Kipande cha tofali chazua mambo

06:47:00 Unknown 0 Comments

Miaka 10 iliyopita kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa kampuni mmoja mashuhuri alikuwa akisafiri kwa gari kutoka mji mmoja kwenda mwingine.

Gari lilikuwa spidi sana na wakati huo alikuwa alikuwa akiwangalia watoto waliokuwa wakicheza na akapunguza mwende kwani alihisi kuna kitu amekiona kabala ya kushtushwa na kipade cha tofali kilichorushwa na kuupiga mlango wa gari lake jipya aina ya Bentley ambalo lilikuwqa na miezi miwili tangu anunue..

Akasimama haraka na kuliangalia gari lake nakuona limechubuka rangi na kwa hasira akamwona mtoto aliyelirusha lile tofali na sura ya ukalia akamsogelea na kumwambia unajua ulichokifanya kitakugharimu kiasi gani??

Yule mtoto akawa akilia na kumwomba samahani yule kijana huku akisema nilirusha tofali lile ili nipate msaada kwani nimekaa kwa muda na kila nikiomba msaada watu kusimama hakuna aliyefanya hivyo.

Huku machozi yakimtoka akamwonyesha yule kijana nyuma ya gari moja lililopaki na kuona kuna kijana mmoja mlemavu kaanguka kutoka katika kiti chake cha kutembelea baada ya kiti kuteleza na kisha kuanguka na mdogo akashindwa kumrudisha. 

Yule kijana huku akijikaza kujizuia hasira na kuvuta pumzi nzito akamsaidia yule mlemavu kurudi kwenye kiti na akatoka kitambaa chake na kujifuta vumbi huku akangalia yule mdogo akamsukuma kaka yake katika kile kiti na kutokomea..

Akalifuata gari lake na kuondoka kuendelea na safari na hakulitengeneza lile eneo ambako kilr kipande cha tofali kilipiga ili iwe kama sehemu ya kumkumbusha kuwa hatakiwi kuharaka na maisha au busy na maisha mpaka mtu amrushie kipande cha tofali ili kipata masaada wake.

Kuna vipande vingi vya tofali katika maisha yetu, vingine vikubwa na vingine vidogo ambavyo kila siku tukutana navyo bila kujua au kwa kujua na kupuuzia.

Kamwe usiwe busy na maisha na kuja kukumbuka kuwa kuna nyakati nyingi za furaha na faraja uliziacha njiani au hata kupoteza watu muhimu kwa kuwa wao hawakukurushia tofali ili kukukumbusha kuwa uwepo wako kwao unahitajika.

Mungu atujalie wepesi wa mapito yetu na busara tele




 

You Might Also Like

0 comments: