Kama hutaweza kujikubali basi tegemea kuwa kama binti huyu mpuuzi

20:22:00 Unknown 0 Comments


Selina baada ya kukaa zaidi ya miaka kadhaa bila kuolewa huku mpaka mdogo wake wa mwisho akiwa akolewa, dada alikata tamaa na kuamua kuendelea kuishi na mam yake kwani alihisi kama yeye hana bahati.

Selina alibarikiwa uzuri asilia na alijipenda sana ingawa sasa hakuna na jinsi zaidi ya kuachana na ndoto za kuolewa na kuwa busy na majukumu yake akimsaidia mama yake pale nyumbani.

Miezi michache baadae akiwa katika bustani moja amejipumszisha na anasoma kitabu chake mara alikakutana na mzungu mmoja ambaye naye alikuwa mpenzi wa eneo lile tulivu.

Wakawa marafiki na baada ya muda urafiki ule ukakua na baadae mzungu akaonyesha nia za kuifahamu familia yake na baada ya kuonana mama na kuzungumza naye yule mzungu akakubaliwa ombi la kuoana na selina.

Mzungu alijaribu kueleza jinsi alivyompenda selina na kusema ataomba aende kwao na akirudi watafunga harusi yao na kisha kuanza kuishi maisha ya pamoja kama mtu na mmewe.

Selina na mama walifurahi na baada ya mzungu kwenda ulaya akawasimulia ndugu kuwa kapata binti wa kitanzania mzuri sana na ana rangi asili ya mtanzania na wala hatumii mikorogo.

Wakati mzungu akiwa huko huku nyuma selina akaona ili apendwe zaidi na mzungu basi ngoja ajichubue na aifanye mambo ya karolaiti na kuwa mrembo zaidi hivyo akabadilika kutoka binti mweusi na kuwa mzungu nusu.

Siku mzungu anarudi akafika pale nyumbani na kuonana na selina bila kujua akamuuliza nimemkuta selina? kama yupo naomba niitie. Selina akasema ni mimi

mzungu akamuuliza kimetoka nini mpaka ukabadilika??? Mimi nilikupenda kwa jinsi ulivyokuwa na sio kwa hivi ulivyo... Ndoa ikaishia hapo hapo.

Wengi tumekuwa tukipoteza baraka kwa kuongeza uongo au tabaia zisizo zetu ili watu watupende zaidi au kuongeza uaminifu na mwishowe tukajikuta tumebaki bila kuwa na baraka hizo na kushuhudia zikiangukia kwa wenye kujitambua

Nakuombea pamoja na matatizo na misukosuko ya maisha kamwe usipoteze bahati kwa kufanya kitu kitakochokupotezea baraka katika maisha yako


You Might Also Like

0 comments: