Mende kidogo asababishe kifo muda huu

14:55:00 Unknown 0 Comments



Siku moja nilikuwa katika hoteli moja maeneo ya uswahilini hapa mbeya.Kuna mende mmoja mkubwa akaruka kutoka kusikojulikana na kumrukia binti mmoja.

Ghafla yule binti akaanza kurukaruka na kupiga kelele za hofu zenye kuashiria kuwa alihitaji msaada.

Jitihada zake za kumtoa yule memde ziliendelea huku akiwa anatetemeka na kuirusha mikono yake na kujipukuta kwa muda.

Meza ile waliyokuwa wamekaa wale mabinti na hata meza jirani watu wote wakawa na hofu huku na wengine wakionesha kutaka kukimbia na wengine wakipiga kelele pia.

Mwishowe mende  akaruka na kwenda kumwangukia binti mwingine ambaye walikuwa wamekaa nae pale.

Sasa, ikawa ni zamu ya binti mwingine kuendelea na sakata lile huku kelele sasa ikiwa kubwa zaidi.

Mhudumu wa hotel akaja haraka na kutaka kumsaidia lakini akiwa bado hata hajatoa  msaada mende yule akamrukia sasa mhudumu.

Mhudumu akasimama kwa ujasiri na kumtazama yule mende aliyekuwa  kwenye shati lake  kwa umakini.Baada ya kuwa na uhakika na yule mende huku amejiandaa akamshika mende yule na kumtupa nje ya hoteli hiyo na amani ikarejea tena pale hotelini.

Nikanyanyua glass yangu ya juisi na kuangalia mshangao uliokuwa pale hotelini kwa kila mmoja, mara antena zangu kichwani zikanipeleka kwenye dimbwi la mawazo yaliyofuatiwa na mchanganuo wa hapa na pale na nikaanza kushangaa kama kweli ni mende aliyesababisha hali ile pale hotelini au laah?

Kama ni ndio, basi kwa nini mhudumua hakupiga kelele wala kusumbuliwa na na mende yule?

Alifanikiwa kumtoa nje bila hata ya kuwa na kelele palee ndani na hali ikatulia.

Tatizo sio mende, bali tatizo ni binti kushindwa kuhimili hofu na usumbufu uliosababishwa na mende ambaye alimfanya binti ashikwe na hofu.

Kupitia hilo nimejifunza kwamba, sio kelele za familia, boss wangu, jamaa na ndugu zinazonisumbua mimi, ila ni tatizo ni mimi kushindwa kuhimili kelele hizo na usumbufu wake unaonifanya mimi nipate shida.

Na kikubwa zaidi ni hatua ninazozichukua kwenye kukabili matatizo yangu ndio zinazonitengenezea matatizo zaidi katika maisha yangu na wanao nizunguka

Tunachotakiwa kukiweka kichwani zaidi

Tunatakiwa kuelewa kuwa hutakiwa kuwa na hofu au kuguswa katika maisha .

Tunatakiwa kila siku kukabiliana na hali zetu, wanawake walikosa ujasiri lakini mhudumu yeye alikabiliana tena kwa kujiandaa kwa ujasiri.

Kuguswa siku zote hukupa kuwa na hofu ambayo ukufanya kukosa ujasiiri lakini kukabiliana ni jambo jema ili kuokoa hali kutokuwa mbaya au kusababisha makubwa zaidi.

Daima epuka  nyufa katika mahusiano, kufanya maamuzi ukiwa katika hasira, kuwa na wasiwasi, msongo wa mawazo au haraka katika maisha

Jambo jema zaidi ni kuepuka kusoma habari hii

Soma  Comments

Women resolution 2015
We are now in the third month of the year ,How far are you with your 2015 resolution
Are you facing challenges in growing your business? Would you benefit from peer support and the insights and experiences of successful women?
A call is now being issued to ambitious women who would love to participate in Women resolution 2015 event .
Women resolution 2015 We are now in the third month of the year ,How far are you with your 2015 resolution Are you facing challenges in growing your business? Would you benefit from peer sup...
KARIBUMBEYA.COM

You Might Also Like

0 comments: