MAMBO KUMI YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANZISHA BIASHARA

11:43:00 Unknown 0 Comments


1) Fanya unalopenda
Unaweza kutenga muda mwingi na nguvu kwa dhumuni la kuanzisha biashara na kuitengeneza biashara iwe yenye mafanikio makubwa, hivyo ni muhimu sana kufanya jambo unaliolifurahia na kulipenda sana ikiwa ni uvuvi, ujenzi, ufugaji wa kuku, utalii na usafiri, mkahawa, ufinyanzi au kutoa ushauri wa kifedha.
2) Anzisha biashara yako wakati bado umeajiriwa.
Ni kwa kipindi gani mtu ataweza kuishi bila ya fedha? Sio muda mrefu. Utakuwa ni muda mrefu kabla biashara yako mpya haijaanza kutengenezea kipato. Kuwa mwajiriwa wakati unapoanzisha biashara kutakuhakikishia kuwa na kiasi cha pesa mfukoni mwako hivyo kuwa na uhakika wa kuendelea na biashara bila wasiwasi. Lakini pia hiki sio kikwazo bado unaweza ukaanzisha biashara ukiwa haujaajiriwa.
3) Usifanye peke yako;
Unahitaji mfumo wa kukusaidia wakati wa kuanzisha biashara (na pia baada). Mwana familia au rafiki ambaye mnaweza mkashirikiana kimawazo na kusikilizana vyema mpaka kiwango cha kuanzisha biashara hiyo hata ikiwa vyema unaweza kumtafuta mtu au shirika lenye uwelewa mpana au unaweza ukajiunga na mchakato wa kibiashara kama “biashara binafsi au ujasiria mali’’ (Start your Own Business SYOB) katika ofisi zetu au washauri wa kibiashara wengine walio karibu na wewe. Wakati unapoanzisha biashara ni vyema kuwatafuta washauri wazoefu wakusaidie katika mambo mbalimbali.
4) Watambue wateja au tengeneza wateja kwanza.
Usisubiri mpaka ufungue rasmi, kwa sababu biashara inawategemea sana wateja. Tengeneza mtandao, fanya mawasiliano uza au toa huduma zako kwanza. Hauwezi kuanza kufanya masoko kwanza.
5) Andaa Mpango wa biashara.
Sababu kuu ya kuandaa mpango wa biashara kwanza wakati unawaza kuwa mfanya biashara ni kwamba utakusaidia kuwa makini usije ukapoteza muda wako na fedha zako kwa kuanzisha biashara isiyokuwa na mafanikio.
Kumbuka, si lazima kufanya kama ilivyo katika mpango wa biashara, kila biashara mpya ina wazo jipya linalokuja nalo. Kupitia mchakato wa Anzisha biashara yako Mapema na Zabeco (Zabeco’s Quick Start Business) itakusaidia kutengeneza wazo lako vyema.
6) Fanya utafiti
Utafanya utafiti sehemu mbali mbali katika kuandaa Mpango biashara, lakini huo utakuwa ni mwanzo tu. Wakati unaanzisha biashara, unatakiwa kuwa mataalamu katika tasnia yako, bidhaa na huduma kama hauko tayari. Kujiunga na tasnia kama hizo pia kabla haujaanzisha biashara yako ni wazo zuri sana.
7) Pata msaada wa kitaalamu.
Kwa upande mwingine, haimaanishi kwamba unatakiwa kujua au kuwa mtaalamu wa mambo yote. Kama wewe sio Mhasibu au mtunza daftari (book keeper)kodisha mmoja au wote. Ikiwa unahitaji kuandika mkataba na wewe sio wakili, ni vizuri ukamkodisha. Utapoteza muda mwingi na pesa katika kujaribu kufanya mambo usoweza au usoyajua kuyafanya.
8) Andaa pesa zako tayari kuanza biashara.
Kusanya au dunduliza pesa ikibidi ili kupata kiasi unachohitaji kuanza biashara hiyo. Fika kwa wakopeshaji na wawekezaji hisa mbalimbali ili kupata fedha kisha andaa mipango yako.
Usitegemee kuanzisha biashara kisha ndo uende benki kutafuta pesa. Wakopeshaji wa kawaida hawapendi mawazo mapya na pia hawapendi biashara ambayo haijajulikana kuwa na mafanikio.
9) Kuwa hodari wakati unapoanza.
Kila kitu unachotarajia na namna unavyofanya biashara inahitaji kuwaonyesha watu kuwa wewe ni mtaalamu na unaendesha biashara yako kitaalamu. Hii inamaanisha kuwa na vikorokoro vyote kama Kadi ya biashara (Business cards), Simu ya biashara, na barua pepe ya Biashara na uwahudumie watu kitaalamu na kwa nidhamu.
10) Pata mamlaka yote ya kisheria na mambo ya kodi mapema.
Ni vigumu na gharama sana kurejea utakapo kosea hili jambo. Jebiashara yako inahitaji kusajiliwa? Je utahitaji wafanya kazi? Je utatakiwa kuwa na bima na marejesho ya kodi pamoja na makato? Je aina yako ya biashara inaathiri vipi marejesho au faida yako ukilinganisha na hali ya makato au kodi?
Jifunze utaratibu wa ulipaji kodi na makato kabla ya kuanza kufanya biashara na ufuatilize kama utaratibu huo unavyo agiza.
I
Ukifuatilia ushahuri huo wakati wa kuanzisha biashara utakusaidia kiurahisi na kiufanisi na pia bila usumbufu katika michakato hiyo yote. Hivyo utakuwa na biashara ya kisasa na ya kitaalamu ya kudumu.
Wazo la siku “Ulafi wa kuanzisha biashara ni mzuri kuliko ulafi unaoanzishwa na biashara”

Unangoja nini?
Tumia muda huu kuintangaza biashara yako kupitiawww.karibumbeya.com na uungane na mamia ya wafanyabiashara na wateja kupitia mtandao huu.
Kumbuka ni bure na itakuwa bure daima
Karibu mbeya is a leading mbeya’s online site which provides you an opportunity to get several goods and services being available here in Mbeya and other neighboring places. Read more
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: