UNAFIKIRI KILICHOFATIA NI NINI?

23:51:00 Unknown 0 Comments

Jamaa mmoja aliwatembelea wakwe zake, mkoa fulani ambao unasifika kuwa na simba wengi. Ilipofika wakati wa kwenda kulala wakwe zake walimtahadharisha kuwa asitoke usiku kuna simba, wakaagana na jamaa akaelekea kulala chumbani, ambako alilala shemeji yake( mtoto wapata miaka 4)

ilipofika usiku wa manane jamaa alibanwa haja ndogo na huko nje simba wanaunguruma, alishikwa na woga na huku mkojo ukiendelea kumbana. basi jamaa akaamua kumtoa yule mtoto kitandani alipokuwa amelala nakumuamishia kitandani kwake, kisha akakojoa kwenye kitanda alichokuwa amelala dogo.

baada ya kumaliza kukojoa, jamaa alienda kumchukua mtoto ili amrudishe mahali pake, akakuta mtoto amesha kunya kitandani kwake.

UNAFIKIRI KILICHOFATIA NI NINI?

You Might Also Like

0 comments: