Nilijua tu lazima unifuate, Asante rafiki na kwaheri…

11:32:00 Unknown 0 Comments



Katika uwanja wa vita, askari Fuledi alijiandaa vyema kwenda kumrudisha rafiki yake aliyekuwa kaumizwa vibaya sana kwa risasi na aliyekuwa kaanguka umbali kidogo kutoka walipo.
Captian akamwambia Fuledi,

“Huna hata haja ya kwenda kumchukua kwana lazima afe tu hata kabla ya matibabu kwani kaumua vibaya”.
Lakini Fuledi aliendelea kwenda kumfuata rafiki yake na Captain alipofika kwa Fuledi akaona yule askari akiwa keshakufa.
 Captain akamwambia Fuledi
“Nilikuambia lazima atakufa tu”.
Fuledi akamwambia Captain kwa macho ya ushujaa:
“Hapana Mkuu, Limekuwa jambo la faraja kwangu….....Kwani nilipo mkaribia, rafiki aliponiona akatabasamu na kusema maneno yake ya mwisho kabla ya kukata roho:
“Nilijua tu lazima unifuate, Asante rafiki yangu wa kweli na kwaheri……"
——————————————–
Funzo
Ukipata rafiki anayekujali, kukupenda, kukuthamini, na kukuheshimu kamwe usimwache aende zake kwani maumivu yake huwa hayaponi kamwe.
Ni ushujaa kuwa na wale tunaowajali na kuwapigania mpaka tone la mwisho

You Might Also Like

0 comments: