Tabia ya kukubali wanaume ovyo kwenye basi yamtokea puani binti huyu
Huwa napenda sana kukaa siti za mbele nikiwa safarisi kwani huwa naogopa sana kuna gari linvyokimbia au kukata kona kwa spidi kali, yaani huwa nachanganyikiwa na kuhisi kama vile ajali ileeeee.Siku hiyo niliwahi sana pale ubungo na kukata tiketi yangu na nikapewa na kwenda moja kwa moja basi lilikopaki na kuingia ndani. Nikawa busy kwa dakika kama kumi nikiweka mizigo yangu na na kutoa simu yangu tayari kwa kupata burudani.
Nilishangaa kuona mpaka muda wa basi kutaka kuondoka abiria tulikuwa wachache sana hivyo nikamfuta dada mmoja ambaye ni mhudumu wa gari hilo na anakiambia kuwa gari hilo lilitakiwa kuwahi tunduma mbeya ili kesho yake lirudi na abiria kwani basi la huko lilipata ajali.
Kweli safari ikaanza na ndani ya basi tulikuwa kama watu 15 tuu, nikaona nijivute mpaka siti ya nyuma na kuwa busy na mambo yangu. Muda mfupi nilipitiwa na usingizi na nilipokuja kushtuka pembeni yangu alikaa kijana mmoja mabaye kiukweli alikuwa handsome sana.
Hi, Naitwa Failiun, ( nilimpa salamu huku nikiona aibu hasa nikifikiria kama aliniona nilivyokuwa nakoroma)
Naitwa Aaron
Umekaa hapa muda mrefu sana, maana nimelala sana, ( niliona nimuulize ili kujipa matumani hakushuhudia shuzi kadhaa nilizoziachia wakati nalala maana na jana yake usiku nilikula mayai ya kuchemsha)
Noo sio muda sana ila nilikusaidia kufungua na dirisha kidogo maana niliona tumbo lako linaunguruma kidogo. ( alijibu kaka yule na kunifanya nicheke kidogo na kisha tukandelea na maongezi kwa muda kidogo.)
Aaron alikuwa na hadithi na vioja sana mpaka ikafika kipindi nikajikuta kwa bahati mbaya nimemkiss tukiwa siti ya nyumba ambako hakuna mtu aliyegundua kwani wengi wa abiria walikuwa wamelala.
Baada ya ile kiss alinipa zawadi ya juice moja ambayo baada ya kuinywa nililala usingizi mmoja mzito sana. nilipokuja kuamka tulikuwa tuko makambako na nilipoangalia pembeni yangu yule kijana hakuwepo tena.
Nilijaribu kumuuliza yule mhudumu wa basi kama kuna mtu alishuka lakini akakataa na kila abiria niliyemuuliza kama alimuna yule kijana hakuna aliyesema kama alimuona na wala basi halikusimama.
Nikaona kama ni muujiza na nilipoenda kwenye begi langu lishtuka haraka baada ya kuona mfuko nilio weka nguo zangu za nagani tu ndio ulikuwa haupo kwani ulikuwa juu na vingine vipo.
Nikamwita muhudumu na kumwambia ila akanihakikishia labda ni uchovu tuu ila hakuna kitu kama hicho labda nilisahau nyumbani. Safari iliendelea ila wakati huu nikachukua begi langu na kuchukua vidonge viwili vya dawa ya usingizi lakini havikufanya lolote.
Tulifika tunduma saa nne ya usiku na kwa kuwa nilikuwa mgeni nikaona nitafute hoteli nilale. Nilipifika pale nikaenda bafuni baada ya kuweka mizigo yangu na nilipotoa bafuni nilishtuka kuona ule mfuko wa chupi zangu uko pale kitandani.
Nikawa najiuliza umekujaje malango nilifunga na hakuna aliyebisha hodi, lakini akili ikanijia labda nilikuwa nimebana sehemu umeanguka wakati naweka mizigo.
Nikaondoka na kwenda zangu bar ambako nilipiga mitungi bila break ili nisahau mkasa huo na kujisemesha kuwa siku ya pili nitatakiwa kwenda kucheki malaria kwani inaweza kuwa inaninyemelea homa.
Niliporudi chumbani niliufungua mlango na huwezi amaini mtu yule aliyejiita aaron alikuwa kitandani. Nilishtuka nikapiga kelele kwa sauti kubwa lakini haikutoka na yeye akakaa kitandani akinicheka.
" huna ujanja mama wewe tulia tuu na ufuate malekezo yangu" alionge akijana huyo huku akitoa kitu mfukoni kilichonifanya nigundue kuwa ilikuwa ni kisu.
Alikinyanyua na kunifuta pale nilipokuwa na hata kabla ya kumchoma binti yule alishtuka na kugundua alikuwa ndotoni.
Hadith feki nimetaka kukufanya ufikirie mara mbili juu ya mtu unayejikuta unampenda ndani ya basi ndani ya siku moja........................
0 comments: