Mambo niliyojifunza na wewe hutakiwi kuyakwepa
Mambo niliyojifunzaNimejifunza kwamba pamoja na mambo yalivyo magumu, au jinsi unavyoumizwa ila Maisha yanaendelea na kesho yaweza kuwa bora kwako.
Nimejifunza ni jinsi gani mtu anaweza kukazana kuongelea mambo na matatizo ya wenzie na kujisahau kuwa naye ni mzigo kwa watu.
Nimejifunza ya kuwa pamoja na kuwa na mahusiano mabaya au mazuri na wale tuwapendao hasa wazazi, siku wasipokuwepo hapa duniani utawakumbuka na kutambua michango yao kwako, hivyo wapende wakiwa hai.
Nimejifunza ya kuwa mahangaiko ya kutengeneza Maisha ni tofauti na kuishi, hivyo watakiwa ukumbuke unatakiwa kuishi.
Nimejifunza ya kuwa Maisha hukupa mtu nafasi ya pili ya kujaribu baada ya kushindwa ile ya kwanza.
Nimejifunza hutakiwi kujiingiza katika mambo mbalimbali ukiwa mzima mzima, hivyo tukumbuke kina cha maji hakipimwi kwa miguu miwili.
Niimejifunza ukiamua jambo kwa moyo wako wote basi matokeo yake huwa mazuri na ya kuuridhisha moyo wako.
Nimejifunza ya kuwa pamoja na maumivu ya dunia hii sitakiwi kuwatangazia walimwengu wajue mapito yangu.
Nimejifunza kuwa ni rahisi kupata marafiki wapya lakini ni vigumu kuishi na marafiki zako wote.
.
Nimejifunza kuwa bado nina safari ndefu ya kujifunza mambo mengi maishani.
Nimejifunza kuwa ukifanikiwa kuisoma post hii na kisha kulike Karibu Mbeya basi utanifanya nifurahi.
0 comments: