Kama nawe uko kama hawa jamaa kukumbuka MUNGU anakuona

10:46:00 Unknown 0 Comments



1. Unanunua gazeti la udaku halafu unaliweka katikati ya gazeti la Mwananchi- Mungu anakuona
2. Unajenga nyumba kisha unazungushia ukuta wenye geti kubwa, kumbe ndani hakuna nafasi hata ya kupaki baiskeli- Mungu anakuona
3. Home choo cha shimo, unadanganya eti unatafuta fundi bomba flash imeharibika -Mungu anakuona
4. Umekula ugar na bamia halaf unakuja maskan na kijiti mdomon - Mungu anakuona 
5. Unasoma karibu nikutume secondary school bt fb waandika unasoma feza- Mungu anakuona
6. Kwa wale wanaoandika txt, 'Nakumiss' halafu kuituma kwa wapenzi 20..........MUNGU ANAWAONA
7. LUKU imekata kwenu umekaa nje unatext watu,'Niko nje napata upepo mwanana'.......MUNGU ANAWAONA
8. Huna kazi, mpenzi wako mtumishi wa serikali mshahara laki 3 kwa mwezi, Birthday yako unatumia milioni mbili......MUNGU ANAKUONA
9. We ni kiserengeti boy una mupenzi wa miaka 50, unamtext 'Njoo baby', we huyo baby au nyanya yako?.....MUNGU ANAKUONA
10. Unapiga picha sebule ya boss wako unaiweka FB na kukoment Home Sweet Home........MUNGU ANAKUONA

You Might Also Like

0 comments: