SABABU 7 KWANINI HUTAKIWI KUFANYAMAPENZI KABLA YA NDOA ?, HIKI NDICHOKINACHOKATAZWA.

09:38:00 Unknown 0 Comments

SABABU YA 1:IMEKATAZWA NA MUNGU
Sababu ya Kwanza kwanini hatutakiwi kufanya
Mapenzi kabla ya ndoa ni kwa sababu MUNGU
HAPENDI..Amekataa...Na amekataa sio kwamba
hajui Sex ni Tamu,....Anajua utamu woteee
unaousikia ukifanya mapenzi...anajua raha
unayopata ukiwa unacheza kile kiduku pale bed
kwa mbwembwe...Anajua zile hisia unazofeel na
nini kinatokea ukifanya,ANAJUA...
yeye ndo ameziumba zile hisia,USIMFUNDISHE
MUNGU KAZI YA KUUMBA! Alikuumba akijua una
Hormone ambazo zitakusumbua lakini vilevile
amekupa uwezo wa kuzishinda...Mungu hawezi
kuweka jaribu ambalo halina Mlango,kama
alisema usifanye basi anajua uwezo wa
kutofanya upo !.
Tutabisha weeee,ooh haiwezekani,kuna watu
hawafanyi na wapo,wanapumua kama
wewe,wanamtii Mungu na wanaishi..hawafi,na
wanakuja wanaoa na mambo wanakula kama
kawa...Zile stori usipofanya sijui ufutio
unapotea,mara hivi,ni Plan za shetani tu kama
alivyomdanganya Eva akajaa kimiani,anakujaza
na wewe uamini ili upotee.USIKUBALI
SABABU YA 2:UTAMU WA HONEYMOON
KWISHNEY
Utakapooa, utaenda Honeymoon...Nia ya
honeymoon ni wewe kupewa fursa ya kutoa
gundi kwa mara ya kwanza...Kumbe gundi
umeacha Machimachi Guest House miaka mia8
nyuma
UNAENDA HONEYMOON KUFANYA NINI??
KUMDANGANYA NANI??
Hizo hela za Kamati ya Maandalizi watu
wanakuandalia kwenda Honeymoon wakati
Ramani nzima ya huyo mkeo na mmeo USED
unaijua hata ukifumba macho.KATAA HIYO!
SABABU YA 3: UTAKUWA NA AFYA KIROHO
Tunaishi kwa ajili ya Mungu...tuko hai kwa
sababu Mungu ametuacha na kutupa nafasi ya
kurekebisha maisha...Ukifa leo utakwenda wapi?
Umewahi kujiuliza??
Hauko hai kwa sababu wewe ni mwema sana
mbele za Mungu...As long as uko hai inabidi
uishi vile ambavyo Mungu anataka uishi...
MAISHA SAFI MBELE ZAKE!
Na ni ukweli usiopingika kwamba dhambi hii ya
NGONO/UTAMU/UZINZI ndio namba 1 katika
kuharibu maisha ya kiroho ya Watu...Hii dhambi
ndo Weapon namba 1 ambayo Ibilisi anaitumia
kumaliza watu.Laiti hii isingekuwa dhambi basi
watu wengi sana wangeingia Mbinguni,Wengi
sana.
Lakini hali ni mbaya sana...
Naweza kuthubutu kusema Afya yako ya Kiroho
inategemeana na ushiriki wako kwenye Ngono
au La.ukishinda hii,siamini kuna dhambi itakuwa
ngumu kwako kushinda,Jaribu uone!
Unaikosa Mbingu hivihivi kisa pale
katikati....WAZA UPYA!Tangu uanze kuifanya hiyo
kiu imeisha???Mbona unafanya na unafanya na
kufanya haiishi,uskiacha utakufa??Its not late to
start over,na uzuri wa Mungu ukitubu,anafuta
zoteeee za nyuma unakuwa mpya.You can start
afresh LEO!
SABABU YA 4:NI NZURI KWA AFYA YA KIMWILI
Hapa napo imekuwa mgogoro.mwanzoni watu
walisema aaaah ntakaaje na Sweetie wangu bila
ufanya,wakahalalisha...wamefanya weeeee
wamechokana...wakaanza kuiba nje,na wapenzi
wengine,na kwa sababu umekuwa sugu huoni
tabu kuongeza listi...Ishu inakuja Je, hiyo listi
yako iko salama???
Watu wengi wamepata pancha hapo
katikati,wamefikia muda wanataka kutulia na
kufunga ndoa kuanzisha familia...LOH!AFYA
MGOGORO!Siku hizi magonjwa ni mengi
sana,acha tu Ngoma inayozingua kila kona,kuna
magonjwa ya Zinaa ambayo unaweza ukaletewa
na bila kuyatibu vizuri ukaharibu vizazi ile
mbaya.....
Kuna ishu za mimba,maana mechi siku hizi
pekupeku tu...ETI MNAAMINIANA,peku pekua
mara kitu kimejaa...wote ndo mnagundua
hamko tayari kwa mtoto!Upuuzi mwingine
huo...Mko tayari kukata kiuno ila result za kiuno
hutaki...Utafanyaje mtihani halafu useme hutaki
majibu?.
utajuaje umefaulu au kufeli??Mapenzi bwana!
Mwanamke wa watu analazimika kutoa mimba
maskini,mwisho wa siku mkibahatika kuoana
hampati mtoto,HALFU UTASEMA WHY ME
LORD???KWELI???Au mtoto wa kike anaolewa na
mtu mwingine,tayari ushamsababishia kimeo
kwenye ndoa yake,na haya yako kila kona wala
sio mapya.WAZA UPYA!
SABABU YA 5:LINDA HISIA ZAKO
Unampenda mtu unafanya nae
Mapenzi...mnaachana,unapanga misururu watu
wengi kama msururu wa wateja wa NMB
kwenye ATM...Wote hawa unatumia moyo
huohuo,hisia hiyohiyo,wote
umewaonja,wamekupa different tastes,kama
mia7 hivi....wote wamekutenda,Hisia zako
zinakuwa na rangi kibaooooo,hata hukumbuki
moja kati ya hizo ipi sahihi.
Nakutana na watu wanasema hawawezi
kupenda tena,kia wametendwa....Sio
hivyo...Sehemu ya hisia ishatiwa shoti,kila mtu
kaja na bisibisi yake anachomeka tu,size 17
twendeeee size 44 twendeeee,haueleweki hisia
zako zimefikia size ngapi,maana kuna waliozi-
under size,na wengine wameku-
oversize...Umeshakuwa emotionally unhealthy....
Kwanini usitulie uje utumie hisia zako kiusahihi
na mtu sahihi???kwanza hawa unaosex nao
wengi hata wazo la kuao hamna,wanakutumia tu
bureee bureeee,ukimwambia tu twende home
nikutambulishe anajitetea na maneno lukuki
kama konda wa Mazese-Mburahati,ndo utajua
utatumiwa tu kama condom,kisha kitanda chako
jalalani!
SABABU YA 6: UVUMILIVU NI TESTI NZURI YA
UPENDO WA KWELI
Hapa hata sina haja ya maelezo mengi...Mtu
mvumilivu huonyesha nia ya dhati na upendo
wa kweli..Ila mtu anayekurupuka tu huyooo
ndani ya Shuka,utajua tu penzi lake ni la ki-
shuka shuka zaidi.
SABABU YA 7: BARAKA ZA MUNGU MLIYEMTII
NA UTULIVU WA NDOA
Ukimtii Mungu huwa anatoa baraka zake...Na
kinyume chake ni dhahiri...
Wle wanaomuamini Mungu na kufanikiwa kufikia
hapa,maisha yao yanakuwaga tofauti kabisa na
wale walioishi maisha ya kibiriti-Ngoma Style.
Watu mmetoka tangu urafiki mnaibatua amri ya
6 bila huruma....Sasa mnafika kwenye ndoa
mmechokana,Ladha yote imakwisha,,Mke hana
jipya la kukupa...Hakuna machejo ya Mme
usiyoyajua....NO EXCITEMENT.
Sishangai kuona Mwanaume ameoa
anacheat...Hamna jipya,Mke anabakia tu kuwa
Kiwanda cha kufyatua Watoto lakini INTIMACY YA
NDOA HAKUNA. Anaamua kujaribu ladha zingine!
Na effect za Mwanaume asiye na Intimacy na
mkewe zitaonekana hata kwa Mkewe in due
time...Hatampa haki yake kadri inavyopaswa,na
mwishowe mkewe atachoka kulishwa
Makombo,anayoyajua kwa Nusu Karne huko
nyuma...
Kifuatacho hapo ni wote kugeuka
CHEATERS...Mke anapiga show za nje kwa
wizi...Mme nae anakamua mechi za Mchangani
nje kwa kujiiba...Wote hawa wanajaribu kupasha
misuli nje maana ndani Gym imeishiwa
vifaa...Wanajifanya wanapasha moto Kiporo
kilichochacha...Kamwe hiyo ndoa itakuwa ngumu
sana kusimama tests of Time!
ARGUMENTS
Wengi wata-argue kwamba Maadili
yanachangia.NAKUBALI,Siku hizi ni ngumu sana
kumuamini Mpenzi kwamba atavumilia,ndio
maana Wanawake wameamua kujitoa Sadaka
kutoa tunda kama njia ya kuwin penzi la
wanaume...UONGO!Penzi la Mwanaume
halishikwi kwa kumpa Tunda...Kama
anakupenda WEWE atakaa,kama alipenda
TUNDA atakwenda...Simple Rule....
Mwanaume anapaswa akupende WEWE kwanza
na Sio ulichonacho Wewe...Afterall kama ana
ana nia na hicho kitu,si atakimilikisha kuwa
chake Milele na milele??sasa anakiwahi cha
nini??kuku wa Kwako ya nini Manati??
Na wanaume pia,wanalalamika wanawake
hawaaminiki,wana roho ndogo...Wewe
unamtunza hupigi show unadhani kwamba
anakutunzia unashangaa anakuja bwege flani
anakula mali yako kiulaini,Roho inauma,so bora
upige show ili hata ukiporwa,ah fresh mlinganyo
umekaa poa.
Maadili yanachangia lakini na Ibilisi kwa
kulitambua hilo,ameinvest hapohapo kwenye
LOST FAITH ya Maadili,na anawachapa watu bila
huruma.
Mimi nimemaliza hapa..Ukiamua kunisikiliza na
kuamini Mungu na akubariki,ila nikiwa kama
Jogoo anawahi kuamka lakini hafungui mlango
haya..

You Might Also Like

0 comments: