Uroho uroho wa kuchukua namba za mabinti wa fesibuku wamtokea puani

10:46:00 Unknown 0 Comments


Njemba moja ambaye amejipatia umaarufu mkubwa hapa fesibuku hasa kwa tabia yake ya ku-add mabinti kwenye akaunti yake na kuwa na vijimaneno vya WOW you looks so sexy, Beib can i have your number. oooo my gosh ur killing me now, usiku wa kuamkia leo ilimbidi akimbie umbali wa zaidi ya kilomita 10 akiwa na nguo alizo zaliwa nazo  bila kupumzika na mwishowe kukumbuka kuwa hata viatu alivisahau kunako hotel.

Story ilianza baada ya jamaa kupata namba toka kwa dada mmoja humu fesibuku na jamaa akaanza kutumia uhodari wake wa kutunga maneno matatu matamu na kumrushia binti huyo ambaye alikuwa akisisitiza jamaa asipige simu kwani muda mwingi yupo na mmewe.

Jamaa akafanikiwa kumshawishi kigoli huyo ambaye kiukweli inaonekana anajua sana matumizi ya photoshop na baada ya muda jamaa akakubaliana wakutane mafichoni hotel ili waweze kuikosea amri ya sita kwa raha zao.

Kwa mbwembwe zote akafika kunako hoteli na kwenda moja kwa moja kwa rumu, cha ajabu baada ya sekunde kadhaa kulisikika sauti za aina tofauti zilizofuatiwa na mbio kali kutoka kwa njemba kiasi kuwafanya baadhi ya mapaparazi kushindwa kulipata vizuri tukio mpaka pale jitu la miraba kadhaa ambalo inasemekana lilishawahi kuwa bondia kwa miaka kadhaa kutoka chumbani na kusema "wewe si kidume unaependa tembea na kila mwanamke ambaye hujui anamilikiwa na nani simama sasa"

Mpaka asubuhi hii simu ya njemba imezimwa na kila nilivyojaribu kumfuatilia hapa fesibuku kwenye akaunti yake sikukuta posti mpya zaidi ya ile aliyoitupia dakika chache baada ya tukio posti ambayo yasomekahivi " Usimwamini mtu yoyote hapa fesibuku- damn i hate fesibuku"

Tuungane kumwombea njemba maana hatujui nini kilitaka kumtokea na kwa sasa atakuwa wapi 

You Might Also Like

0 comments: