Yaani usiombe uwe na rafiki kanunua gari jipya na tena ni mara yake ya kwanza kumiliki usafiri wa aina hiyo.

11:31:00 Unknown 0 Comments

Hii ndio weekend bwana
Yaani usiombe uwe na rafiki kanunua gari jipya na tena ni mara yake ya kwanza kumiliki usafiri wa aina hiyo.
"Hello fuledi, mambo vipi bwana naomba uje mara moja hapa nyumbani kuna shida kwenye gari" kesi ndio imeanzia hapa
Mimi mbio mpaka kwake kumbuka hiyo ni jana jioni, nafika pale ananiamabia kaka mbona gari haitoki inapiga resi tuu?
Nikamwambia hakuna kitu kama hicho kwani umewekaje?
Mchana niliweka kwenye "D" kama kawaida si unajua D maana yake Day? Sasa usiku huu nimetaka kwenda kumpeleka wife out naweka "N" yaani night naona haiendi au labda imebadilisha majira yaani limezoea kwao maana kule navyojua ni asubuhi mida hii?
Kaka hakuna kitu kama hicho,D= Drive, N=Neutral, P ni Park na R = reverse,.
Basi jioni ya jana tukaachana kwa stlye hiyo.
Sasa leo tena kanipigia asubuhi na kwenda mpaka pale na hana jipya zaidi ya kuniomba nimpeleke sehemu ya kuoshea magari.
Yaani mazungumzo yake ni kuhusu gari mwanzo mwisho na hata kavumbi kakiingia kidogo anatumia mpaka leso yake kulifuta gari lake.
Tumenunua, pafyumu, mp3 player, chaja, seat cover 2 tofauti, air fresh, mito, miwani ya jua ya kuendeshea gari na mapambo mengine ya aina tofauti mpaka gari limekuwa zito.
Ndani kaweka mziki mzito na taa mbalimbali mpaka nahisi x-mas inakaribia nje kaweka stika za man u utafikiri tupo OLD TRAFORD
Pia alivyomakini kaandika siku ya kulifanyia sevisi gari lake ili asije kusahau kitu ambacho ni sahihi kabisa.
Jambo la kuchekesha zaidi kaandika tarehe ya siku aliyonunua gari ili mwakani alifanyie birthday
Mbaya zaidi hapendi wamovateki njiani maana tumekimbizana na gari moja mpaka songwe ili alishinde tu. Mafuta tumeweka zaidi ya mara saba.
KWeli kipya kinyemi
Yaani jamaa anafurahia kutimiza ndoto zake na upande wa pili zinamnyoyoa fedha bila kujua kwani mpaka atakapokuja kulimudu litakuwa limeshampatia hasara ya budget.
Kwa harakahara budget aliyofanya leo kulinogesha gari lake unaweza ukanunua bodaboda moja ya hatari na ukabakiwa na vijisenti vya kusumbulia mjini kwa siku kadhaa.
My Take
Maisha yana mambo mengi sana. Unapopata kitu kipya unatumia nguvu kubwa kuonesha jinsi unavyokijali na kusahavu vile vya mwanzo vilivyochangia kukipata hicho kipya.
Kwa mfano kwenye mahusiano,Kuna watu vilevile huwa na mbwembwe za namna hii kwa wapenzi wapya na mwishowe wanashindwa kuyamudu haya nakujikuta katika migogoro mizito na isiyotatulika kwani jinsi ulivyomchukulia mwanzo umeshindwa kumtunza kwa mwendo ule ule.
Na kama haitoshi utafikiri suluhu ni kumtafuta mwingine......
Kwa mfano wewe unayesoma hii post usikute umekurupukia hii post na kuiacha post ya juu yake....
Maisha ni shida hupendi watu wakuovateki?????

You Might Also Like

0 comments: