.HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI

02:25:00 Unknown 0 Comments

KUNA WIZI UMETOKEA BENKI KUU
•••••••••••••••­ •••••••••••••••­ •••••
JAMBAZI; "wote laleni chini pesa ni
za serikali na maisha ni ya kwenu",wote
wakalala chini
HII INAITWA DHANA YA USHAWISHI-kubad­ilisha
njia ya
kawaida ya kufikiria
•••••••••••••••­ •••••••••••••••­ •••••
Kuna dada kwa woga akawa
amelala chini kimitego,
JAMBAZI; "dada embu kuwa na adabu chukua
kanga jifunike hili ni
tukio la ujambazi na sio la
ubakaji. HUU UNAITWA WELEDI-zingatia
ulichofundishwa­ kufanya
•••••••••••••••­ •••••••••••••••
••••••••• Walipotoka kwenye wizi jambazi
mdogo ambaye ana shahada ya
uzamili ya biashara akamwambia
mwenzake,"tuzih­esabu hizi
fedha,yule mkubwa akamcheka
kwa dharau na kumjibu,"wewe mjinga sana
hizo hazina haja ya
kuhesabu saa mbili watatutangazia
kwenye taarifa ya habari tumeiba
kiasi gani. HUU UNAITWA UJUZI-Siku hizi ujuzi
ndio bora kuliko vyeti
•••••••••••••••­ •••••••••••••••­ •••••
Baada ya majambazi kuondoka
meneja akamwambia mhasibu wa
bank, " ujumlishie na zile milioni
80 tulizo iba sisi".HUKU KUNAITWA KUOGELEA
NA MKONDO WA MAJI- kushabiihana na
mazingira magumu kwa faida binafsi.
•••••••••••••••­ •••••••••••••••­ •••••
Mhasibu akafurahi na
kusema,"dah wizi ukitokea kila mwezi
itakuwa burudani sana.
HUKU KUNAITWA KUWA NA
MAWAZO CHANYA-Furaha ndio
kitu cha muhimu zaidi
•••••••••••••••­ •••••••••••••••­ •••••
Meneja kafurahi sana kwakuwa sasa matatizo
yake yametatuliwa
na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-
shikilia nafasi pale inapojitokeza
hata kama ni hatari kiasi gani
•••••••••••••••­ •••••••••••••••­ •••••
usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa
wizi mkubwa sana wa millioni 100 umetokea
leo benki kuu,Majambazi kuskia hivyo
wakaanza kuhesabu zila pesa lakini
wakajikuta na milioni 20 tu.Yule jambazi
mkubwa akashtuka
na kusema, "dah! yani meneja
kaiba mara nne zaidi yetu bila
kutumia msuli!! bora umeneja
kuliko ujambazi". HII INAITWA ELIMU- ishike
sana elimu ina nguvu kuliko dhahabu.

You Might Also Like

0 comments: