HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 21

15:33:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 21

ILIPOISHIA JANA
Bibi alionesha hali ya kuzidi kuchanganykiwa na kusema, "Mwanangu usicheke mbele ya kifo, mimi nipo mashakani hapa na siwaachi kwani huyu mtu anaonekana ananifahamu na ana roho mbaya sana, hebu fikiri kila nyendo zangu anazijua... hebu kwanza nishikie hii simu yangu. 
Wakati akaiwa anaunyoosha mkono ili kumpa simu bwana mwakibubu ghafla simu ilianza kuita  ...........................

ENDELEA
Wakati akaiwa anaunyoosha mkono ili kumpa simu bwana mwakibubu ghafla simu ilianza kuita na kwa mshtuko baada ya bwana mwakibubu kuiona namba na kugundua ni ya chamdoli ila jina lake limeseviwa MTEJA MPYA.

Mwakibubu alifoka kwa mshangao mkubwa, " Chukua simu yako wewe si umesave ni mteja wako mpya haya hebu ongea sasa na mteja wako" .

Bibi kuona ni namba ya chamdoli alinyakuwa na kumpa nesi pale na kumwambia tafadhali mwambie nimelazwa huyu mpigaji. Nesi aliipokea huku akicheka na kumbwambia yule mpigaji hayo maneno na mpigaji akamwambia kuwa amwambie bibi aache ujinga kwani simu ile ina mhusu yeye.

Wakati nesi anageukwa wodi zima lilikuwa limetawaliwa na vicheko huku mwakibubu akiwa hana hata hamu ya kuangalia yanayoendelea maana alijifunika gubigubi.
"jamani huyu bibi yuko wapi?" Aliuliza nesi

"haha ha a ha ha ha nimemwona alikuwa anaelekea chooni" aliongoea mgonjwa mmoja aliyekuwa kazidiwa na kicheko.

Mama pachu alilirudi akiwa na daktari na baada ya kuwacheki waliruhusiwa waondoke na kuambiwa warudi siku ya pili kuangaliwa hali zao kwani hawakuumia sana zaidi ya mshtuko.
Wakati huo bibi alirudi na kumganda mwakibubu kuwa ni lazima waondoke wote kwani hawezi kurudi nyumbani kwake na mwakibubu ndio kamsababishia yote haya hata kabla ya mwakibubu kuongea bibi akaanza kujisahau na kujinadi tena, " Mjukuu mimi nimetibu vijana wengi sana ila wewe ndio umenikomesha"

" Hivi wewe umejisahau ee? Sasa huyu jini kwangua vocha anakufuataje tena usiniudhi hebu malizana  na mteja wako" alisema mwakibubu

Bibi kwa kwakukurupuka alijibu, " wewe mjukuu hebu elewa huyu sio mteja ni kwangua vocha na hapa anataka roho ya mtu"  Bwana mwakibubu akauliza je wewe umeyajuaje haya bibi hebu acha sanaa zako.

Wakati majadiliano yanaendelea mama pachu alikuwa kakaa kimya akiangalia jinsi mwakibubu na yule bibi walivyokuwa wakihojiana. Mama pachu akamvuta baba pachu pembeni wakati huo wakiwa nje na kumuuliza" baba pachu huyu bibi mbona simwelewi elewi?"

Baba pachu akamjibu kuwa, "Yule ni rafiki wa bibi yake mwakibubu na wanakaa kijiji kimoja sasa kamnunulia simu na anashindwa kuitumia hapo anabishana mhudumu wa mtandano wa simu na habari aliyokuja kumletea ni ya tahadhari kwani  alitumiwa video whatsapp ya kichekesho kinachotahadharisha matumizi ya simu ukiwa unaendesha gari"

Mama pachu alicheka sana lakini ni kama hakuridhishwa na majibu aliyopewa na mme wake. Basi wakarudi na wakaagana na  kuachana na mwakibubu akiwa na yule bibi. Lakini uso wa mwakibubu ulionesha kuwa hali haiko sawa na alitamani baba pachu asiondoke ila ikabidi ajikaze kiume.

Walipoondoka baba pachu na mama pachu bwana mwakibubu yeye akamwabia bibi kuwa ni vyema wapitie sehemu ila wakale. Basi wakajivuta mpaka kituoni na kuchukua bajaji mpaka Hodari Hotel na kuagiza chakula.

Wakati wakisubiri chakula mwakibubu akawa anakunywa juice yake ya embe huku bibi akiwa anakunywa kinywaji kikali ambacho alikunywa huku akidai kinampunguzia machungu na haamini kama amekutana na mwakibubu na mwakibubu kakubali kwenda kukaa naye kwake.

Siku ya leo bibi alionesha kumsifu sana bwana mwakibubu hasa baada ya kumwambia wewe kula kadri ya uwezo wako na kunywa uwezavyo mimi nipo kwa ajili yako bibi si wajua mimi ndio mjukuu pekee?

Basi kwa bibi ilikuwa ni kama faraja kwani alikunywa na kujiliwaza na mziki huku kila dakika akiita mtu wa jikoni akiulizia kama kuku wake wa kuokwa  yuko tayari.

Wakati anaulizia pale mezani alikuwa ameagiza yule mnyama mwenye pua jembe na ndizi nne na kila alipokula ndizi alijifanya kuongea kama bibi aliyekuja mjini kutoka tukuyu... " 

Mjukuu yaani hifi fyote fyangu?""" Mwakibubu alimjibu "kula  tu bibi" ama kweli bibi 
aliifurahia sana hii kauli na kuiona ile siku ilikuwa nzuri kwani alishanza kusahau tafrani yake na kumwambia tena " Baba mwaka huu naomba niumalizie tu kwako"

Wakati huo mwakibubu alikuwa akiinywa juice yake taratibu huku akiichezea simu yake na kisha akanyanyuka na kulekea eneo la jikoni ambako alionekana akimnog'oneza kitu mpishi mkuu na dakika chache akawa kapotea eneo hilo la hoteli.

Bibi gusa unate aliendela kula kwa furaha huku naye akiwa busy na simu yake mkononi. Ulipita muda bila ya kumwona mwakibubu ili amwambie amwongezee lakini hata kabla ahajasema kitu mhudumu akaja na kumuuliza kama alihitaji tena pombe.

 Bibi gusa unate kwa mbwembwe aliinua kichwa kuashiria kukubaliana huku akimalizia na neno " Mjukuu weka vyombo mezani boss kubwa yupo"

Muda ulizidi kwenda na bibi akaanza kuingiwa na uoga na kujihoji kimoyomoyo au bwana mwakibubu atakuwa ameenda kuniagizia mchemsho mbona kakawia au ngoja nivute subira.
Akiwa katakati ya tafakuri hizo mara alishtushwa na kikaratasi kutoka kwa mhudumu kilichoandikwa namba na alipozisoma namba zile vyema akagundua ni fedha halali kwa malipo ya shilingi 55,800 za kitanzania kama billi.Wakati huo bibi mfukoni alikuwa na shilingi 1600 taslimu.

Wakaanza kujibishana na yule mhudumu kuwa mwakibubu atalipa lakini yule mpishi wa jikoni akaja na kusema kuwa mwakibubu alishajilipia juice yake na chakula alichokula yeye na kusema vingine atalipa huyu bibi.

Bibi gusa unate aliishiwa pozi na akawa hajui nini cha kufanya lakini wazo likamjia kuwa hapo ni kwa kujiongeza ili awatishie wale wahudumu kwa kujitambulisha vyeo vyake.

Akaanza kujitambulisha  kuwa yeye ni BIBI Gusa Unate Mganga mashuhuri wa Afrika mashariki na kati na ni mwekezaji hapa nchini akitokea nchi jirani ya Zambia  na anatibu na kutoa ajira pia ni bwana afya na pale alikuwa  anataka kuonja ubora wa vyakula vya hoteli ile na kuwa amegundua huduma zao ni mbovu na hazina ubora na wako matatani kwani anaweza kutoa ripoti mbaya itakayowapelekea kufungiwa kuendelea kufanya huduma hizo

Walipomumboa kitambulisho hakuwa nacho jambo lililomfanya ashikwe na kuanza safari ya kwenda kituo cha polisi. Wakiwa njiani simu ya bibi iliita na alipoongea na mpigaji aliambiwa aangalie salio lake la pesa kwenye simu.

Kuangalia namba ilikuwa ni kutoka kwa MTEJA MPYA (Chamdoli)  na alipoangalia salio aliona kuna shilingi 62, 000 ambapo akaomba ajaribu kuzitoa na baada ya kutoa aliwalipa na kuanza kuondoka huku akijiongelesha.

Mtoto jambazi aliyekubuhu anadiriki kunidhalilisha sasa mimi leo nitalala wapi na hii hela nimeambiwa niilipe kabla ya saa sita usiku je nitailipaje na huyu Chamdoli anadiriki kunilipia na kuniambia niache upumbavu wa kupenda vya dezo na ukizingatia sauti yake ile ni kama ya kabinti kadogodogo ambako hakana nidhamu aisee hii dunia kweli ni kabambe.

Alianza  kutembea na kwakuwa alikuwa na mawazo hakujua yuko eneo gani na ukizingatia alikuwa kanywa pombe nyingi akashikwa na haja ndogo na akaamua bora ajisaidie kwenye kakichaka kadogo mbele yake.

Ile amemaliza tuu alisikia sauti, " Arooo Umemariza haya nyanyuka juu", ile kugeuka alikutana na gwanda za jeshi kuashiria alikuwa eneo la jeshi na kilichofuata pale ilikuwa adhabu ya  kupiga deki kwenye bwalo la jeshi.

Alipokuja kuachiwa ilikuwa ni mida ya saa sita kasoro dakika tano za usiku huku akiwa kachoka chakali na hajui nini afanye. Wakati anatembea kwa mwendo wa haraka  akitoka eneo lile  mara simu iliita .............................

Je nini kitamsibu bibi ?

Usikose kisa hiki kesho  jioni


Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014

Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

share, like na comment

You Might Also Like

0 comments: