Kutoka kwa kaka aliyepigwa vibuti mara nyingi kabla ya kuamua kuoa
Suala la kuwa na mpenzi waweza amua muda wowote ule utakao lakini suala la ni nani atakaa na wewe daima ni suala la wawili kushirikishana na kukubaliana.
Kama mlikutana bar, club au sehemu yoyote ile ya starehe na huyo mpenzi wako kamwe usiamini kuwa ukiingia kwenye mahusiano na hasa mahusiano ya ndoa utaweza kumbadilisha kwa dakika ishirini kama ilivyo rahsi kukubaliana kuingia hotelini na kulala ndani ya dakika hata kumi.
Sumaku hunasa vitu vyenye asili ya chuma na mara nyingi watu twakutana na wapenzi wanaotokana na jinsi sisi tulivyo ingawa wengi hujitahidi kuzificha tabia zetu kutokana na muda mfupi tuutumiao kufahamiana na kisha kutangaza kuwa twataka kuishi pamoja.
Unaweza ukavumilia kwa usiku mmoja na kulala na mtu mwenye kunuka harufu ya pombe, sigara au hata mapungufu mengi aliyonayo lakini huwachukua watu wachache sana kuvumilia hali hizo milele.
Naongea hivi kwani leo kuna mtu akaniuliza inachukua muda gani Fred kwa mtu kuomba talaka na kupewa.... Nilishtuka sana kwani tumemchangia fedha ya harusi mwaka mmoja na nusu uliopita na mbaya zaidi alikuwa na moto wa mapenzi wenye mtetemo zaidi ya simu ya kichina.
Iweje leo aongelee sula la talaka.
Guys, suala nyeti na bovu kuhusu maisha yetu ya mahusiano ni kwamba twatumia mizani feki kwa vitu vyenye kuhatarisha mahusiano yetu na hata furaha na uhuru wa maisha yetu ya baadae.
Wengi twatamani sana ndoa sio kwa maana ya kuelewa maisha ya ndoa ila kuchangiwa zawadi ukumbini na kuona umewaziba midomo watu na kuwa sasa una mke au mme.
Idadi kubwa ya kina dada wao huamini anapoingia katika mahusiano huenda kumbadilisha tabaia mwanaume na baada ya kujaribu na kuona ameshindwa kumbadilisha awe kama vile atakavyo huna na ndoa imeisha. Na haya ni matokeo ya mahusiani ya siku mbili kwenye safari ya gari moshi yanayozaa ndoa bila hata ya watu kufahamiana.
Kwa mtazamo wangu nafikiri kabla ya kufikia maamuzi ya kuoa au kuolewa ni vyema kupata muda wa kufahamiana na huyo mwenza wako kwa muda na kujuana vilivyo hasa tabia, maono, historia zenu, itikadi, elimu zenu, uwezo wenu wa kutambua mambo na jinsi ya kukabiliana nayo.
Inanishangaza ukaingia bar meza tatu tofauti wote wanajadili jinsi mahusiano yao yalivyomabovu na wengine wakidiriki hataka kutoa siri za wapenzi wao .... inatisha sana na kuwakatisha tamaa wale ambao hawajaoana au hata wale wanaofikiria kuoana na kuona ndoa ni jeshi dogo .
Mwisho suala la ndoa ni jinsi wewe unavyotaka iwe ukimshirikisha mwenzio... mnaweza kuchagua furaha, kuheshimiana na kutatua matatzo yenu wenyewe na hutaliweza hili kama huna mapenzi ya dhati kwa mwezio.
Hebu tuukatae ule usemi wa sasa kuwa ndoa nyingi za sasa zasababishwa na mimba wapendano wajitambue na kusema ndoa yao ilitokana na wakati, kupendana na baada kufanya tathmini ya kuwa sasa wanahitaji kuwa pamoja.
Kutoka kwa mjukuu wa Gusa Unate anapatikana HAPA

0 comments: