“'Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana”

12:27:00 Unknown 0 Comments



Leo hii tunakumbuka siku ambayo Hayati Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere alitutoka, kweli kila mtu ilimuuma na tunaendelea kuumia kwa namna tofauti sana.

Mimi kipindi hicho nilikuwa bado kijana sana lakini nimekuwa nikisoma na kusimuliwa mambo mengi mazuri ambayo baba wa taifa ailiyafanya na kuyapigania kwa uwezo wake wote kwa ajili ya Tanzania na watu wake.

Sio baba wa tafia tu, lakini pia tuna mifano hai ya babu zetu wengine kutoka nchi tofauti hapa barani Afrika, ambao nao walifanya na wanaendelea kufanya mambo makuu na ya kishujaa kwa manufaa ya jamii zao.

Mfano hai, rahisi na wa karibu ni wa rais wa zamani wa Afrika ya kusini Nelson Mandela ambaye bado yupo hai na tumeambiwa na kusoma mambo mengi ya kishujaa aliyoyafanya enzi za uongozi wake.

Ushujaa na ujasiri wao walioufanya kwa mapenzi ya nchi zao ndio sisi twapata faida leo na yale maumivu, mateso na hata jasho walilotoa kutukuombo leo ndio faida na furaha tosha tuliyonayo.

Enzi hizo ilikuwa ni ngumu kuzungumuza kwa lugha moja, mawasiliano yalitumia muda, usafiri na baadhi ya miundombinu ilikuwa sio ile ya kukupa urahisi mtu yoyote Yule, lakini bado wao walitumia fursa walizo kuwa nazo na leo hii watakumbukwa na vizazi vyote kwa ujasiri wao.

Ndugu, leo hii kuna fursa kibao ambazo ziko mbele yetu na pengine ni ujasiri na hata ule moyo wa kutokata tama ungehitajika ili uweze fikia malengo yako na hata baadae nawe kuwa mfano kwa jamii yako lakini bado tunakuwa wagumu na wengi twapiga kelele kuwa Maisha ni magumu.

Swali, ni je kama leo wewe usipochukua hatua ya kutambua fursa ulizonazo na kuzifanyia kipaumbele nani atafanya hivyo kwa ajili yako?

Wazo langu

Kila tunapoikumbuka siku hii ni vyema nasi tujiulize tunatumiaje uwezo wetu wa kufikiri na kutumia fursa zetu tulizo nazo katika kuyabadilisha Maisha yetu na jamii zetu ili nasi baadae tuje kukumbukwa na vizazi vyetu.

Nitanukuu maneno haya ya Baba wa Taifa“'Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana”

You Might Also Like

0 comments: