Jamani kuna watu hawaishiwi vioja na hawa watu hunifanya niamini kuwa hakuna siri yaweza kuwa ya kudumu.
Jamani kuna watu hawaishiwi vioja na hawa watu hunifanya niamini kuwa hakuna siri yaweza kuwa ya kudumu.
Jamaa kakaa na mpenzi wake kwa zaidi ya miaka mitatu na wakabahatika kuwa na mtoto mmoja na hatimaye mtoto akawafanya waona ekwa ndoa ya kanisani.
Si wajua bwana masuala ya ndoa za siku hizi asilimia kubwa zasababishwa na binti kuwa mjamzito au bwana kuamua akae tuu na binti aliyemzalisha kwa mkupuo kwani hana jinsi.
Basi jamaa wakakaa kwenye ndoa yao na kubahatika sasa kumuongeza mtoto wa pili katika ndoa yao hiyo na maisha yakawa yanazidi kwenda kwa furaha sana sana sana.
Miaka michache baadae kukaanza kutokea mambo ya ajabu yaani beki tatu wao akawa kila siku akiamka kwenda kuanza majukumu ya siku anakutana na bahasha mlangoni ikiwa na vijizawadi vidogo vidogo
Yaani mle kwenye bahasha kuna kuwa na vichocolate, ice cream mara keki mara soseji mara mikate ya chocholate mara keki mara pop corn za asali na madubwana mwengine mengi sana sana.
Beki tatu akawa anavifungia ndani na kuvila kama kawaida. siku moja mama mwenye nyumba kaingia kwa beki tatu kakutana na baadhi ya mazagazaga hayo na kumuuliza kulikoni asije kuwa anaiba fedha na kununulia.
Beki tatu baada ya kupokea kelebu kama mbili tatu basi ikambidi aseme kuwa naye huwa anaziokota na kuzila. Siku ya pili yake asubuhi mama akawahi na kweli akakutana na mazagazaga yale na yeye akaona ngoja atumie tena bila uoga.
Ikawa siri ya beki tatu na mama kwa muda mrefu lakini siku moja baba akashtukia mchongo na kumdaka usiku beki tatu akiwa anauokota ule mfuko wa mazaga zaga baada ya kujificha kwa muda.
Beki tatu akala kichapo na kusema hata mama huwa anajua mchezo mzima basi mama akamkana beki tatu na ule msala ukawa ni wa beki tatu na mzee akatupa zile zaga zaga.
Lakini sasa kila siku zikawa zinakuja na mzee anaokota na hajui huyo mtu huwa anaweka muda gani.Mzee akaona ajadili na mkewe na kusema kama mwanzo walikuwa wanakula ana hakuna madhara basi wale tu labda kuna mtu anamnyemelea beki tatu wao na anashindwa kuongea maana beki tatu wao aliumbika balaa.
Zikapita kama siku tatu wanakula bila hata ya kuhofia na siku ya nne badala badala ya zawadi akaweka bahasha na yenye ujumbe ndani.
" Leo ni tarehe 6 na ifikapo tarehe 12 ya mwezi huu hamjarudisha kila kitu mlichokula tena sio hela ni kila mlichokula basi mtakufa wote kifo cha ajabu na kabla ya kufa moto mtauona... Asante"
Jamaa wakaokota na kuisoma, unaambiwa wakachanganyikiwa pale na baada ya kujaribu nini wanye wakagundua hawataweza kukumbuka vyote hivyo hakuna jinsi zaidi ya kufa tu.
Siku zilivyozidi kukaribia jamaa na mkewe wakaona waanze kuombana msamahaa kwa kila waliyoyatenda kabla ya kufa hiyo tarehe 12.
Mama akaanza, " mme wangu nisamehe unajua mtoto wa kwanza sio wako kwani ni warafiki yako dan,huyu wa pili kweli ni wako na pia nisamehe kwani nina biashara ya siri niliifungua hapo mtaa wa pili na nina akaunti ya siri ina milioni 10.
Baba nisamehe kwani nimetembea pia na josia ambaye ndie aliyenipa mtaji wa siri wa hizi biashara.
Baba yeye akasema nisamehe mke wangu mimi ndiye niliyekuwa nikiwaletea hizi zawadi nikimtuma Jim aweke usiku kwani nilitaka nikuambie hiyo tarehe 12 wakati wa siku yako ya kukumbuka kuzaliwa maana nilitaka kukuambia pamoja na huu umaskini ila naweza kuwafanya mkawa na furaha kiasi.
Na wewe ukumbuke kuwa hakuna mtu anayeweza kukupa kitu cha bure bila malipo yake kwani nilifahamu juu ya yale mahitaji ya bei nkubwa uliyokuwa ukileta na kunidanganya...... kila zawadi ina malipo yake..
Ungekuwa wewe ndio mama ungefanyeje?
0 comments: