Facebook iliponifanya kuwa mtumwa wa ngono ughaibuni (kisha cha kweli na cha kusisimua)

16:55:00 Unknown 0 Comments

KISA CHA KUSISIMUA CHENYE UKWELI NDANI YAKE

Nilianza kutumia mtandao wa facebook mapema mwaka 2009.

Na kama vijana tulio wengi hapa facebook mimi nilikuwa na lengo kuu la kupata vimwana wa kuchati nao na kuangalia deal za kunitoa kimaisha.

Mapema mwaka 2010 nikanza urafiki na binti mmoja wa kizungu aitwaye Mirabel na kwa wakati huo alikuwa akiishi nchini Australia na alionyesha kuifahamu sana Tanzania.

Urafiki huo ulidumu kwa mwaka mmoja kabla ya 2011 kuanza kuwa wapenzi rasmi na kwa kuwa hatukuwahi kuonana zaidi ya mtandaoni na kwa kuwa mimi sikuwa na fedha za kutosha akaniambia nisiwe na wasi wasi atanitumia kila kitu na mimi nisafiri na kwenda huko tayari kwa kuwa pamoja.

Akaendelea kushughulikia documents na baaada ya kukamilika miezi michache baadae nikasafiri na kwenda mpaka Australia.

Nilipokelewa airport na kijana mmoja mwenye umri wa kuanzia miaka 37 na kuendelea hivi kwa mwonekano wake na akaniambia yeye ni kaka wa Mirabeli na kuwa mirabel yeye kaondoka kidogo atakuja.

Akanipeleka mpaka nyumba moja kubwa nzuri yenye mandhari ya kuvutia na kuniambia ni ya kwao na dada yake na kuwa dada yake atakuja hivyo niwe na subira na kunipa chumba changu na yeye kuondoka.

Kile chumba kilikuwa kimepambwa picha za binti mirabel ambaye kwa sasa ni mke wangu mtarajiwa na nilikuwa na hamu sana ya kumwona na nikaona masaa hayasogei.

Usiku yule kaka wa Mirabel akaja kunichukua na kunipeleka hotel na baada ya hapo tukapata vinywaji na kuniambia kuwa dada yake kapatwa na tatizo na hata weza rudi mapema itambidi akae kwa siku tatu ndio aje. Sikuwa na taabu nikasema poa kwani niliamini lazima aje tu.

Masaa yakasogea na hatimaye siku tatu ikafika lakini hakuja yule dada na nilipomuuliza akaniambia atakuja tu hivyo niwe mpole.

Siku ya pili akaja nikiwa nimelala na kuanza kunitomasa jambo lililonifanya niwe mkali na kumfukuza. Asubuhi nilipoamka akaniambia hakuna cha mirabel wala nini ila alinipenda na yeye anataka ndoa za jinsia moja na kaniona naweza kuwa mkewe.

Nilikataa na kugombana naye ingawa juhudi hazikufua dafu na akaniingilia kinyume na maumbile yangu na kuanza kunifanya mkewe.

Nikaja kugundua kuwa hiyo ndio tabia yake kwani kuna documens nilizibamba na emails kibao alizokuwa akitumiana na watu kibao akijifanya yeye mwanamke... Na pia alikuwa mwizi wa njia ya mtandao

Hali ile ilinikosesha raha na mbaya zaidi kila document yangu aliificha na sikuwa na fedha na ni mgeni maeneo yale na sijui wapi kwa kuanzia niweze kutoroka.

Ikapita miezi kadhaa kabla ya kufahamiana na kijana mmoja ambaye yeye ni baharia na baada ya kumsimulia akaniambia ataona ni jinsi gani anisaidie.

Mwezi mmoja baadae akaniambia kuna meli ya mizigo ambayo anaweza kuniombea msaada watanisaidia kwani walikuwa wakielekea Mombasa.

Siku ilipofika nikafanikiwa kumwibia yule haramu fedha na kukimbia na ile meli ikaanza safari.Kamwe siji kuikumbusa safari hiyo maana kwanza niliteseka vya kutosha nikifanyishwa kazi mle kwenye meli bila huruama.

Na wale mabaharia wa kigiriki walikuwa kila jioni wakiniingilia kinyume na maumbile na nakumbuka kuna siku ilibakia kidogo nijirushe majini kama sio kudakwa na yule kijana ambaye mle ndani hakuwa na sauti.

Nilipigwa mpaka nilitamani kufa na baada ya hapo huruma ikawaingia kwani nilianza kuumwa homa iliyoufanya mgongo wangu kuuma kulikosababishwa na kazi nyingi pamoja na kuingiliwa kinyume na maumbile.

Baada ya safari ya shida na mateso iliyochukua zaidi ya miezi kadhaa na hatimaye nikawasili Mombasa ambako napo kidogo mambo hayo yajirudie kama sio rafiki yangu mmoja niliyekutana naye nakunifanyia mpango wa kutoroka na baadae kupata usafiri wa kuja bongo.

Nilimshukuru Mungu na naendelea kumshukuru Mungu kwa kuniokoa na kurudi salama na nikaenda kwa daktari na kuniona sijaathirika na mpaka sasa ile tabia aliyonifanya yule bedui nimeiacha ni kijana mwenye familia ya mke na mtoto mmoja wenye furaha na amani.

Ndugu zanguni nimeamua kutuma ujumbe huu kupitia ukurasa huu nikitaka kuwaasa wale wanaowaona anawake facebook na kuwashobokea sio kila picha ya mwanamke ni mwanamke na wengine wanamalengo yao.

Sio tu unamwamini mtu mara moja na kumpa details zako na hata kukutana naye.. sikatai ya kuwa kuna marafiki wazuri bali natoa angalizo maana mimi yamenikuta kwa mtu niliyemwamini.

Pia hakuna mtu atakaye kutumia fedha na hata kukupeleka nje na kwenda kukuangalia tu akikufurahia, wengine wana mipango yao michafu ya kukudhalilisha.

Tujaribu kuwa waangalifu sana kwa mahusiano yetu ya hapa facebook.

Comment maoni yako juu ya mwenzetu huyu mtumiaji wa facebook kama wewe na kisha Share kutoa tahadhari kwa mwenzako.

You Might Also Like

0 comments: