Japo najua nitakachoongea ni kama pumba ila nisikilize tu aisee!

16:45:00 Unknown 0 Comments

Mwanamke mwenzangu!...nisikilize!...
Japo najua nitakachoongea ni kama pumba ila nisikilize tu aisee!
Sometimes na mimi huwa naongea pumba zenye maana hahahaaa.... DADA kama bado hujabeba mimba na kuzaa hasa wale ambao bado hamjafungamana na mtu na hata mnaotarajia kufungamana ila tayari ndiiii au mmeshafungamana…. Ustawi wa jamii kuna wake za watu kibao ukooo hivyo usidhani haikuhusu nisikilize tu…..!!
Kuna waliobahatika kupata wanaume wanaojielewa… wanaojua wajibu wao na wanaojitambua haswaaa linapokuja suala la kuhudumia familia…. wewe na mtoto au watoto… na huyu utamjua kiumbe akishakuja…usijidanganye kwa kutazama kazi yake sijui umri sijui zagazaga gani unakaotea huyu atakuwa family man…shoga unaweza ukajikuta unamtafuta Joyce kiria kushtakia dunia ohoooo! kila siku nasema hawana muamana hawaaaa usikiii!?
Siku ile unapogundua u mjamzito akilini mwako jua huo ni mzigo wako!... yaani jiandae kisaikolojia kuwa huyu mtoto ni zawadi yangu….ni mzigo wangu…ni jukumu langu….. ni wajibu wangu…. Trust me! you won’t be disappointed akianza drama zake!!
Hawa viumbe baadhi ni janga la kitaifa ….ni msaada wa ziada kwenye malezi maana akili zao Mungu tu anajua…. Na ukitaka kujua ni msaada wa ziada waulize single mothers kadhaa…. Nenda pale ustawi usikilize kesi zilizopo…. Nenda Tawla…nenda Tamwa…. Ndio utajua nazungumzia nini hapa!
Usibebe mimba na akili za kuwa ni mimba yenu na mwenzio….dadaaaa utatanga mitandaoni humu kuomba ushauri mpaka ukome!... we ukibeba jiandae kulea…mwenzio akikusaidia Hewala shukuru Mungu na akileta ngebe ngebeni fanya yako tu sio kwa system hizi za kibongo zinazoweza kumbana mwanaume kirahisi akuhudumie…vinginevyo uandae fungu la pesa kukimbizana naye mahakamani sijui wapi uko…. Muda huo si ukachague vitenge kariakoo utembeze maofisini!!
Wapo wanaume wengi sana ni mababa jina tu… kazi yao kujiproud uko nje ‘like faza like son’ huku ndani ni majanga matupu…mizigo imewaelemea wanawake vibaya mno…. Si ajabu kusikia amezaa mlemavu mume kakimbia… (rejea kesi ya mbunge wa zenji kukimbia mtoto mlemavu)… amezaa wa kike tupu mume kawatelekeza…
Hivyo dada usitake kutumia nusu ya maisha yako kwenye majuto na maumivu ya kutelekzwa kiasi cha kupoteza muelekeo wa maisha kisa tu bwana kakimbia…. Wewe jiandae kisaokolojia tu kuwa mtoto ni wako mengine majaaliwa!!....
Atakapokuja baadaye sasa mikono nyuma akidai mtoto amtambue sijui haki za mtoto kumjua baba hapo ni juu yako…kwangu mimi nadhani atanikumbuka maisha yake yote baada ya hiyo siku atakayojitokeza kudai mtoto! Maana atasimulia watu wake wa duniani hadi wa kaburini!! !....
UMENIELEWA LAKINI?.....


Credit: Laura Pettie


WALENGWA:
Wanaoanza kabisa (Beginners Class)
Wenye uzoefu kidogo (Intermediate Class)
Utaalamu maalumu (Master Class)
Ada
FASHION & USHONAJI Beginners-200,000 kwa mwezi(Husoma kwa miezi miwili)
Intermediate-250,000(Huchukua mwezi mmoja tu)
Master class-400,000(Huchukua wiki sita)
UREMBO NA SALON Salon anayeanza kabisa-250,000 (mwezi na nusu, Anyeongeza ujuzi kwenye mambo ya salon-200,000 (Huchukua mwezi mmoja)
Utaalamu zaidi-Maharusi, Make up zote, kufunga vitambaa-make 350,000

TRUE ROAD COLLEGE of FASHION DESIGNING, TAILORING & SALON STUDIES MAHALI: DAR WEST- TABATA MASOMO: YANAYOFUNDISHWA 1....
KARIBUMBEYA.COM



Posted by Fred Kihwele · 5 hrs · Edited · 
Mwezi huu www.karibumbeya.com tunapenda kumpongeza Josepher wa GODRICH HEALTH CENTRE kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwa elimisha watembeleaji wa tovuti yetu juu ya masuala ya afya na ujasiriamali.
Unaweza kufuatilia post zake kupitiahttp://karibumbeya.com/author/josepher/
Nawe unawe unaweza kutoa elimu au kuitangaza biashara yako bure kwa kuifuata link http://karibumbeya.com/register/

CHUNUSI NA MADOA YATOKANAYO NA CHUNUSI AU KUUNGUA NA JUA Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hushambulia sehemu za usoni na kuharibu sura ya mwanadamu hasa wanaw...
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: