MAMBO 16 AMBAYO KAMA UPO KWENYE UHUSIANO AU UNATARAJIA KUWA NA UHUSIANO NA BINTI/KIJANA UNATAKIWA KUYAZINGATIA KIKAMILIFU
00:19:00
Unknown
0 Comments
00:19:00 Unknown 0 Comments
1. Huwezi kuwapenda watu wa nje kama huna mapenzi ya dhati kwayule uliyenaye kwenye uhusiano sasa.
2. Kumsaliti mwezio kwa kisingizio cha kulipiza kisasi huwa njia rahisi ya kukuingiza katika mgogoro binafsi na mwishowe kukuharibia kila mipango yako.
3. Kamwe usijidanganye kuwa utaweza kumsaliti na kumdanganya mwenzio kwa muda mrefu bila kugundulika, kila usaliti ni sawa na mimba lazima kuna muda utafika kila mtu ataiona tu.
4. Mahusiano yoyote hujengwa na uaminifu na kuthaminiana huku neno samahani na nimekusamehe likiwa nguzo kwa utatuzi wa kila tatizo mbele yenu.
5. Kusema nisamehe sio kuonekana mjinga bali pia huweza kukupa heshima na kuongeza mapenzi ya dhati baina ya yenu.
6. Neno nitakuacha au tuachane isiwe silaha ya kumwonea mwenzio maana nalo likizoeleka huweza kumfanya mwenza wako kuchukua maamuzi magumu kwani huashiria wewe una watu huko nje wakupao kiburi.
7. Kamwe usiwe mwepesi wa kuamini nini watu wanasema ila mshirikishe mwenzio kila uvumi ukoonyesha kumwamini na kumpa nafasi ya kukupa ufafanuzi.
8. Kila mahusiano huja na Baraka zake na huondoka na Baraka zake, unaweza ona unapata mafanikio sasa kwa sababu ya kuwa na huyo uliyenaye. Hivyo jitahidi kuzitazama kwa makini kila fursa njema upatazo na ona je zikiondoka utakuaje.
9. Fedha huleta ufahari lakini kamwe haina mchango katika kuleta furaha kwenye mahusiano yenu, hivyo pendaneni kama vile ni matajiri na maskini, kwani fedha yaweza kupotea muda wowote na kama mnapendana itarudi pia kwa kushirikishana jinsi ya kuirudisha lakini mapenzi yakiisha hata uwe na gunia la pesa ni kazi bure sawa na kuirudisha ladha ya chumvi siku ikiisha.
10. Mahusiano ya wawili hupendeza kama hayataingiliwa na watu wengine nanyi mkishirikishana katika kutatua matatizo na kuwa na maamuzi ya pamoja kwa kila jambo.
11. Ni vyema kutengeneza mazoea ya kujivunia na kuona ufahari kwa huyo uliyenaye na kama ukishindwa kuyafanya hayo kwa huyu hata ukimpata mpya mchezo utakuwa huo huo kwani bado huna ujuzi wa kuishi na mwenzako.
12. Huitaji kuwa dikteta kwa kuwa na misimamo ya kikoloni bila ya kuwa na utambuzi wa kuwa mko watu wa wili hivyo acha tabia za ubinafsi.
13. Wanawake wazuri na wanaume wenye mvuto hawawezi kwisha amini uliyenaye hukumpata kwa bahati mbaya, mpende kwa dhati.
14. Kila maamuzi ufanyayo sasa ukiwa na stress au huna sress huwa na tabia ya kuihaibu kesho yako, hivyo jitahidi kuwa na subira katika kila jambo.
15. Mapenzi hayaonyeshwi kwa kufungua zipu au kwa binti kupanua miguu tuu, mapenzi ni hisia, jinsi mnavyoishi, maelewano, ushirikiano na mambo mengine mengi.
16. Upendo hausubiri siku ya Valentine, kila siku ifanye kuwa siku ya valentine kwa mpenzi wako.
Mambo ya muhimu kuzingatia unapokuwa na rafiki katika maisha yako.
1. Usiwe mwepesi wa kutoa lawama na kumhukumu kwa kila jambo ila jaribu kumwelewa na kumfanya akuelewe wewe pia
2. Usijifanye kuwa wewe ni wa muhimu kuliko yeye ila amini yeye ni wa muhimu zaidi jambo litakalo mfundisha nae kukuona wa muhimu
...See More
Kijana asiye na kazi aitwaye Nolesy aliamua kumwoa rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa akifanya kazi katika benki moja mashuhuri.
Nolesy alijitosa katika ndoa licha ya hofu na ushauri mwingi aliopewa na ndugu kuwa ni vibaya kuoa ukiwa huna kazi.
Kila mwezi yule binti alimpa mmewe mshahara wake wote wa 800,000 baada ya kutoa fungu la kumi kwa ajili ya kanisani.
...See More
Dada mmoja alihitimu chuo na kutafuta kazi kwa muda mrefu sana kiasi cha kukaa mika 15 akiwa hana kazi. Mbaya zaidi katika kipindi hicho alipata wakati mgumu namna ya kupata fedha za kujikimu.
Siku moja akawa na elfu tano tu na akaingia katika hoteli moja ili aweze kupata chakula cha mchana, akaketi na kuagiza chakula chake.
Baada ya kuletewa akasali na kabla ya kula chakula wakaingia wazee watatu wakionekana wamechoka na wanajaa pia....
See MoreFuledi Mwagito
Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii adimu sana ya kufurahi, kuelimika na kubadilishana mawazo. Nitafurahi sana kama utaniachia comment hapo chini ili nijue kama habari,ucheshi, simulizi na vioja vioja hivi vimekupa siku yako kuwa BOMBA. Kumbuka nawe waweza share nami chochote ulichonacho kwa kunicheki kupitia whatsapp kwa namba 0713317171 au kupitia comment. Asante.
0 comments: