Je mwanamke kamaa huyu tumpe jina gani la kumfaaa...

11:38:00 Unknown 0 Comments



Mama mmoja aitwaye Mary​ yeye alikuwa ni mcha Mungu sana na aliamini kuwa kamwe Mungu hawezi kumwacha katika kila jaribu na mapito ya kidunia.

Mary alikuwa anakaa kijiji kimoja kilichokuwa kimezungukwa na ziwa kubwa na mara kwa mara walipatwa na mataatizo ya mafuriko lakini alisali na kumwomba Mungu na akaweza kuokoka katika kila furiko hata kama lilichukua maisha ya watu wengine.

Siku moja mvua kubwa ikaanza kunyesha  na kila dakika ikaonekana kuwa ni kubwa zaidi ya hapo awali. Watu wakaanza kukimbia kutaka kujiokoa lakini yeye akabaki ndani akiamini kuwa Mungu hatamwacha afe.

Maji ya mvua yakazidi kuingia mle ndani mara yakaanza kulowesha baadhi ya vitu lakini yeye akabaki akiamini Mungu atamwokoa kwa muda muafaka. 

Mara maji yale yakamfikia magotini na na kuna watu wakaja na boti ili kumwokoa lakini yeye akakataa akaiamini Mungu tatmwokoa kwa muda muafaka na boti ile ikaondoka.

Maji yalipozidi akachukua koti lake la mvua na kupanda juu ya paaa na kukaa huko. Ikaja helkopta ya uokozi lakini bado alikataa kuondoka kwani alijua kuwa Mungu atamwokoa.

Basi mvua ikazidi na baadae mary akafa kwani maji yalifika juu ya paa na nyumba ikawa imefunikwa na maji na hakuna kwa kukimbilia na hakuna mtu aliyekuja tena kumwokoa kwani watu walikimbia eneo hilo.

Mary akajikuta yuko mbinguni yuko na Mungu, mary akamuuliza mungu " Baba mbona nilikuwa nikisali na kukuomba nikijua utakuja kuniokoa na haukuja mpaka nimekufa"

Mungu akamjibu, " nilikuletea boti ya uokozi ukakataa, nikakuletea helkopta nayo ukaiacha iende ulitaka nikusaidie kipi tena mwananagu"

Mary akabaki akiwa analia na hakuna tena namna ya kurudi duniani.

Watu wengi tumekuwa tukimwomba Mungu atupe baraka fulani katika maisha yetu lakini bahati hizo zimekuwa zikitujia lbila ya sisi kuona kama ni bahati.

Tunatakiwa kumwomba Mungu atupe pia na macho ya kuzitazama baraka hizo........ AM OUT

www.karibumbeya.com


Women resolution 2015
We are now in the third month of the year ,How far are you with your 2015 resolution
Are you facing challenges in growing your business? Would you benefit from peer support and the insights and experiences of successful women?
A call is now being issued to ambitious women who would love to participate in Women resolution 2015 event .
Women resolution 2015 We are now in the third month of the year ,How far are you with your 2015 resolution Are you facing challenges in growing your business? Would you benefit from peer sup...
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: