Binti akauficha uso wake na mkono wake na kusema " mimi mbaya huwezi kunioa"
Miaka mingi iliyopita kuna kijana mmoja alijikuta akimpenda sana binti mmoja kutoka familia ya kitajiri ingawa yeye alitokea familia ya kimaskini zaidi lakini wazazi wa binti walimpenda kijana yule.
Hivyo kijana akaona ni bora aonane na wazazi na binti na kuwaomba kuwa amchumbie mtoto wao. Kwa kipindi hicho wazazi hawakuwa na neno kwa kuwa waliona kijana anampenda mwanao wakakubaliana nae.
Ila kuna tatizo likajitokeza upande wa kijana: Kijana alikuwa ni mwanajeshi na katika nchi jirani vita ikawa imetokea na kijana anatakiwa kwenda vitani nje ya nchi kwa mwaka mmoja kama mlinda usalama.
Wiki moja kabla ya kuondoka kijana alimwendea binti yule mbele ya wazazi wake na kumpigia magoti na kumwambia, ". Je utakubali kuolewa na mimi?” Binti akafuta machozi na kusema " NDIO" na wakavalishana pete na kuahidiana kuwa baada ya kijana kutoka vitani wataoana.
Lakini kuna jambo la ajabu lilitokea siku chache baada ya kijana yule kuondoka, kwani binti alipatwa na ajali mbaya ya gari iliyomuumiza sana kichwa chake na kuacha majeraha mabaya sehemu nyingine za mwili wake.
Baada ya kukaa siku kadhaa hospitali akiwa hajitambui hatimaye alpata fahamu na kuamka na kuona baba na mama wakiwa pale wanalia. Kwa haraka akatambua kuwa kulikuwa na tatizo.
Baadae akagundua kuwa alikuwa kaumia kichwa na pia ubongo wake kama walivyosema madaktari na uso wake pia ulikuwa umeharibika sana na kuupoteza ule mvuto wake.
.Alilia sana alipojiona kwenye kioo na kusema, "ni juzi tuu nilikuwa nina uso mzuri, lakini leo natisha kama mdudu wa ajabu na mwili una majeraha ya kutisha"
Kuanzia hapo mpaka alipopona akawa kila mara akiomba avunje ahadi yake na mchumba wake. Alitambua kuwa kutokana na kuharibika kule ni dhahiri mwanaume yoyote asingetamani kuishi naye hivyo akataka amsahau na asimwone tena.
Kwa mwaka mzima kijana yule mwanajeshi alikuwa akiandika barua kwa binti lakini binti hakujibu na hata alipopiga simu binti hakupokea wala kumpigia.
Lakini baada ya mwaka kwisha kijana alirudi na alipoenda nyumbani kwa binti ili aonane naye binti alimwambia mama yake kuwa asimwambie kijana kuwa yupo ndani na hakutaka kamwe kuonana na yule mchumba wake.
Mama akamwambia, “Kijana amekuja kukuambia anatarsjis kuoa,” na akampa kati ya mwaliko
Binti alishtuka kwa kuwa alimpenda na sasa alikuwa akitaka kumsahau hivyo akaichukua kadi ile na kuifungua kwa uchungu mkubwa.
.
Na kashangaa zaidi kuona jina lake lipo mle ndani pia.!
Huku akiwa kachanganyikiwa akauliza, “ Hii nini?”
Hapo ndio kijana akaingia akiwa kashika maua na kupiga magoti pembeni yake na kuushika mkono wake na kumwambia, “Will you marry me?”
Binti akauficha uso wake na mkono wake na kusema " mimi mbaya huwezi kunioa"
Kijana akasema, “ Bila ya kibali chako mama yako amekuwa akinitumia picha zako , nilipokuona nikaona hujabadilika na bado ni mzuri kama binti yule niliyemwacha ambaye nina mpenda"
Kumbuka true love ipo SOMA COMMENTS
0 comments: