Nimelia baada ya kukisoma kisa hiki,,... hakika wanawake wana roho ya kikatili...

16:45:00 Unknown 0 Comments

Nakumbuka ilikuwa ni february 14 ya mwaka 2012 majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ambapo nilipokea simu kutoka kwa Mary iliyonifanya niishiwe nguvu na kupandwa na BP.

Ni kitu cha kustaajabisha kuwa kama simu hii angepigiwa mtu mwingine basi saa hiyo na muda huo furaha ingetanda eneo lote hilo na hata baadhi ya watu wa karibu kupewa taarifa ili wafurahie pamoja.

Kwani kuna watu wamekufa, wameachika na hata wengine wamejikuta wakiwa katika mahusiano mapya ili tu wajaribu bahati yao ya kuitwa baba au mama na wengine mpaka dakika hii wanaishia kumlilia Mungu awape miujiza ya kuwa na watoto.

Lakini kwangu siku hiyo ilikuwa mbaya zaidi kwani simu hiyo ilitoka kwa binti ambaye nilitembea nae usiku mmoja tuu baada ya pombe kutupanda kichwani nikiwa njiani kumrudisha kwao baada ya halfa fupi ya kumwaga mama watoto wangu aliyekuwa akienda masomoni nje ya nchi kuisha.

Niliumia sana kwani mary ni rafiki wa karibu sana wa mke wangu hata baada ya kitendo kile sikua na furaha na kila siku nilijitahidi kusahau ila kama wasemavyo wahenga kuwa hakuna mtu anayeweza kukikimbia kivuli chake kwa kuwa kina mjua na kina uwezo wa kumtafuta popote aendako.

Simu hii ilinifanya nijikute naamka haraka na kuondoka nyumbani bila hata ya kukumbuka kuwaandaa watoto kwa ajili ya kwenda shule na muda mfupi nikawa nyumbani kwa mary.

Nilitumia zaidi ya masaa mawili kumshawishi ili atoe mimba ile lakini hatukufikia muafaka kwani alihitaji kuzaa na kuhofia afya yake. Na mbaya zaidi akanipa mkwara mzito kuwa kama nisipomuoa na kuwa mke wangu wa pili basi atanifanyia kitu kibaya.

ofu kozi sikuwahi kuonekana bar asubuhi ila siku hiyo ikanibidi niwahi kwani hofu ilinitanda sio ile ya kufanyiwa  kitu kibaya ila juu ya kuwa na mke mdogo na mtoto mpya katika familia jambo ambalo lingeniharibia heshima kwa familia na jamii inayonizunguka hasa ukizingatia nafasi yangu kanisani kwetu.

Baada ya kama bia tano hivi nikajikuta napata ujasiri wa kupindukia na kumtumia meseji nzito mary ya kuwa afanye chochote mie siogopi na kuwa hata iweje siwezi kuwa nae kwani naipenda familia yangu.

Tulijibishana sana sms na nakumbuka mwisho wa siku akaniambia sasa anaondoka na kuwa anafanya kitu ambacho kitaninyima uhuru daima. Nikampa maneno makali na kisha nikaendelea kunywa.

Mmmmh kuna muda hofu ikanishika kwani kuna kama sms 5 hivi nilimtumia na hakuwa amejibu kitu, hivyo wasiwasi ukanijaa na kuamua niende nyumbani kwake nikajaribu kumpa maneno ya kumfanya ashushe hasira ili tuweke sawa na lisiharibu hadhi yangu.

Nilifika pale nyumbani na kuona mlango uko wazi na niliposogea sebuleni kwenye sofa lake nikaona kuna dalili ya damu, hofu ikanijaa zaidi na nikaona nimwendee chumbani kwake ambako pia nilipatwa na mstuko mkubwa baada ya kuona damu nyingi kitandani kwani mlango ulikuwa wazi.

Nikaogopa sana na kutoka haraka hapo nikihofia kama kunaweza kuwa na mauaji na kikahusishwa.Hivyo breki ya kwanza ikawa nyumbani kwangu ambako pombe zile zilizokuwa kichwani zikanifanya niangushe usingizi mzito.

Nakumbuka nilikuja kushtuka mida ya saa moja kasoro na nilipoishika simu yangu nikakutana na ujumbe wenye picha kutoka namba ngeni kupitia whatsapp. Picha ilinionesha mie nikiwa naingia kwa mary na kutoka na kisha ujumbe ukasema " hatumwoni mary ila leo mtu mwisho kuwa na mary ulikuwa ni wewe, hivyo tunaomba tujue ndugu yetu yuko wapi"

Shuzi moja matata ilinitoka na kujikuta nikitokwa na maji usoni akili ya haraka ikanifanya niangalie kama juu ya paa kuona kama kumetoboka na mvua inanyesha lakini sikuona kitu mpaka pale akili iliponirejea na kugundua lilikuwa ni jasho.

Ghalfa nikasikia muungurumo wa gari na nilipochungulia nikagundua ni polisi, niliiangalia picha ya mke wangu pale ukutani na kusema kimoyomoyo, "nisamehe mama yaani usiku mmoja tu wa furaha sasa unanifanya niinchungulie hukumu ya kifo" kisha nikausohelea mlango ili kuwafungulia polisi wale waliokuwa wakiugonga mlango kwa nguvu.

Aliingia polisi mmoja wa kike ambaye kwa kweli alikuwa kaumbika balaa na kwa mshangaao akaja na kuninong'oneza kitu sikioni na kunifanya nistuke na kupiga kelele kama kichaa muda huu hapa ofisini, kumbe kuna jamaa alikuwa akiniamsha maana nakoroma mmno muda wa kazi

ndoto za kazini taamu

Posted by Fred Kihwele · 51 mins · 
Kitabu cha Boma kilichoandikwa na Fred Kihwele ki tayari. Nakala moja inauzwa shilingi 5,000/=
Kitabu cha Boma kilichoandikwa na Fred Kihwele ki tayari. Nakala moja inauzwa shilingi 5,000/=. Unaweza kuagiza sasa moja kwa moja kupitia kwa mwandishi wa kitabu kwa namba 0713 317 171 /...
KARIBUMBEYA.COM
27 people reached
Like ·  ·  · 240
Posted by Fred Kihwele · 3 hrs · 
ISANA TRAVEL AND TOUR SERVICE
Offer for International flight From Dar es salaam international airport - London - Tokyo - Mumbay - Beijing From Kilimanjaro international airport - London - Tokyo - Mumbay - Beijing From Za...
KARIBUMBEYA.COM
51 people reached
Like ·  ·  · 22
Posted by Fred Kihwele · 3 hrs · 
Dubai Aluminium Profile
Tunauza na kutengeneza Aluminium kwa bei nafuu. Tupo Kabwe mkabala na kanisa la Full Gospel . Wasiliana nasi ka namba 0652885006
KARIBUMBEYA.COM
36 people reached
Like ·  ·  · 1
Karibu Mbeya updated their cover photo.
4 hrs · 
Like ·  ·  · 4
Posted by Fred Kihwele · 7 hrs · 
DOLPHINE SIGN ART
Dealers in production of BANNERS, CALENDER, GRAPHICS DESIGN, BROCHURE, STICKER, LOGO DESIGNING, BUSINESS CARDS, POSTERS, TYRE COVER, FLYERS, T-SHIRT PRINTING, CAR & SALOON BRANDING, KEY...
KARIBUMBEYA.COM
14 people reached
Like ·  · 
Always be thankful in what you have. Even if it’s a problem. Problem will gives you learning and experienced and happiness from things, blessings. So why do you need to be sad if you can think about the positive things that you can get?
123 people reached
Like ·  ·  · 6
Katika siri ya mafanikio kuna vitu vitatu lazima vizingatiwe.
1. Jiulize unaitaji nini ktk maisha yako.
Apa lazima uzitambue ndoto zako au malengo yako. Chukua kalamu na karatasi andika ndoto zako. Kisha jiulize unataka maisha yako yawe ya namna gani kisha andika kwenye karatasi.
...See More
SIRI YA MAFANIKIO Habarini za leo ndugu zangu,nifuraha yangu tena kukutana na nyie leo hii katika harakati za kupambana na uyu adui yetu umaskini. Napenda niongelee topiki hii ngumu kidogo i...
KARIBUMBEYA.COM
326 people reached
Like ·  ·  · 55
Anza wiki mpya kwa kuipa sauti biashara yako na kuifanya ifahamike na watu wengi zaidi kupitia tovuti yako uipendayo ya www.karibumbeya.com

Ni rahisi sana, jambo la kufanya ni kuibofya link hii na kisha fuata maelekezo
...See More
Complete the fields below to create your free account. Your login details will be emailed to you for confirmation so make sure to use a valid email address. Once registration is complete, you will be able to submit your ads.
KARIBUMBEYA.COM
270 people reached
Like ·  ·  · 2116
5 JAYS CURIO SHOP, Tumefungua duka linalouza Vitu Vya Asili maeneo ya Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya, Duka hili linauza vitu mbalimbali vya Asili kama vile nguo, Viatu, pochi/Mikoba aina tofauti, Vikoi, sandals, Kofia, Mashati ya kiume, urembo, vitu mbalimbali vya nyumbani, na Vinyago kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika.
5 JAYS CURIO SHOP, Tumefungua duka linalouza Vitu Vya Asili maeneo ya Uwanja wa Sokoine, Jijini Mbeya, Duka hili linauza vitu mbalimbali vya Asili kama vile nguo, Viatu, pochi/Mikoba aina to...
KARIBUMBEYA.COM
26 people reached

You Might Also Like

0 comments: