Nikahamia kwa baba ambaye alinikataza nisijihusishe na mapenzi au kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu wa aina yoyote ile bila kujua tayari nilikuwa mjamzito.
Nikiwa mdogo nilinyanyaswa kijinsia na kimapenzi na mjomba wangu pamoja na kupigwa sana na bibi yangu huku nikifanyishwa kazi nyingi.
Nilipigwa mpaka damu zilinitoka mgongoni na kuangukia nguo yangu ya kanisani na baada ya bibi kuona hivyo akaanza kunipiga tena tukielekea kanisani huku akiniuliza kwa nini nguo ilikuwa na damu.
Nilikula na kunywa maji kwa taabu nilitumia mikono yangu na bibi hakupenda kuniona hivyo akazidi kunichapa.
Kipindi hicho nilikuwa na umri wa miaka 6 na nilipofika miaka 9 nilihama kwa bibi na kwenda kuishi na mama.
Nikiwa na miaka hiyo 9 nikabakwa na mjomba wangu baada ya kubakwa damu zikiwa zinachuruzika magotini akanichukua na kunipeleka kuninunulia ice cream.
Na niliendelea kuibighudhiwa kimapenzi pamoja na kuendelea kubakwa kuanzia miaka 10 mpaka 14 kabla ya kupata mimba na mama kunifukuza.
Nikahamia kwa baba ambaye alinikataza nisijihusishe na mapenzi au kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu wa aina yoyote ile bila kujua tayari nilikuwa mjamzito.
Wiki mbili baada ya mtoto kuzaliwa alikufa.Ilikuwa huzuni kwangu na kwa baba pia ingawa kwangu niliona ni kama nafasi ya pili kwa mimi kuanza maisha mapya nikijipanga upya.
Maisha ya yule mtoto aliyekufa yalinipa uchungu wa kuona kuwa nahitaji kuyazika yote ya kale na changamoto za utoto hata kama nitakutana na mpya ila mtoto alinipa hamasa ya kujituma na kumtegemea Mungu.
Nafahamu ilivyo shida na ngumu kuishi na watu wasio kuthamini au hata kukujali maishani, lakini pia waweza kuutumia mwanya huo kama kichocheo cha mafanikio.
Watu wengi tunayaona maisha na changamoto zake kama ni kero kwetu na tunaonewa. Una kila sababu ya kusimama na kuzikabili changamoto zako.
Niliishi katika jamii ambayo mtoto alionekana na hakuthaminiwa na kamwe sikujua kama ndani yangu nilikuwa na nguvu ya kujiamini na kuja kufanya mambo makubwa kama haya.
Kila mtu ana hadithi tofauti na yenye kukuliza na kukuumiza kuliko hii ya Opra winfrey, lakini hadithi yake ilimfanya ajitambue na kufikia hatua aliyonayo sasa ya kuwa mwanamke tajiri zaidi duniani.
Kupitia hadithi hii tunajifunza kuwa katika maisha tunatakiwa kusonga mbele pamoja na changamoto mbalimbalu na mwisho tuje kuwa na mwisho mzuri.
Sala yangu kwako
Pamoja na mapito magumu nakuombea kwa mwenyezi Mungu kila changamoto uipitiayo sasa ije kugeuka na kuwa mafanikio yako kwa kadri utakavyo mtanguliza Mungu katika mapito yako huku ukijituma. Na utafanikiwa na kuja kuwa mfano kwa jamii yako...Amen
Comment AMEN kwa kubofya HAPA na kisha share kama unaamini uwepo wa MUNGU katika mapito yako


0 comments: