SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 2
SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 2
Ilipoishia
" maskini samira pole sana mwanangu, mimi shangazi yako kabisa ingawa nilikuja siku moja tu ya msiba wa baba yako na nikafukuzwa kwenye kikao na siku chache baadae nilihama kutoka mji niliokuwa ninakaa ambao pia ulikuwa mbali na kwenu na kuja hapa na mjomba wako, tutaongea vizuri kesho haya jiandae ule chakula"
Usiku huo haukuwa na maneno ya ziada zaidi ya kila mmoja kuwahi kulala huku nyumba nzima ikiwa imezingirwa na furaha yenye maswali mengi ndani yake
Endelea
Siku ya pili yake asubuhi Aunt Amina aliwahi kuamka na kila mmoja akaelekea kwenye mihangaiko yake na huku nyuma walimwacha samira akiwa katika dimbwi zito la mawazo na kujiuliza maswali mengi.
" hivi ni kwa nini baba mkubwa aliamua kunifanyia hivyo? na kwa nini aunt alifukuzwa kikaoni?"
Haya ni baadhi tu ya maswali aliyojiuliza samira huku akianza kupatwa na taswira sahihi ya maisha yake na familia yake na ni wakati huu ikamjia picha ya mtoto walikwenda kumwona hospitali ingawa yeye alikuwa mdogo kiasi cha kushindwa kukumbuka kwa usahihi juu ya mtoto huyo uhusiano wake na familia yao.
***
TUKUNYEMA BAR
Ilikuwa ni jioni moja katika bar ya Tukunyema alionekana Mzee Zombo akiwa kwenye meza moja iliyosheheni vinywaji huku ikiwa na mabinti na baadhi ya wapambe waliozunguka meza hiyo na kumfanya Mzee Zombo a.k.a Bilionea la ukubwani kuonekana kwa taabu.
Wapambe wale walikuwa wakimpa mzee zombo kila aina ya sifa na kumfanya ainuke mara kwa mara na kuanza kuwarushia fedha huku wengine akiwamwagia vinywaji nao wakifurahia na baadhi wakiongezewa vinywaji.
Pembeni kuna baadhi ya wateja nao walikuwa wakimshangilia na wengine wakiyatamani maisha yale lakini wachache walishindwa kujizuia na kujikuta wakinong'onezana.
" Huyu mzee alikuwa maskini sana na historia yake ni kuwa hata shule alikimbia......" hata kabla ya kumaliza maongezi yale kijana mmoja ambaye ni shushushu wa Mzee zombo aliyekuwa amekaa pembeni alinyanyuka na kwenda kumnong'oneza mzee zombo.
" Mfalme, nina taarifa za kishushushu, niruhusu kukuambia"
" Sema! sema! kijana nani nataka kuharibu hali ya hewa hapa?"
" Nimesikia wakinong'onezana kuwa wewe ni gaidi namba moja wa kimataifa na kama haitoshi wanamashaka na utajiri wako, kwani wewe boss umeishia darasa la ngapi?"
" pumbavu! pumbavu! wewe wakuniuliza mimi nimeishia darasa la ngapi? do you know what time is it you pig son? kama ningekuwa sijasoma shule ningewezaje kukutukana kiingereza?" alifoka mzee zombo huku akimzaba vibao yule kijana
" sio mimi boss wameongea wale vijana" aliongea kijana yule huku akiwanyooshea kidole wale vijana ambao hata kabla ya mzee kuongea neno walishaanza kutabasamu kutokana na maneno ya mzee zombo
Alinyanyuka kwa haraka mzee zombo pale alipokuwa amekaa na kuwaendea wale vijana, " nyie vijana!!! mnafikiri kila mwenye mvi ni mzee? wengine wanafanya kazi kwenye mashine za kusagia nafaka, habari zenu nimezipata, mnahoji juu ya utajiri wangu? mimi mtoto wa mjini toka kitambo sana.
Kwanza ile nyumba nikaayo ni ya kwangu, maana nimeanza kusikia hapa mjini kuna watu wanadai ile nyumba ni ya mdogo wangu na mimi nimehamia baada ya yeye kufa na mkewe.
Mimi niliijenga nyumba ile na kumpa mdogo wangu ili mimi nikae kwenye kale kanyumba kadogo na kabovu ili nijaribu kuona maskini mnapata taabu kiasi gani, na nimeichukua nyumba yangu na kuanza kukaa baada ya mdogo wangu kufariki lakini nashangaa mnaanza kuleta majungu yasiyo na msingi.
Ni upendo wa aina gani mpaka niamue hata kumpeleka mtoto wa pekee wa mdogo wangu kusoma nje tena ulaya na sio ulaya vijijini bali ulaya mjini city center.....Wengine hapa hata kukaa na paka tuu mnashindwa upendo kama huu mtaupata wapi? ilitakiwa mnisifie na kunifanya mfano wa kuigwa
Sasa nyie vidudu ambao tena hamna mbele wa nyuma mnaanza maneno au hamkupitiwa na ofa wakati nimesema bar nzima mnywe kwa bili yangu?
Mhudumu wape hawa kreti moja kila mmoja" alimaliza mzee zombo huku akianza kuondoka kwa madaha
" mzee sisi hatutaki bia zako na ukweli ni kwamba wewe shule huna na mjini waishi kwa mipango feki na kama ungekuwa na uchungu wa fedha hizo kamwe usingetumia kipuuzi hivyo" aliongea mmoja wa vijana wale na kuondoka eneo hilo
Mzee zombo alirejea kukaa kwenye nafasi yake huku akionesha tabasamu la hasira, " kunyweni!, kunyweni! hapa ni burudani tuu achaneni na vijana wenye hila zao"
Hazikupita dakika nyingi mzee zombo a.k.a bilionea la ukubwani alinyanyuka na kuondoka akiwaacha vijakazi wake kwa ahadi za kurudi baadae huku akionekana mwenye mawazo mengi na aliendesha gari kwa umbali fulani na kisha akasimama.
" hivi binadamu wakoje? mbona wanapenda sana kufuatilia mambo yasiyowahusu? hivi hela za mdogo wako si za kwako? na elimu inahusiana vipi na matumizi tena bar? au natakiwa ninywe kwa calculator? wameniudhi sana wale vijana na nikionana nao naweza hata wagonga na gari"
Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo yasiyo na msingi wowote mara dirisha la gari lake liligongwa na alipolifungu alikutana uso kwa uso na..............................
Je nini kitamsibu mzee zombo a.k.a bilionea la ukubwani?
Asante kwa Karibu Mbeya kuirudisha hadithi hii
Itangaze bure biashara yako kupitia http://karibumbeya.com/register/
Itangaze bure biashara yako kupitia http://karibumbeya.com/register/
Unaweza kuwa mdhamini wa simulizi hii au kutumiwa TELEGRAM kwa kuwasiliana nasi kwa namba
0 comments: