Jinsi ya kulifanya tangazo lako livutie wanunuzi kupitia karibumbeya.com

10:42:00 Unknown 0 Comments

Jinsi ya kulifanya tangazo lako livutie wanunuzi kupitia karibumbeya.com
1. Mwekee mteja wako mazingira ya kukuamini
Unapoweka tangazo lako katika tovuti ya karibumbeya.com ni vyema kujua kuwa watu wengi hapa nchini bado hawaamini sana biashara ya njia ya mtandano.
Hivyo ni vyema kuwa makini na mwenye kumsaidia mteja wako kujenga imani na wewe kwa kuweka taarifa sahihi juu yako na bidhaa husika. Ni vyema kuweka taarifa ya sehemu uliko, mawasiliano sahihi, kutotumia majina ya utani, au hata kutoweka taarifa sahihi juu ya bidhaa yako au huduma uitoayo.

2. Msadie mteja wako
Wateja wengi wanashindwa kununua bidhaa au huitumia huduma yako kwani hawana uelewa wa kutosha juu ya huduma yako. Matangazo mengi huwa na maelezo yasiyojitosheleza kwa wateja hasa kwa bidhaa au huduma mpya.
Kwa kuandika maelezo yaliyojitosheleza kutamsaidia mteja wako kuifurahia huduma yako jambo ambalo hata kwako ni njia nzuri ya kuongeva kipato na kupitia hilo unajitangaza pia kwani mteja anakuwa balozi wa huduma yako kwa kuwa sasa anaielewa.

3. Weka picha kubwa na zenye uhalisia, rangi za kuvutia na zinazojieleza
Katika utafiti tulioufanya tumegundua kuwa kwa kutumia picha zenye kujieleza na kuvutia huwa na watembeleaji wengi zaidi kuliko matangazo mengine
Idadi kubwa ya wanunuzi huvutiwa sana na picha za bidhaa na kulichagua tangazo husika ili wasome zaidi. Kutokana na tangazo lako kuwa la kuvutia utasababisha idadi kuwa ya watembeleaji ambao tunaamini kuwa watabadilika na kuwa wateja wako

4. Kuwa na mpangilio mzuri wa malezo ya tangazo lako
Jinsi ya kulifanya tangazo lako livutie wanunuzi kupitia www.karibumbeya.com 1. Mwekee mteja wako mazingira ya kukuamini Unapoweka tangazo lako katika...
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: