Kila jaribu huja na baraka zake

06:27:00 Unknown 0 Comments

Loyce alifiwa na baba na mama yake katika ajali mbaya na ya kusikitisha iliyotokea mkoa mmoja hapa kusini mwa tanzania akiwa kidato cha tatu.
Baba aliumwa kwa muda mrefu huku mama akitumia akiba yote tena akihangaika huku na kule kuuza baadhi ya mali zao na hata kukopa fedha za kuokoa uhai wa baba na hata mauti ilipomkuta baba yao walibaki wakiwa hawana tena mali wala akiba ya kuendesha maisha yao..
Maisha yalizidi kuwa magumu na huku mama akizidi kudhohofu mwili kabla naye kuja kugundulika ya kuwa ana saratani ya kizazi ambayo alipigana nayo kwa muda mchache na akafa huku akimwacha loyce akiwa katika dunia isiyo na msaada.
Loyce aliomboleza huku akijaribu kuhusisha marafiki ambao wao uwezo wao uliishia pale alipohitimu kidato cha nne na matokeo yake yakawa sio mabaya sana ingawa akawa hana tena uwezo wa kwenda chuo au kuendelea na kidato cha tano na cha sita.
Moyoni mwake alilipinga sana wazo la kuolewa kama njia ya kutatua maisha yake hata alipofuatwa na kila aina ya wanaume kwani alijua waliufuata uzuri wake na mwisho wake wangemtelekeza hivyo akawa akijishughulisha kwa kulima na kuuza mboga mboga.
Mwaka mmoja baadae aliliona tangazo kutoka katika shule moja ya wasichana ambalo lilionyesha kuwa kuna mradi wa kuwasaidia mabinti wenye matatizo walioshindwa kwenda kidato cha tano na cha sita.
Loyce akaomba na kufanikiwa kupata ambako akasoma na mtihani wa kidato cha tano kwenda cha sita alifaulu na kuongoza kwa wasichana na mama mmoja raia wa kigeni kutoka Denmark aliyeitembelea ile shule akamwambia mwalimu mkuu kuwa atampa ofa ya kumsomesha loyce masomo ya juu kwa kiwango chochote hivyo akihitimu ajulishwe.
Baada ya kuhitimu mwalimu mkuu akafanya hila na kupeleka taarifa kuwa kwa bahati mbaya loyce aligundulika na mimba na hakuweza kumaliza masomo yake na hivyo kaolewa hivyo mama akatoa ufadhili huo kwa binti wa mwalimu huyo huku akiumia juu ya loyce.
Loyce alifaulu na kufanya vyema masomo yake na kisha kwenda ualimu na baadae akapangwa kwenda kufundisha shule moja iliyopo kijijini. Kufika huko baada ya mwaka akapata ufadhili wa kwenda kusoma nje ya nchi na kuhitimu masters yake.
Upande wa pili yule mtoto wa mwalimu mkuu hakufanikiwa kusoma kwani huko alikoenda yule mama hufanya biashaya ya kuuza watu kwenda kuwa watumishi katika majumba ya watu huko bila ujira. Binti yule kwa bahati alifanikiwa kurudi na hivi sasa ndio anaanza mwaka wa kwanza chuoni.
Rafiki unayesoma hili, kumbuka kuwa katika kila hila kuna baraka mbele zake na ni mpango wa Mungu kukuepusha na mambo makuu kama dada yetu loyce alivyoepushwa na sasa na mwanamke mwenye mafanikio na anasaidia wengi na kuwafanya wengi wahamasike.
Rafiki Mungu akujalie na kukufungulia milango ya mafanikio katika kila jaribu unalolipitia na ukumbuke kuwasaidia wanao hitaji msaada wako.

You Might Also Like

0 comments: