"SOMA NA SHARE NA KILA RAFIKI UNAYEMJALI"

05:09:00 Unknown 0 Comments

1. Kamwe usitegemee utajiri wa wazazi au ndugu wako huwezi jua nani atakauja kesho na kuupokonya utajiri huo.

Jifunze kufanya vitu wewe mwenyewe na kuyafurahia mafanikio yako huku ukijifunza kwa kila mapito yako.

2. Mungu kampa kila mtu kipaji jitume huku ukiomba akuonyeshe kipaji chako na fanya kazi kwa kujituma kufurahia kipaji hicho.

3. Usikae chini na ku-tweet, kupost Facebook bure wakati wenzako wanatumia muda huo kutumia vipaji vyao kutengeneza fedha huku wewe ukiendelea kuwashabikia. Hebu fikiria mara moja na kuanza kuona ni jinsi gani nawe unaweza kupata fedha kupi
tia kipaji chako.

4. Ni vyema kukubali kazi za wenzako na kuwapa sifa zao, ila jitahidi usiwe mwepesi wa kutumia muda mwingi katika mabishano ya kazi za watu jaribu kufikiri ni lini nawe watu watakaa na kujadili mambo mazuri kuhusu wewe..... Tumia muda mwingi kujibidiisha na kuyabadili maisha yako.

5. Usijione wewe ni bonge la mjanja kwa kulala na wanawake wengi, kumbuka wengine ndio wamekufanya uwe na maisha ya shida hivyo kwa kuwa wanakuja na mikosi maishani mwako. Tafakari na chukua hatua.

6. Jifunze kuwa jirani na mkeo au mpenzi wako wa kike na kumshirikisha katika kazi zako ili ufanikiwr zaidi.....kumbuka wanasema, " bila mwanamke mwanaume hawezi kuwa na mafanikio makubwa"

7. Jifunze kutatua matatizo yako kwani maisha ndio yanavyotaka... Usiwe mtu wa kukopi na kuishi kama wengine jifunze kuchukua mambo na kuyatengeneza yaendane na mtazamo wako ili kufanikiwa.

8. Acha kunywa pombe na sigara kupindukia kwani ni hatari kwa afya na maendeleo yako.... Jitahidi kunywa na kuvuta kwa mipaka na ukiweza acha kabisa.

9. Jifunze kuwa na moyo wa huruma kwa kuwasaidia wenye uhitaji kwani nao watatumia mioyo yao kukubariki nawe utazidi pata mafanikio.

10. Fikiri mambo yasiyowezekana katika maisha yako na jitahidi kuyaweka yawezekane.Hata matajiri na watu wenye heshima kubwa duniani walianza hivyo.

11. Muhimu kuliko yote ni kumtegemea MUNGU na kumshirikisha kwa kila jambo katika kufanikiwa kwako

You Might Also Like

0 comments: