwa ni namba ileni  ile iliyompigia jana yake usiku. Alisimama kwa hofu pale chini alipokuwa amekaa na kunaza kutembea mwendo wa taratibu akiwa hajui anataka kutoka nje au kurudi ndani mpaka aliposhtushwa na sauti.
"Mama pachu vipi mbona unachelewa muda na wa kwenda hospitali umefika?" aliongea baba pachu huku akijivuta kwa kuchechemea kuelekea nje. Basi mama pachu akaingia ndani na kujiandaa haraka kisha akauchukua mkoba wake na kulitoa gari lake na kuanza kuondoka kuelekea hospitali.
Wailifika hospitali na kumkuta mwakibubu akiwa tayari kashahudumiwa  na kwa haraka mwakibubu akamvuta baba pachu pembeni na kumpa hadithi ya jana yake jinsi alivyomkaribisha mjini bibi gusa unate na wote wakaishia kucheka na baba pachu baada ya kuhudumiwa wakaanza safari ya kurudi nyumbani.
Walirudi nyumbani na wakati huo na mama pachu akawaandalia chakula huku akili yake ikiwa haiko sawa akiwaza juu ya ile meseji na kuwa kwanini awe amejiandaa kwani kuna nini kitatokea?
Baada ya chakula baba pachu na mwakibubu wakawa wako busy wakiangalia marudio ya mechi ya mpira wa miguu na wakati huo muda ulikuwa ni saa nane na madakika.
Mama pachu akiwa nje huku akiwa kuna kitu anakifanya na tayari alishajiandaa akapokea simu kutoka kwenye ile namba ngeni ikimtaka aende Tandika Tulale Guest House na akifika pale aulizie chumba namba 802. 
Simu hii ilimfanya mama pachu achanganyikiwe zaidi na kutafuta njia ya kwenda huko kwani aliambiwa asipofanya hivyo kuna jambo kubwa baya lingeweza kumtokea. 
Basi mama pachu akaingia ndani na kumbusu shavuni baba pachu huku akiomba ruhusa ya kwenda sokoni kununua ndizi na nyama ya utumbo chakula ambacho baba bachu alikuwa akikipenda sana.
" Hakika ni kwa kitu hiki tuu huwa sijutii kukuita kipenzi cha moyo wangu asante sana mama pachu mke wangu wewe nenda mimi nipo na mwakibubu hapa tunadiscuss mawili matatu" aliongea baba pachu na hata kabla ya mama pachu ahajaanza kuondoka mwakibubu naye alidakia
" Aisee mnanifanya nimkumbuke mama amigo maana hataki kabisa kurudi mpaka amalize kazi zake za shamba yaani mna mapenzi moto sana nimewaonea wivu" alimaliza bwana mwakibubu huku akionesha dalili za wivu na kushushia na glass ya juisi iliyokuwa mezani.
Saa tisa na dakika kumi mama pachu aliwasili pale hotelini na kupelekwa mpaka chumba namba 802 na kukigonga. Mlango ulipofunguliwa mama pachu aliishiwa nguvu na kulazimika kuingia haraka chumbani na kuufunga mlango"
" Shukurubu!!!!!!!!!! Shukurubu!!!!!!!!!!  unajua mimi ni mke wa mtu na yote yaliyotokea kipindi kile nilikuambia ilkuwa ni kutokana na pombe tu sasa kwanini unanze kumwaambia huyu binti anipigie nije hujui unaweza kuhatarisha ndoa yangu? Unajua baba pachu yupo? na je umerudi lini Mbeya???????" Aliongea mama pachu kwa  jazba na mshangao wenye kukata tamaa.
Wakati huo shukurubu naye alikuwa akishangaa iweje mama pachu aje pale wakati yeye alikuwa na ahadi na mke wa mzee mmoja mfanya biashara mashuhuri sana hapa mjini na muda wowote ule angeweza kuingia. 
" Kwanza imekuaje na nani aliyekupigia?" alihoji shukurubu

Mama pachu akaingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa simu kisha akajaribu kuitafuta ile namba na kumwonesha shukurubu ambaye alionesha kutokuifahamu kisha shkurubu akamwambia mama pachu kwa kufoka.
"siifahamu hii namba na tafhadali naomba uondoke  haraka nitakutafuta utaniharibia biashara yangu hapa" Aliongea shukurubu huku akimfungulia mlango mama pachu ili aondoke.
Shukurubu ni kijana wa mjini ambaye baada ya kuhitimu mafunzo yake ya elimu ya juu akisomea uandishi wa habari na kujikuta akiwa katika wakati mgumu wa kijipatia ajira ya kueleweka akaanza mikakati ya kutembea na wake za watu ili waweze kumhudumia mjini.
Siku moja miezi michache iliyopita wakati baba pachu akiwa iwindi kikazi mama pachu aliamua atoke kwenda kupata kinywaji sehemu na ndipo alipokutana na kijana Shukurubu ambaye alikaribishwa kinywaji na kutokana na ujanja wake wa maneno alifanikiwa kufanya tukio moja la siri na mama pachu baada ya pombe kuwazidia.
Tangu siku hiyo mama pachu akawa akijitahid kumkwepa kijana huyo mpaka kudiriki kutumia fedha nyingi ili amwamishe mkoa ambapo kwa sasa alijua kuwa bwana shukurubu yuko jijini dar akiendesha biashara ya duka la nguo kutoka katika mtaji aliopewa na mama pachu kwa makubaliano ya yeye kutorudi wala kuifumbua siri bila kujua kijana shukurubu hakwenda popote zaidi ya kupotelea mwanjelwa akiendelea na jitihada zake za kwanasa wake za watu
Mama pachu wakati anatoka pale kwenye guest akiwa kwenye korido alisikia kelele ikimwita "mjukuu!! mjukuu!!! mjukuu!! vipi? kumbe na nyinyi mnalala hapa hapa au hii ni guest yenu yaani sikujua nimelala kwenye nyumba ya mjukuu wangu? haa wapumbavu sana hawa watoto hawajui kuwa hii ni nyumba ya mjukuu wangu ? ngoja niende nikachukue hela yangu ".aliongea bibi gusa unate ambaye alilala jana yake hapo
Wakati bibi akiwa anelekea mapokezi mama pachu alimwahi na kwenda kumshika mkono na hata kabla ya kuongea neno mama pachu alishtuka baada ya kuona jirani yake aitwaye mama toinyo akiingia chumba namba 802.
Hakika mama pachu alishtuka kwani yule mama alikuwa ni mama aliyeokoka  na  pia alikuwa ni mama aliyesifika kwa jinsi alivyoweza kupangilia maneno wakati yake wakati sala au mahubiri kanisani na pia alikuwa mshauri mkuu wa masula ya ndoa na maisha pale mtaani.
Mama toinyo aliingia mle chumbani kwa aibu baada ya mamcho yake kugongana na mama pachu na mama pachu hakuongea neno zaidi ya kufungua mkoba wake na kutoa kiasi cha shilingi elfu ishirini na kumpa bibi huku akimwambia uchunguzi wangu umekamilika unamwona huyo mama anyeingia hapo ndani bibi??
Bibi akajibu "ndio"
"Basi mama huyo amekuwa akitembea na  mtoto wa dada yangu ambaye nasikia yuko chumba hicho namba 802, hivyo sasa niache naenda kuchukua polisi nakuja sasa hivi wewe kaa kimya na tumia hiyo hela kupata bia wakati mimi naenda polisi" kisha mama pachu akaondoka kwa haraka
Bibi gusa unate aliposikia neno polisi na kukumbuka ile adhabu ya kudeki bwalo na utapeli alioufanya jana yake akaona kuwa polisi wangeweza kuondoka na yeye pia hivyo akaondoka haraka na kwenda kuitafuta guest nyingine ili alale kabla ya kujiandaa kurudi aneo lake la kazi.
Mama pachu aliendesha gari huku  akionesha kuwa na mawazo na kuchanganyikiwa zaidi juu ya ni nani aliyetoa siri hiyo na kumpa mpigaji na kama haitoshi akaanza kuhoji kuwa nini itakuwa hatma ya yeye na ndoa yake hasa akikumbuka jinsi baba pachu alivyo mtu wa hasira na maamuzi ya ghafla.
Akiwa katikati ya dimbwi la mawazo hayo mama pachu alipigiwa simu na baada ya kuipokea msemaji alimchanganya zaidi kwani alisema................................

Je mama pachu aliambiwa nini?

Usikose kisa hiki kesho  jioni

MUHIMU

Kwa msomaji wa simu ya ajabu aiishie Mbeya jumamosi hii tutakuwa na cake nyingine kama hii pale hoteli ya penge kuanzia saa saba mchana mpaka saa mbili kamili za usiku kwa kiingilio cha shilingi 5000 tu.

Karibu ushiriki nasi katika burudani hii ukiwaona live kina mwakibubu, baba pachu, mama pachu, mama amigo, bibi gusa unate na marafiki wengine wengi amabao ni wasomaji wa hadithi hii.

Pia kama una birthday yako kutakuwa na zawadi nyingi za kushtukiza.

Wasiliana nasi kwa namba 0713317171 whatsapp au piga namba 0654690368 ili kupata tiketi yako mapema kwani nafasi ni kwa watu 30 tu

Karibuni like Simu ya Ajabu

You Might Also Like

0 comments: