Hali ile ilinikosesha raha kabisa kabisa

23:15:00 Unknown 0 Comments

Kuna kijana mmoja kwa miaka kadhaa alikuwa akisumbuliwa sana na ndoto mbaya na za ajabu pamoja na kukosa kulala kwa furaha na amani.

Alitembea sana kwa waganga na hata watu mbalimbali ili aweze pata ile amani lakini nao wakashindwa kumsaidia.

Miezi chache iliyopita alisafiri kwenda kumtembelea kaka yake aishie jijini Dar, kijana yule baada ya kula na kuongea kidogo aliona awaage kwa kuwa alikuwa amechoka na alihitaji kupumzika.

Akiwa anainuka mtotomdogo wa nyumba ile mwenye miaka 2 akasema anko tusali kwanza ndipo ukalale, nae kwa aibu akakubali ingawa haikuwa jadi yake kusali iwe anataka kula, kulala, kuamka hata akiwa safarini pia.

Usiku ule hakupata ndoto ya aina yoyote ile mbaya kama zile za mwanzo.

Kuanzia hapo akawa mtu wa kusali kila mara na wakati wowote atakapo kufanya jambo.

Kama nawe unaamini uwezo wa sala katika kukupa faraja na ulinzi maishani mwako basi ulale na kuamka kesho ukiwa salama

You Might Also Like

0 comments: