SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU LANGO LA MOTONI CHAPTER 1

10:48:00 Unknown 0 Comments

SIMULIZI YENYE UKWELI WA KUUMIZA JUU YA MAISHA NA MATUKIO HALISI YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU
LANGO LA MOTONI
CHAPTER 1
JUMAMOSI YA TAREHE 14.3.2013
Majira ya saa tisa na dakika arobaini na saba kulionekana dada mmoja ambaye hakuonekana nadhifu kwa mwonekano wa mavazi yake pamoja na nyewe zake zilizoonesha kutimka kama vile alikuwa akikimbizwa na kitu au yupo katika dimbwi la mawazo.
Dada huyu bila hata ya kuangalia upande wa pili yake kama uko salama ili avuke barabara yeye alianza kuvuka na hata kabla hajamaliza alishtushwa na kelele za watu waliokuwa wakimtahadharisha na kufuatiwa na mshindo mkuu uliofanya arushwe upande wa pili wabarabara na gari hilo lililosabasha mshindo huo kusimama mbele kidogo.
Alishuka mama mmoja ambaye kwa mwonekane alionekana kuwa ni mtu mweye uwezo wa kifedha na ndani ya gari kulionekana watoto wawili na dada zao ambao walikuwa na furaha muda mfupi uliopita na furaha hizo zilisitishwa na mshtuko wa kile kilichoteokea mbele yao.
Mama alifika pale alikoangukia binti na wakati huo watu walianza kukusanyika huku wakipiga kelele za kutaka mama huyo apigwe kwa kusababisha ajali hiyo.
Mara wakatoeka wasamaria na kumsaidia mama yule kumbeba binti huyo na kumwingiza kwenye gari la mama na kisha wakaondoka kwenda kumwahisha hospitali.
Walifika hospitali na baada ya kupewa huduma ya kwanza binti huyo alibainika kupatwa na mshtuko na hakuwa ameumia. Hivyo akapewa dawa na kuruhusiwa ili aende akapumzike nyumbani kwa ahadi ya siku ya pili yake arejee ili kwa uchunguzi zaidi.
"pole sana dada, naomba nisamehe na sijui uliingiaje barabarani, kwani nilikuona kwa mbali ukiwa pembeni tena mbali ya barabara, punde si punde nikashangaa uko ubavuni mwangu"
" Mama!! Tafadhali naomba usiseme samahani, nashukuru kwamba niko salama na naomba mimi nikuombe samahani" alimaliza kuongea binti huyo huku akijivuta kuanza kutaka kuondoka eneo hilo.
" Dada naomba nikupeleke nyumbani kwako ili nipafahamu na kesho niweze kuja kukupitia turudi hapa kwa uchunguzi zaidi"
" Hapana sina nyumba"
" Huna nyumba kivipi? mbona sikuelewi dada au bado unamshtuko?"
" Niache tu mama, asante kwa ukarimu niache niondoke"
" hapana, Binti naomba basi hata twende ukapumzike kidogo na baadae utaondoka" Alimalzia kuonge amama huyo huku akimshika mkono na kumsaidia kumpeleka maegesho ya magari na muda mfupi baadae walikondoka na kuwasili nyumbi kwa mama huyo.
Wakati wote huo wale watoto pamoja dada zao wao walikuwa kimya wakimwangalia mama yao aliyeonesha kuchanganyikiwa na tukio la siku hiyo huku wakiwa wamekatishwa furaha yao kwani mtoko wa siku hiyo uliishia kutiwa doa na ajali.
"poleni wanangu tutaenda siku nyingine mungu akitujalia na wakati huu nitawapeleka hoteli nzuri zaidi tuombe uzima baba yenu akiwa karudi salama"
" Sawa mama" aliitikia dada yao mkubwa huku akiwasaidia wadogo zake kushuka garini na muda mfupi familia nzima ilikuwa sebuleni ikitazama tamthliya ya simu ya ajabu na wote walikuwa wakiwa katika furaha hasa wakimwona bibi mmoja aitwaye gusa unate alivyokuwa akitetemeshwa na simu mmoja kutoka kwa mpigaji asiyefahamika.
Lakini binti yule aliyekoswa kugongwa na gari alionekana akiwa na tabasamu lililokosa matumaini huku fikra zake zikionesha kuwa alikuwa dunia ya peke yake tena yenye maumivu na kila aina ya kukataliwa na watu wanaomzunguka.
Machozi yalianza kumtoka dada huyu na baada ya muda alishindwa kujizua na kujikuta akitoa kilio cha chinichini na hii ilizidi baada ya kuona familia ile ikiwa na furaha.
Wenyeji wake walishtushwa na kufadhaishwa na hali ile, kwa busara mama alimwomba amchukue binti yule na kumpeleka chumbani ili ampumzike kwani alihisi kuwa binti huyo ana ana jambo zito na kwa muonekano wa kawaida ni kwamba amefikia kiwango cha mwisho cha kulihimili jambo hilo.
"Dada naomba nikuoneshe sehemu yako ya kupumzikia"
" Nina muda mrefu sijawahi kupata usingizi, ni bora nikae hapa nione mkifurahi itanifariji zaidi na kama waweza naomba maji ya moto kwenye kikombe ninywe"
" yawekwe chochote maji hayo?"
" hapana, ila kama kuna kahawa ningependa"
" ipo" alimjibu mama huyo huku akienda kummwandalia maji hayo na kumletea muda mfupi baadae na wakaendelea na mazungumzo.
Ilikuwa imeshatimia saa tatu za usiku na watoto walikuwa wakisafisha meza baada ya chakula na mama pamoja na mwenyeji wake walibaki pale sebuleni wakiwa wawili huku wakiongea.
" samahani sikujitambulisha mimi naitwa mama ukundi na mimi ni mwalimu ambaye nimeamua kujiajiri na pia mkurugenzi wa taasisi moja ya kina mama hapa mjini, na pale tulikuwa njiani nkwenda na watoto sehemu kwa ajili ya mapumziko na chakula cha jioni"
" Asante dada, mimi naitwa MARIAM..................."
***
"Samira! Samira! Samira! bado umelala? amka mwanangu jiandae kwenda shule na mimi nataka kuwahi hospitali kumwangalia mtoto ili nawe nikupeleke ukamwone haraka na kisha uwahi shuleni" ilisikika sauti ya mama samira ikimwita ili kumwamsha samira aliyekuwa bado amelala na wakati ni muda wa kujiandaa kwenda shuleni.
Samira alimaka na kusaidiwa na dada wa kazi kujiandaa na muda mfupi baadae alikwa kwenye gari pamoja na wazazi wake na wakati huu walikuwa wameshatoka hospitali kumwangalia mtoto na sasa walikuwa wakimpeleka shuleni na muda mfupi walimwacha shuleni na wao kuondoka kuelekea kazini kwao.
Wakiwa njiani kabla ya kufika kazini ghafla lwalimwona mtoto mmoja mdogo akiwa anasimamisha gari kama alihitaji msaada wa dharula. Bila hiyana baba samira alisimamisha gari lake na kushusha kioo ili aweze kuongea na mtoto huyo.
Mara wakatokea vijana wawili waliokuwa waliokuwa wameshika vitu mkononi na kuwapulizia wawili wale na kisha kutokomea kusikojulikana. baba samira na mama samira walianza kupiga kelele za kuomba msaada kabla ya kujikuta wakiishiwa nguvu na hatimaye gari moja likasimama pembeni na mtu mmoja akashuka na kuwachukua na kuwapeleka mpaka hospitali ambapo muda mfupi baadae walifariki dunia.
Zilipita wiki kadhaa na siku moja walionekana watu kama saba wakiwa kwenye kikao cha familia na mmoja wao alikuwa ni samira akiwa na wanafamilia wengine.
Pamoja na kuwa na umri mdogo tena wa miaka minne tu lakini samira alionekana akilia kwa uchungu baada ya kusikia kauli kuwa " kuanzia sasa samira atatakiwa kuhamishwa shule na kwenye nyumba ili iuzwe na yeye atatafutiwa shule nyingine, na kwa kuwa yeye ni mtoto wa kike hata husika katika mirathi na atasimamiwa masomo tu"
Kauli hiyo iliyotolewa na baba mkuwa wa samira iliungwa mkono na ndungu wengine ingawa shangazi yake hakuridhishwa na maamuzi yale lakini hakuweza kutoa kauli yoyote ya kupinga kwani mfumo dume ulikuwa kazini. alipoonesha kutoridhishwa na maamuzi hayo alifunguliwa mlango wa kutokea huku akisindikizwa na makofi yaliyomwacha na alama mashavuni mwake.
Siku mbili baadae baba mkubwa wa samira alionekana akiwa kasimama nje ya jumba moja kukuuu kukuu akiwa kamshika mkono samira aliyekuwa na begi lake dogo na kumkabidhi samira huku akitoa maelezo ya kuwa ni samira ni mtoto yatima na alimwokota barabrani.
Baada ya kupokelea samira alianza kukaa hapo kwa maisha mapya huku akisahau kabisa kuwa ana familia tena zaidi ya wakati huu kuwa karibu na watoto wenzake.
***
Miaka mitatu ilipita bila shangazi kujua wapi samira yupo na wakati huo alikuwa amehamia mji mwingine na kila alipojaribu kumpigia kaka yake ili apate taarifa za samira aliambiwa kuwa yuko shule ya bweni na siku mmoja likizo watampeleka.
Shangazi yake samira yeye alijulikana kwa jina la Aunt Amina na alishakaa kwenye ndoa yake kwa muda wa miaka saba bila ya kubahatika kuwa na mtoto. Alibahatika kumpata mme ambaye hakuwa na fedha ila alikuwa na mapenzi ya dhati kiasi kwamba walikubaliana kuwa wasubiri kudra za mwenyezi Mungu ili muda ufike awape watoto.
Lakini ilikuwa imepita miaka mingi na ndugu walishaanza chokochoko ingawa mmewe na Aunt Amina yeye alibaki kuwa na msimamo na ni wakati huu ambapo waliamua kwenda kituo cha watoto yatima ili waweze kumchukua mtoto wampendaye na kumfanya mtoto wao.
Jumatatu moja asubuhi majira ya saa nne Aunt Amina na mmewe walionekana wakiwa kwenye ofisi moja ya kituo cha kulelea watoto yatima huku wakiangalia watoto mbalimbali.
Macho ya aunt amina yaligongana na macho ya Samira na kwa mshtuko wenye usiri ndani yake baada ya kumtambua samira ambaye yeye hakutambua kitu wakati huo, aunt amina alimvuta mmewe pembeni na alimnong'oneza kitu,
" Mpenzi wangu huyu mtoto nimempenda sana, naomba tumchague huyu awe mwanetu"
" haina shida kama umempenda mtoto huyu mie sina neno mpenzi wangu"
" asante kwa kunielewa" alijibu aunt amina huku akielekea ofisini kwa mkuu wakituo na kumwacha mmewe akielekea nje kuipokea simu iliyokuwa ikiita muda huo.
" samahani kaka, hivi jina sahihi la mtoto huyu anaitwa nani?"
" Kulingana na taarifa zake tulizopewa wakati akiletwa msamaria mwema jina lake aliandikishwa Janeth Simon Shikopa"
" ok nashukuru sana" aliongea aunt amina huku akipokea taarifa za samira ambaye katika kituo hicho cha kulelea watoto alitambulika kwa jina la Janeth.
Waliondoka pale na kujerea nyumbani ningawa muda wote huo akili ya aunt amina ilikuwa ikimfikiria janeth na kujiuliza je ni janeth kweli au ni samira? na kama ni samira iwaje wepo kituo cha watoto yatima badala ya kuwepo shule ya bweni? na je ni kwanini apelekwe pale? au kutakuwa na sababu nyuma ya hayo yote?
Walifika nyumbani na maisha yakaendelea huku janeth akiwa mchapakazi na mtoto aliye na bidii na heshima katika kila kazi aliyopewa na shuleni alionekana kujituma pia pamoja na udogo wake.
" mme wangu tumekaa na huyu janeth kwa zaidi ya miezi mitano sasa ila mimi kuna kitu nafikiri zaidi juu ya mtoto huyu"
" unafikiri nini mke wangu"
" huyu mtoto ni mtoto wa marehemu kaka yangu,. hata kama sikubahatika kuonana nae zaidi ya ile siku ya msiba wa kaka lakini naamini ni huyu tuu ingawa sijui kuna nini maana kaka mkubwa anadai yupo shule ya bweni na kila nikitaka amlete ananipa viswahili"
" mmmh kwani mtoto wa kaka yako marehemu alikuwa anaitwa nani?"
"Samira"
" sasa mbona huyu pale kituoni walituambia anaitwa janeth?"
" na mimi ndio nafikiri hapo kuna kitu, sasa mimi leo akirudi toka shuleni nataka nijifanye kumwita samira nione kama ana kumbukumbu"
" Aiseee kweli dunia matata sasa kwa nini kaka yenu afanye hivyo au kuna kitu kuhusiana na utajiri wake?"
" Uko sahihi nafikiri hivyo pia ila ngoja tuone mwisho wake"
Walimaliza kujadili na kila mmoja wao akawa busy na kazi zake mpaka ilipofika mida ya saa moja na nusu usiku wakiwa sebuleni wanaangalia luninga aliingia Janeth akiwa natokea masomo ya jioni na kuwakuta wakiwa pale.
" samira mbona umechelewa leo kurudi?"
" Mama umelijuaje hili jina? ni mama na baba yangu tuu walikuwa wananiita kabla hawajafa"
Bila hata kuongea neno aunt amina alinyanyuka na kwenda kumkumbatia Samira na kuanza kulia kwa uchungu jambo lililomfanya na mme wake nae atafute kuitambaa chake na kuufuta uso wake kushairia nae alishikwa na huzuni baada ya kumwona mkewe akiwa analia kwa hisia.
" ilikuaje ukawa pale samira?"
" mwalimu aliniambia nilipelekwa pale na baba mmoja aliyeniokota"
" maskini samira pole sana mwanangu, mimi shangazi yako kabisa ingawa nilikuja siku moja tu ya msiba wa baba yako na nikafukuzwa kwenye kikao na siku chache baadae nilihama kutoka mji niliokuwa ninakaaambao pia ulikuwa mbali na kwenu na kuja hapa na mjomba wako, tutaongea vizuri kesho haya jiandae ule chakula"
Usiku huo haukuwa na maneno ya ziada zaidi ya kila mmoja kuwahi kulala huku nyumba nzima ikiwa imezingirwa na furaha yenye maswali mengi ndani yake.
Simulizi hii itaendelea KESHO JIONI
Asante kwa Karibu Mbeya kuirudisha hadithi hii
Itangaze bure biashara yako kupitia http://karibumbeya.com/register/



Mwezi www.karibumbeya.com tunapenda kumpongeza Josepher wa GODRICH HEALTH CENTRE kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwa elimisha watembeleaji wa tovuti yetu juu ya masuala ya afya na ujasiriamali.
Unaweza kufuatilia post zake kupitiahttp://karibumbeya.com/author/josepher/
Nawe unawe unaweza kutoa elimu au kuitangaza biashara yako bure kwa kuifuata link http://karibumbeya.com/register/
CHUNUSI NA MADOA YATOKANAYO NA CHUNUSI AU KUUNGUA NA JUA Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hushambulia sehemu za usoni na kuharibu sura ya mwanadamu hasa wanaw...
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: