Kisa kilichoombwa kurudiwa mara nyingi na marafiki

05:29:00 Unknown 0 Comments

Tulifunga ndoa yetu kwa mbwembwe sana na binti Maria miaka 3 iliyopita na kila siku alisisitiza akisema, "Mtafya wewe ndie daktari wa moyo wangu"

kwa upendo tulioonyeshana, mahaba ya dhati na uaminifu baina yetu niliamini kila wakati kuwa nimempata mke mwenye hadhi ya kupelekwa KUTUKUYU KUSAUZI tena sio nusu.

Nilipenda sana kutoka kazini na kurudi nyumbani kula chakula cha mchana kisha kuendelea na majukumu ya kiofisi kwa kuwa tulikaa jirani na sehemu ya kazi.

Jambo hilo pia lilimfurahisha mwenzangu kwani yeye hakuwa na kazi hivyo nilijaribu kumpa kampani kwa kula naye mida ya mchana na usiku na asubuhi kama nikiwa ofu kwenda kazini ili kumtoa upweke pia.

Miezi michache baadae nikaanza kupata tetesi kuwa mimi nikirudi ofisini mara baada ya chakula cha mchana naye huchukua chakula na kuingia nacho kwenye geto la masela ambako ana jamaa yake mtaa wa pili toka kwetu.

Habari zile ziliniuma sana na ikanibidi nianze kufuatilia na kuja kugundua kuwa ni kweli huwa anapeleka chakula na kuwa jamaa kahitimu chuo ila hana kazi anakaa magetoni na ndio walikuwa wakianza kudeti na hawajaibanjua amri ya sita bado.

Sikutaka kumuuliza ila nikaaamua kutumia busara za kizushi ili kuokoa ndoa yangu changa isije paranguka kwani sipendi kuachana na huwezi jua naweza kuja kukutana na shetani zaidi nikijua ni malaika na mimi nampenda sana mke wangu.

Siku moja nikawahi kurudi home kula Kama kawaida na wakati nasubiri chakula nikaamua kujilaza kitandani,wakati huo yeye kaenda duka jirani kununua baadhi ya mahitaji.

Ile navua viatu niweke uvunguni nikaona kama nasukuma kitu kucheki kumbe ni hotpot ya kuhifadhia chakula

Nikaifunua ile hotpot na kuona kuna pilau na nyama kaziweka pale na mie kwa akili ya haraka nikaifungua nikatoa chakula kidogo ili kuachia nafasi na kuutumia mwanya huo kuachia KIMBA la maana na kuifunga ile hotpot vizuri isitoe harufu kisha nikairudisha na kuendelea kulala.

Baada ya wife kuja tukala kisha nikajifanya kuondoka na kujificha jirani na kuona wife akitoka na mfuko nikajua kaichukua pilau yake na kutokomea vichochoroni na mie nikarudi zangu home.

Nusu saa baadae mke wangu akaingia akiwa kavimba uso na pia damu zamtoka huku baadhi ya nguo zikiwa zimechafuka na kuchanika pia akinuka ushuzi jambo lililoashiria kuwa kapewa kipigo hevi na jamaa yake kwa kupeleka KIMBA badala ya msosi.

Nipomuuliza alidai amevamiwa na vibaka alitaka kwenda sokoni na wamempiga, mwagia maji yanukayo kama mavi na kumnyang'anya fedha tasilimu.

Mpaka leo hajaniambia ukweli ila nimefuatilia na kugundua waliachana na yule jamaa tangu siku ile na hana mtu tena zaidi yangu.

Hofu yangu ni je nimwambie kuwa nilifanya vile au nitulie au na yeye atakuwa anahisi mimi kuwa niliitegesha ile kimba?

You Might Also Like

0 comments: