00:29:00 Unknown 0 Comments



Mama yake mtafya aliwmsomesha mtoto wake kwa taabu na shida nyingi hasa baada ya baba yake kufariki.
Mtafya akafanikiwa kwenda nje ya nchi kusoma na baadae kurejea nchini na kupata kazi nzuri sana.
Akakaa mjini zaidi ya miaka miwili akigoma kwenda kumwangalia mama yake kwa madai kuwa ni mama mshamba asiye wa kisasa na kuongea nae au hata kumkaribisha mjini ni sawa na kujidhalilisha mbele ya marafiki zake waishio kisasa.
Mama yake mtafya akaanza kuugua na siku moja Nolesy ambaye ni rafiki wa karibu wa mtafya akaenda kijijini na kuamua kupita kumsalimia mama rafiki yake na kushuhudia akiwa taabani kwa kuumwa.
Akaambiwa mtafya alirudi weekend na aliponwona anaumwa alimpa shilingi elfu mbili ili anunue dawa kwani sio lazima kwenda hospitali.
Kwa hasira Nolesy akamchukua mama yake mtafya na kumpeleka mjini na kumwambia mtafya amuhudumie kwa kumpeleka hospitali.
Mtafya akamchukua na kumpeleka hospital na hakumhudumia wala hakumtafuta mtu wa kumhudumia na hakuonekana hospital.
Nolesy akaaamua kumlipia bili zote na alipotaka kumpeleka nyumbani kwa mtafya, mtafya alikataa akidai kuwa ni mwanamke mchafu ikambidi Nolesy ampeleke kijijini na kuendelea kumtunza kwa muda kabla ya kurudi mjini.
Mama mtafya alilia na kuhuzunika kwa jinsi mtoto wake alivyobadilika na kumwacha mama yake alieyemlea kwa shida na machungu mara baada ya baba yao kufariki.
Miezi michache baadae mama akafariki na kuja kugundulika baaada ya mwili wake kuanza kutoa harufu kwa kuwa hakuwa na mwangalizi pale nyumbani.
Miaka miwili baadae mtafya akapatwa mamatizo ofisini kwake na kusimamishwa kazi, akaamua kuchukua akiba akiyojiwekea na kuingia kwenye biashara ya magari kabla ya kuingia mkenge wa kutapeliwa na kupoteza kiasi kikubwa cha fedha.
Biashara zikaanza kusuasua akaamua kuchukua mkopo ambao haukuchukua muda akashindwa kulipa na kufilisiwa mali zote zilizobaki alizokuwa akimiliki.
Mtafya akaanza kuhangaika akilia kutafuta kazi na kila alikokwenda hakufanikiwa na marafiki wakimbia jambo lilimpa wakati mgumu na hatimaye kuanza tabia ya wizi ambayo nusura kifo kimkute kabla ya kumwacha akiwa hana vidole viwili vya mkono.
Mpaka leo mtafya hana mafanikio karudi kijijini kila siku analia akilisafisha kaburi la mama yake bila mafanikio na hali yake ikizidi kuzorota na hapati kazi na hakuna amwaminie pamoja na elimu yake.
*Rafiki hakuna mtu nwenye mchango mkubwa katika maisha yako kama mama
*Elimu, utajiri na umaarufu havina kazi yoyote kama huna busara na moyo wa shukrani kwa ujasiri na uvumilivu na matendo mema ambayo mama yako aliyafanya kwa ajili yako
*Una kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kukupa mama na baba yako kwani kuna watu wengi wamekosa nafasi hiyo na wanatamani waipate
*Usisubiri mpaka mama yako apotee hapa duniani ndio uanze kuhisi kuwa kuna upendo hukuuonyesha
Anza leo kumpenda mama kwa kumwonyesha upendo, kumshukuru kwa kila gumu alilopitia katika kukukuza na kukufanya uwe kama ulivyo.
Comment "Nakujali Mama" kisha share kama una kila sababu za kumshukuru Mungu kukupa wazazi/walezi
ONYO: KAMA HUJAWASILIANA NA MAMA YAKO AU MLEZI WAKO TANGU JANUARY IANZE NA YUPO HAI USIANDIKE CHOCHOTE

Happy Women's Day



Posted by Fred Kihwele · 3 hrs · 
Napokea oda za kusambaza fruits salad kwenye maofisi na kwenye sherehe/party
Napokea oda za kusambaza fruits salad kwenye maofisi na kwenye sherehe/party. 0767634082
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: