Mwanamke aliyedhamiria kumpa limbwata mmewe aumbuka hadharani

13:41:00 Unknown 0 Comments


Aisee unajua sikuwahi kuwa na mwanaume mpole kama mme wangu?
Na tangu tuoane ilikuwa sasa imeshatimia miaka mitatu sasa na nzuri zaidi ni kwamba haikuwahi kutokea akanichapa vibao au kunitukana hata kunisema zaidi ya kunipenda na muda mwingi tulikuwa tukitoka wote.
Wakati huo mimi nilikuwa nina biashara yangu pale nyumbani ya duka la nguo ambayo haikunifanya kuwa busy sana na yeye aliajiriwa katika shirika moja la kijamii ambalo mara kwa mara walisafiri kwenda vijijini kuhudumia wananchi.
Kuna tabia hapa katikati aliianza kiukweli kunipa wakati mgumu kuivumilia hasa tabia yake ya kurudi kutoka kazini na hata housegirl akimpa chakula hali na mimi nipo dukani chumba cha nje na wala haji kuniona na kuondoka zake kwenda kwenye pombe.
Akirudi anakuwa kalewa na ni usiku na ule muda wa kula chakula anakuwa hana na kama haitoshi kunakuwa na ugomvi mkubwa sana kati ya mimi na yeye na kuishia kupigana na mwishowe analala sebuleni wakati mwingine na kuna baadhi ya siku nikiamka nagundua alishaondoka kwenda kazini.
Maisha yakawa magumu na kama haitoshi upendo na ule mshikamano wa kwanza ukapotea ikawa ni kulia kila siku na mme wangu akinipa mawazo mengi labda kapata mchepuko au laa!!!!!!.
Nikaamua kwenda kwenda kwa rafiki yangu mmoja aitwaye Salome na akaniambia kuwa ana dada yake aitwaye selina anamfahamu mganga wa jadi ambaye huwasaidia watu wenye matatizo ya ndoa.
Baada ya kumwambia Selina akaniambia jumamosi moja atanichukuwa na kunipeleka kwa mganga huyo. Jumamosi ilipofika tukaenda mpaka kwa mganga naye akanisikiliza na mwishowe akanipa dawa.
Dawa zile zilikuwa za aina tatu tofauti, ya kwanza nitaiweka mdomoni kaila arudipo usiku nisiongee kitu dawa ile ikiwa mdomoni, na ya pili ni ya kumwekea kwenye maji ya kuoga na chai kabla ya kwenda ofisini na kuhakikisha nambebembeleza anywe na na chakula kila arudipo kutoka kazini.
Na ya tatu ni ya kuhakikisha naitumia katika kufulia kwenye nguo zake na hasa kuhakikisha naziweka pia wakati napasi nguo zake na onyo ni kwamba asifanye mtu mwingine zaidi ya mimi na asinione mtu nikiwa nafanya hivyo na nitafanya hivyo kwa miezi miwili mfululizo.
Mwanzoni iliniwia vigumu ila niakajikuta nazoea na wakati huu akawa akirudi ule ugomvi haupo tena zaidi ya salamu nami naogopa kusema kwani dawa ingeonekana, chakula cha asubuhi na jioni arudipo kutoka ofisini maji ayakiwa tayari na anaoga.
Nguo zake nikawa nahakikisha nazifua na hata kuzinyoosha mimi na ile tabia ya housegirl kuingia chumbani kwetu kufanya usafi nikaipiga marufuku ili asije ona dawa nilikozihifadhi.
Taratibu mme akaanza kuacha kwenda kunywa pombe na kama akitoka basi tuko pamoja na hata ikitokea yuko peke yake basi atawahi kurudi tofauti na zamani na ugomvi ukawa umeisha kwani muda wote sikuwa mtu wa kuongea sana nikihofia dawa kuonekana mdomoni.
Miezi mitatu baadae nikaenda kwa mganga ili aniongeze dawa kwani iliisha ndipo nilipogundua kuwa ninauwezo wa kukimbia kwani alinichapa viboko viwili na kuniambia hebu niondoke ... alichonipa yalikuwa ni maji ya kawaida ya mdomoni na manukato ya kuweka kwenye maji ya kufulia na sabuni ya harufu nzuri kwenye maji ya kuogea na ile kwenye chakula ilikuwa ni viungo vyenye harufu nzuri vya kunukisha chakula...
Haki ya nani tena nikaacha tabia ya kuropoka arudipo usiku, kutomjali na kujisahau kama zamani, kumtumia house girl kufua mpaka kofuli zake ....Na sasa maisha ni mazuri.
Mapenzi hayana uchawi wapendwa.

Posted by Fred Kihwele · 1 hr · 
Semina kubwa ya wanawake wajasiliamali itafanyika katika ukumbi wa Jk Nyerere international conference wakina mama wote mnakaribishwa kujifunza jinsi kuboresha biashara zetu itakua tarehe 1/3
Semina kubwa ya wanawake wajasiliamali itafanyika katika ukumbi wa Jk Nyerere international conference wakina mama wote mnakaribishwa kujifunza jinsi kuboresha biashara zetu itakua tarehe 1/...
KARIBUMBEYA.COM
28 people reached
Like ·  ·  · 3
Posted by Fred Kihwele · 4 hrs · 
MWISHO WA UMASKINI NDIO MWANZO WA UTAJIRI
Niwakati wako sasa ndugu yangu kuweza kuyabadili maisha yako,kwa kusema umaskini sasa basi. Nataka nikwambie ndugu yangu mpendwa,ulimwengu wa leo unaendeshwa na watu wenye pesa na sio maskini. Ungana na mimi kwa Tsh 26,000/= tu nikuonyeshe jinsi inavyoweza kubadili maisha yako. Dunia hii ya karne ya 21 imetawaliwa na biashara nyingi zinazo fanyika kwa njia ya mtandao.
MWISHO WA UMASKINI NDIO MWANZO WA UTAJIRI Niwakati wako sasa ndugu yangu kuweza kuyabadili maisha yako,kwa kusema umaskini sasa basi. Nataka nikwambie ndugu yangu...
KARIBUMBEYA.COM
16 people reached
Like ·  ·  · 3
Posted by Fred Kihwele · 21 hrs · 
NAFASI ZA MASOMO – MARCH INTAKE 2015
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) (INCORPORATED BY ACT OF P...
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: