Rafiki wa kweli huyu hapa

03:10:00 Unknown 0 Comments





Siku moja marafiki wawili waliamua kutembea porini katika matembezi yao ya jioni. Kwa kuwa walikuwa wana historia ya lile pori wakaahidiana kuwa lazima walindane na wawe na umoja kama chochote kingetokea.
Ghafla, wakaona kundi la dubu likija upande wao. mmoja wa wale marafiki akakimbia na kupanda mtui haraka. Rafiki mmoja yeye alishindwa kupanda mti kwa kuwa hakuwa anajua jinsi ya kupanda juu ya mti, hivyo akili ya haraka ikamtuma ajiangushe chini na kujifanya kafa wala asipumue kwa kuwa dubu huwa hawali viumbe waliokufa.
Dubu mmoja alipofika pale akawa akimnusa masikioni kuona kamani jamaa ni mzima au amekufa kisha akaondoka zake bila kufanya kitu akijua jamaa kafa. 
Yule rafiki aliyekuwa juu ya mti akashuka na kumuuliza mwenzie, "rafiki, nini dubu alikuwa akikufanya sikioni kwa muda wote huo?" Rafiki akajibu " alikuwa akiniambia usimwamini tena rafiki asiye mkweli"

Funzo: Rafiki wa kweli ni yule ambaye husimama upande wako kwa kila aina ya dhoruba

You Might Also Like

0 comments: