HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 22

16:03:00 Unknown 0 Comments

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Photo: HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Season 22

ILIPOISHIA JANA

Ile amemaliza tuu alisikia sauti, " Arooo Umemariza haya nyanyuka juu", ile kugeuka alikutana na gwanda za jeshi kuashiria alikuwa eneo la jeshi na kilichofuata pale ilikuwa adhabu ya  kupiga deki kwenye bwalo la jeshi.

Alipokuja kuachiwa ilikuwa ni mida ya saa sita kasoro dakika tano za usiku huku akiwa kachoka chakali na hajui nini afanye. Wakati anatembea kwa mwendo wa haraka  akitoka eneo lile  mara simu iliita .............................

ENDELEA

Alipokuja kuachiwa ilikuwa ni mida ya saa sita kasoro dakika tano za usiku huku akiwa kachoka chakali na hajui nini afanye. Wakati anatembea kwa mwendo wa haraka  akitoka eneo lile la jeshi mara simu iliita.

Kwa hofu ya kuipokea simu eneo lile ikambidi aizime na kuongeza mwendo wa kutoka eneo lile na hatimaye akaishika barabara kuu na kuendelea kutembea kwa mwendo wa haraka  mpaka alipoanza kuyaona makazi ya watu.

Akapita uchochoro mmoja uliomfanya atokee mbele ya bar moja na upenuni mwa ukuta wa bar hiyo akakutana binti mmoja aliyekuwa akilia kwa sauti ya chini chini kuashiria alikuwa na tatizo likimsumbua usiku huo.

Kwa akili ya haraka bibi gusa unate akaona hii ndio fursa ya kupata fedha ya kwenda kulipa deni kwa chamdoli, akaanza kumuuliza yule binti kwa sauti yenye kuashiria alikuwa ni msaada kwake.

"Mjukuu wangu pole sana, hebu nyamaza na nieleze kitu gani kinakusibu usiku huu wa manane?"

" Bibi acha tu hapa nilipo natamani kufa maana nimetumia gharama zangu kubwa sana kumfanya huyu mwanaume ajue nampenda lakini huwezi amini nimefika hapa na... "

Hata kabla ya kumaliza bibi gusa unate alimdakia na kuanza kuongea lugha isiyofahamika kama vile alikuwa akiwasiliana na mizimu na kisha akasema "Mjukuu, nilitaka kupita njia nyingine na ghfla mizimu yangu ya TIKISA MDODO ikaniambia nije hapa kuna mtu ana matatizo eneo hili, kumbe ni wewe mjukuu?

Binti kwa mshangao akajibu haraka "Ndio bibi!"  

Wakati huo bibi akachukua nafasi  hii na kumvuta pembeni na kuanza kumwambia matatizo yake. 

Kwanza kabisa bibi alimsifia kwa kusema, " Kwanza mizimu yangu imeniambia kuwa wewe una roho nzuri sana na imesema inakuzawadia nyota mpya ya ndege"

Wakati huu bibi akakumbuka kuwa akiwa anadeki kule bwaloni aliokota nyoya la bata hivyo akatumia muda huo kama fursa ya kujiongezea maksi kwa mteja wake huyo mpya.

Bibi akamwambia, " Mjukuu shika nyoya hili haraka maana inaonyesha hivi karibuni utapata safari ya ndege na mpenzi wako wewe hayuko katika mji huu yuko huko ughaibuni na kwa msisitizo wa kuonyesha kama lugha inapanda akasema yuko ABROAD na kusindikiza kwa lugha ya kizambia WAUMFWA UMWANAKASHI (yaani umenielewa msichana).

Binti huku akionesha dalili za kuogopa na macho yake yakionesha kuwa ujasiri ulianza kumnyemelea alidakia na kusema, 

" Ni kweli bibi waweza kuwa unasema ukweli kwani hata hivi karibuni nilivyoomba mkopo ili na mimi nisafiri kwenda nje kufunga mali za duka nilipata kwa haraka sana tofauti na wenzangu ambao mpaka sasa hawajapata"

Bibi alidakia kwa lugha ya kigeni akisema " Ndefwaya one zali, Ndefwaya one zali,Ndefwaya one zali,Ndefwaya one zali,Ndefwaya one zali," na binti kwa hofu zaidi akauliza ni nini unaniambia bibi mbona sikuelewi?

"Ni mizimu hii mjukuu inataka utoe shilingi laki moja kwa ajili ya mimi kukuchimbia dawa ya wewe kutimiza ndoto zako na siku utakapoenda kuchua pasipoti yako uipate kwa haraka na huyo mpenzi wako wa ughaibuni akutambue mapema" bibi aliongeza kwa ujasiri mkubwa.

Binti akasema, " sasa ni usiku muda huu kwanini usiende kulala nyumbani kwangu ili asubuhi nikupe?" 

"hapana mjukuu,  mizimu yangu hainiruhusu kulala usiku huu kwani muda huu unaponiona nipo ON DUTY, na pia mizimu huwa haipokei fedha mkononi si nimekuona una kilonga longa hapo?." aliuliza bibi

Ndio nina kilongalonga naomba unipe namba yako nikurushie kwani watumia mtandao gani? 

Bibi akadakia usiniulize mtandao wewe chukua namba hii na kisha rusha haraka na kumbuka wakati unarusha uwe unasema maneno haya, " TIKISA MDODO!, TIKISA MDODO!, TIKISA MDODO!, TIKISA MDODO!,  mpaka pale unakapomaliza kuirusha.

 Na wakati huo mimi nitakuwa nimeondoka na hilo nyoya kila mara ukipata tatizo utaliweka sikioni na ukiona unasisimka ujue ndio TIKISA MDODO amekuja kufanya kazi yake. Alimaliza maneno hayo bibi gusa unate huku akianza kuondoka.

Bibi aliondoka kutoka eneo lile na baada ya umbali kidogo akajificha na  kisha akawasha simu na kupokea ujumbe kutoka kwa yule dada kuwa ametumiwa shilingi laki moja na nusu na meseji kutoka kwa dada ikisema, " Asante sana bibi kweli wewe umetumwa na wenye nia nzuri na mimi na pia asante kwa hili nyoya kwani hapa nimejaribu kidogo tuu kuligusisha sikioni nimeona TIKISA MDODO! akianza kufanya kazi asante"

Bibi gusa unate alicheka mpaka akaka chini na kisha akasema I AM A PROFESSIONAL  HEALER  na kisha akanyanyuka na kwenda mtaa wa pili na kuiona nyumba moja ya kulala wageni yenye bango lililoandikwa TANDIKA TULALE GUEST HOUSE.

Akaingia ndani na kuchukua chumba na kisha kumwita mhudumu kwa sauti ya juu yenye amri na kusema kuwa " weee kamtu nilitee vyombo hapa nianze kazi" binti yule alisindikizwa na kofi moja la mgongoni huku bibi akisea "acha kushangaa predeshee nimeingia hapa ndani"

*********************************************************************************************

Saa tisa kamili za usiku baba pachu akiwa amelala na kazidiwa kwa usingizi na dawa zikiwa nimemchosha mama pachu aliamka na kukaa kitandani na kuanza kuwaza mambo mengi juu ya simu ya mumewe na jinsi ambavyo hapo karibuni mambo yamekuwa yakibadilika.

Makubaliano ya wawili hawa kwenye mahusiano yao toka enzi hizo ni kwamba walikuwa hawana utaratibu wa kupekuana kwenye simu na kuwa kila mtu awe mwaminifu kwa mwenzie na simu ya mtu ibaki kuwa yake ama aitumie kwa uhuru usioweza kuidhuru familia au kuhatarisha ndoa yao.

Lakini wakati huu mama pachu alifikia hatua ya kukosa imani kabisa na mmewe kwani tabia ya kupigiwa simu nyakati za usiku na kukimbia kwenda kuipokelea bafuni au nje au hata kujifanya natoka kwenda bar kupata moja baridi  zilianza kumtia wasiwasi mama pachu.

Akiwa katikati ya mawazo hayo akapata wazo la kuiiba simu na kwenda nayo chumba cha pachu na kuanza kuipekua. Aliipekua ile simu kwa muda mrefu na hakukuwa na meseji yoyote ile mbaya zaidi ya meseji kutoka kwa mwakibubu wakitaniana na nyingine za mwarafiki wengine.

Ghafla simu ikaanza kuita na kwa ujasiri ulioendana na wivu akaona namba hii ngeni lazima ni ya mchepuko hivyo akaipokea na kuisikia sauti ya kike na kwa jazba mama pachu akasema, 

" Wewe ni nani unayempigia mme wa mtu simu usiku wote huu, ,hebu achana na kafanye umalaya wako mbele ya safari nyang'au mkubwa wee, mwana mtoka pabaya usiye na heshima wala haya kwa waume za watu, PUMBAVU"

Muda wote huo mpigaji hakuongea neno lolote zaidi ya kusikiliza jinsi mama pachu alivyokuwa akitweta kwa hasira. Mara hii mpigaji akamuuliza "umemaliza wewe mwanamke?"

Ule moto wa mama pachu ukapungua makali na kwa upole akadakia " Unasemaje sasa? kama ukweli nimeshakwambia huyo ni baba wa familia.

 "Mpigaji akajibu kwa kebehi, " Baba wa familia si kalala? Inaonesha wewe una appetite ya kupokea simu sasa nitakupigia kwenye namba yako ili tuongee vizuri, lakini sasa hivi wewe nenda kalale"

Mama pachu akamwambiwa huwezi kuwa na namba yangu wewe janamke wala usinitishe kwa lolote. 

Mpigaji akasema huku akikata simu, " Nimekwambia nenda kalale"

Mama pachu huku akianza kuwa na hofu akarudi chumbani na kuifuta ile simu iliyopigwa na kisha akalala. 

Asubuhi mama pachu aliamka kwa kuchelewa na kumkuta baba pachu akiwa kakaa sebuleni akisubiri kwenda hospitali. Basi mama pachu akachukua simu yake na kuona kuna missed calls 8 na meseji 3 moja kati ya meseji hizo zilimfanya mama pachu akimbie haraka na kwenda nje.

Meseji hiyo iliandikwa.........................................................................

Je meseji hiyo iliandikwa nini? na je huu ndio mwanzo wa sakata kumwangukia mamapachu?

Usikose kisa hiki kesho  jioni

MUHIMU

Kwa msomaji wa simu ya ajabu aiishie Mbeya jumamosi hii tutakuwa na cake nyingine kama hii pale hoteli ya penge kuanzia saa saba mchana mpaka saa mbili kamili za usiku kwa kiingilio cha shilingi 5000 tu.

Karibu ushiriki nasi katika burudani hii ukiwaona live kina mwakibubu, baba pachu, mama pachu, mama amigo, bibi gusa unate na marafiki wengine wengi amabao ni wasomaji wa hadithi hii.

Pia kama una birthday yako kutakuwa na zawadi nyingi za kushtukiza.

Wasiliana nasi kwa namba 0713317171 whatsapp au piga namba 0654690368 ili kupata tiketi yako mapema kwani nafasi ni kwa watu 30 tu

Karibuni.

You Might Also Like

0 comments: