Mama akutana na mtihani wa mwaka.....
Mama mmoja alikuwa nyumbani peke yake mara mlango ukagongwa kuashiria kuna mgeni pale mlango.Alipoufungua mlango alikutana na mzee mmoja, "karibu ndani" aliongea yule mama. " Asante mme wako yuko ndani" alihoji yule mzee. Mama akamwambia kuwa mme hayupo na akamkaribisha ndani.
Mzee akakataa " niko na wenzangu hivyo tutakaa nje mpaka mmeo akirudi" aliongea mzee huyo huku akiwaonesha wazee wengine wawili waliokuwa nje ya geti.
Jioni mme alirudi na mama akamsimulia juu ya wazee wale, mme akashtuka na kwa sauti akamwambia " waite haraka tatuwezi kukaa ndani na kuwaacha wazee wakipigwa na baridi ndani.
Mama akaenda na alipowakaribisha ndani kuwa mme karudi mmoja kati ya wazee wale akasema, " mama hatuwezi kuingia wote kwani mimi naitwa Upendo na wenzangu ni Utajiri na Mafanikio.
Hivyo anatakiwa kuingia nyumbanni kwako mmoja tuu, nenda kaongee na mmeo na muone ni nani mtamkaribisha"
Mama akarudi na kumsimulia mmewe na kisha akamwambia, "mimi nafikiri tumkaribishe mafanikio kwani utapandishwa cheo ofisini amabcho umekuwa ukikihangaikia kwa muda mrefu na mambo yatatunyookea"
Ingawaje na mme naye akafikiri na kumwambia, "mpenzi wangu, nimekuwa nataka kupandishwa cheo ili nipate marupurupu mengi na kuwa matajiri. Hivyo tukimkaribisha utajiri sitakuwa na haja tena ya kutaka kupandishwa cheo kwani tutakuwa matajiri, nafikiri utajiri ni chaguo sahihi"
Moto wao wa kike alikuwa akiwasikiliza hivyo nae akaongea, " mama na baba, hapa nafikiri tuchague upendo, kwani tukiwa na upendo hatutakuwa na muda wa kuhangaikia utajiri na mafanikio kwani mafanikio yatakuwa ndani yetu kutokana na upendo"
Wazazi wakafikiria kwa muda na kuona ni bora waafikiane na wazo la mtoto wao hivyo mama akatoka nje na kwenda kumwita yule mzee aliyejitambulisha kwa jina la upendo.
"ok, tumejadiliana na kumchagua upendo aje nyumbani hivyo naomba usimama na uje ndani karibu" Upendo akasimama na kuanza kuongoza ndani lakini alipokuwa anaufuata mlango mama akaona na wale wazee wengine nao wanamfuata.
"ngoja kwanza, nimemwita upendo lakini mbona na wengine wanakuja" alihoji mama yule kwa mshangao.
Upendo akasimama na kwa upole akamjibu mama " kama ungecaguo utajiri au mafanikio angeingia mmoja, lakini kila aendapo upendo lazima utajiri na mafanikio nao waje"
Mafanikio huja pale ambako kuna amani, upendo, uelewano ndani yetu na nje yetu na kama tutafanikiwa kuzifanya familia zetu kuwa na amani, upendo, uelewano ndani yetu na nje yetu, upendo kwa Mungu, upendo baina yetu, upendo kwa jamii, upendo kwa binadamu basi kupitia upendo huo tutajikuta tukiwa mafanikio kila siku
Nimesahau sijui nilikuwa naandika nini
Soma Comments
0 comments: